Wataalamu wa Taasisi ya Ocean Road wafanya vipimo vya Saratani bure Mkoani Mara, Wababa waongoza kujitokeza

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road imeendelea na kampeni ya kutoa elimu, vipimo na matibabu ya Saratani katika mikoa mbalimbali Nchini Tanzania, ambapo safari hii timu yao imefika Mkoani Mara.

Wataalamu wabobezi wa Saratani ya Ocean Road wamewasili Mara tangu Jumatatu ya Juni 12, 2023 na watakuwepo hadi Ijumaa Juni 16, 2023.

Lengo la kampeni hiyo ni kuwafanya Wananchi wengi kuwa na ufahamu kuhusu Ugonjwa wa Saratani na kuwapa elimu jinsi ya kukabiliana na changamoto hiyo ya kiafya.

10657a27-1a7f-4ab8-9c61-1c1c0d7027bc.jpg

Afisa Mawasiliano na Uhusiano wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Islam Mposso anasema kampeni hiyo ya kuzinguka mikoani ni kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoa elimu na matibabu kuhusu Saratani katika mikoa mbalimbali hasa nje ya Dar es Salaam.

Amesema “Rais Samia alitoa maelekezo na kugharamia huu mchakato kupitia Serikali yake, ambapo tunatembea katika mikoa mbalimbali kufanya huduma hiyo bure kwa asilimia kubwa.

e35b53f3-95c3-40c3-8da8-2cc43c73ca58.jpg

“Kwa sasa tupo katika Hospitali ya Rufaa ya Mara, Wananchi wanapokuja kwenye huduma zetu katika maeneo tunayotembelea huduma inakuwa ni bure tofauti na wanapokuja ofisini.

“Tunawasaidia kuwapunguzia gharama kubwa ambayo ingewafanya watoke mikoani na kwenda Dar es Salaam.”

Huduma wanazotoa mikoani
Kuna huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo lakini kubwa ni Satarani mlango wa kizazi, Saratani ya Matiti na Saratani ya Tezi Dume.

1490a605-fa77-4fe0-8934-19a2b6564dce.jpg

Watu wanaojitokeza kwenye huduma
Mposso anasema “Mwitiko ni mkubwa, asilimia kubwa ya walioanza kujitokeza mwanzoni ni Wababa lakini baadaye ni kakawa wanawashawishi wanawake nao kujitokeza, hivyo mwitikio ni mkubwa na watu wanaendelea kujitoeza.

“Pamoja na hivyo wapo ambao wanajitokeza wakiwa na changamoto nyingize na uvimbe ambao wanahisi unahusiana na Saratani, tunawafanyia vipimo na kuwapa majibu.”

09705b14-893a-4b50-8743-852b8cb8447d.jpg

Daktari anaelezea
Meneja wa Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani na Elimu kwa Umma, Dkt. Maguha Stephano anafafanua “Taasisi ya Ocean Road huwa tunatoa huduma mkoba zinazohusisha matibabu ya Saratani pamoja na uchunguzi, ni huduma za kibingwa ambazo badala ya kufanyika kwenye taasisi yetu pekee tunazunguka na kuzitoa katika Hospitali za Rufaa mikoani pamoja na zile za Kanda.

“Lengo la huduma hii ni kuongeza mwamko wa watu kujitokeza kupata vipimo pamoja na madaktari kuwa na uwezo wa kubaini dalili za awali za Saratani ili kuwawezesha kuwapa rufaa mapema Wagonjwa kwenda katika vituo vinavyohusika na Saratani.”

19319620-638b-44ca-8990-5f35954c124d.jpg

Wagonjwa wanachelewa
Dkt. Maguha anaeleza “Wapo wanaoamini kuwa ukitibiwa kwa mionzi basi unajitengenezea mazingira ya kupata Saratani jambo ambalo si la kweli kwa kuwa kuna watu wametibiwa Saratani ya matiti, mlango wa kizazi na walipona miaka mingi iliyopita.

f82837e3-08e7-4e54-ab86-89b7bc1b2122.jpg

0489c29b-9047-4d34-8702-6a7baae6cd15.jpg

Saratani inawaumiza watu wazima zaidi
“Saratani inawaathiri watu wa rika zote bila kujali jinsia lakini watu wazima wapo katika hali hatarishi zaidi ya kupata Saratani kutokana na umri.

Umri unavyosonga mbele ndivyo ambavyo uwezekano wa kupata Saratani pia unakuwa mkubwa kutokana na asili ya ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Saratani unatokana na mabadiliko ya chembechembe hai za mwili ambazo zinabadilia taratibu, mfano Saratani ya Mlango wa Kizazi mabadiliko yake ndani ya mwili yanaweza kutokea ndani ya kipindi cha miaka 10 hadi 20, ndio mtu anaanza kupata dalili za wazi.

Wanaume na Saratani ya Tezi Dume
Mfano wa Saratani ya Tezi Dume, Wanaume ambao wana umri wa miaka 50 na kuendelea wapo hatarini zaidi kuliko vijana wadogo.

Kawaida Mwanaume anapofikisha umri wa miaka 40 na kuendelea Tezi Dume yake huwa inaongezeka ukubwa pia kama mabadiliko yalianza kabla ya hapo, ndipo mabadiliko ya chembechembe hai yanapoongezeka kwa kasi.

Saratani ni ugonjwa unaotokana na chembechembe hai mwilini ambazo zinabadilika, nyingine zinakuwa nyingine zinakufa.

Madaktari bingwa Ocean Road
Tuna mashine ya PET-CT Scan ambayo inagundua saratani katika hatua za awali kabisa kuliko mashine nyingine, pia inafatilia mwenendo wa matibabu kwa wagonjwa waliopata matibabu.
 
Madaktari bingwa Ocean Road
Tuna mashine ya PET-CT Scan ambayo inagundua saratani katika hatua za awali kabisa kuliko mashine nyingine, pia inafatilia mwenendo wa matibabu kwa wagonjwa waliopata matibabu.
Huu uzi muhimu sana ila sioni wachangiaji zaidi ya mimi na mleta mada
 
Back
Top Bottom