Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Amesema “Napenda kuwajulisha Wanaume kuwa tunafanya uchunguzi wa Magonjwa hayo katika huduma zetu hapa Singida, zinafanyika kwa njia rahisi kama vile tunavyopima Malaria na majibu yanapatikana ndani ya muda mfupi.”
Amesema hayo akiwa Mkoani Singida ambapo Taasisi ya Ocean Road inafanya Kampeni ya kutembelea Hospitali za Rufaa za Mikoa ili kushirikiana na Wataalam mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha elimu inawafikia watu wengi zaidi kuhusu Ugonjwa wa Saratani.
Ameeleza kuwa huduma hiyo ya vipimo na elimu kuhusu ugonjwa huo katikakampeni yao hiyo Mkoani Singida ilianza kutolewa Alhamisi ya Septemba 21, 2023 na inatarajiwa kumalizika Jumapili Septemba 24, 2023.
Amesema “Lengo lingine la huduma zetu hapa ni kubadilishana uwezo kwa wataalam, kugundua Saratani mapema.
“Tunakumbushana na Wataalam kuwa wanatakiwa kutoa Rufaa mapema kwa kuwa ikigundulika mapema ni rahisi kupata matibabu.
‘Kwa kipindi cha Septemba 21 hadi 23 tumeona Wananchi 400 kati yao Wanaume ni 100 wakati Wanawake ni 300, kati yao zaidi ya watu 30 wameonekana kuwa na matatizo mbalimbali.
“Wanawake 6 wameonekana kuwa na viashiria vya Saratani, Wanawake watatu wameonekana kuwa na viashiria vya Satarani ya Matiti, sita wamegundulika kuwa na viashiria vya Satarani ya Mlango wa Kizazi.
“Pia kati ya Wanaume 100 waliopimwa, wawili wameonekana kuwa na viashiria vya Tezi Dume ambapo tumewaelekeza wafanyiwe uchunguzi zaidi na baadaye kwenda katika Taasisi ya Ocean Road kwa ajili ya matibabu zaidi.
“Ikumbukwe kuwa huduma hii tunayoitoa hapa ni bure kama ambavyo tunatekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu aliyotoa, hiyo pia inaambatana na huduma ya kumuona daktari bingwa, nawasisitiza watu wa Singida wana nafasi ya kuja kupata huduma ya vipimo bila malipo kwa kuwa Jumapili ya Septemba ndio itakuwa mwisho kwa hapa Singida.”