Rais mstaafu wa awamu ya pili wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaji Ali Hassan Mwinyi anaendelea kupatiwa matibabu ya kifua akiwa chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari bingwa
"Anaendelea kupatiwa matibabu na baadhi ya wakati anakuwa na uangalizi wa karibu sana wa madaktari na wamesema kwamba wataendelea kumpa matibabu kwa hapa, hakuna haja kwa sasa ya kumsafirisha labda kama wataona haja ya kufanya hivyo hapo baadaye kwa sababu na umri pia umesogea kidogo lakini mimi chakusema tu ni kwamba tumuombee mzee wetu, tufanye dua, tumuombee aweze kuimarika afya yake na aweze kutoka katika hali hiyo ya maradhi ili aungane na sisi tena tuendelee kupata faida kutoka kwake" -Dkt. Makame
Dkt. Abdallah Makame aliyekuwa Katibu wa Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi amezungumza hayo alipofanya mahojiano maalumu na Azam TV Februari 15.2024