Hii kitu ni ovyo kabisa.
Mimi sina uhakika kama ilikuwa hiyo au kitu kingine. Nilipigwa homa kali. Koo kuwashwa, homa kali, kichwa, viungo kuuma, kizunguzumgu kikali ambacho nilikuwa sijawahi kushuhudia. Sasa nipo kazini lakini kuna muda nasikia kichomi upande wa kushoto mwa kifua. Sijui ni madhara yaliyosababishwa au ni tatizo jimhine. Na hapa ndiyo naona ubaya wa kuzuia watu kupimwa. Unabakia unahisi tu!
Lakini kwa ujumla, mwili upo fit kabisa. Hata wakati wa kuugua, hakuna kitu kiliniumiza kama kizunguzungu - maana siku kama 3 hivi, ilishindikana kabisa kutembea kwa kujitegemea.