Dkt. Janabi na Wanaharakati wa Afya tuache upotoshaji. Nchi ina tatizo kubwa la Utapiamlo na sio uzito wala unene

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,234
22,317
Leo ninaandika nikiwa na hasira zilizochanganyikana na huzuni kwa upotoshaji mkubwa unaofanywa na huyu daktari pamoja na madaktari wengine uchwara wanaolazimisha ionekane kuwa nchi ipo kwenye tatizo kubwa la unene uliopitiliza wakati ni kinyume chake.

Tumekuwa tukiwasikia msile wanga mara usikun kuleni tu matunda na maji mengi wakati wananchi wengi wanakula tu ili kuzuia msiba na sio kuzingatia mlo kamili kwasababu ya umaskini.

Hizo nguvu mnazotumia kwa ajili ya kikundi cha watu wachache mngetumia kuonyesha ukubwa wa tatizo la lishe kwa wananchi mngepata thawabu. Dr Janabi huna tofauti na mke wa mfalme wa Ufaransa aliyesema watu kama hawana mikate wale keki.

Kwa mujibu wa mtandao wa STATISTA hadi kufikia November 2021 kulikuwa na 31.8% ya watoto wa chini ya miaka miatno wenye utapiamlo uliokithiri (Chronic Malnutrition). Ni 4% tu ya watoto huzaliwa wakiwa overweight.

Kimsingi hivyo vyakula anavyosema Janabi watu wasile ni ndoto za watanzania wengi kuvipata angalau mara moja kwa siku. Mikoa mingi ya Tanzania inakabiliwa na tatizo la lishe. Ninachoona ni ndugu Janabi kudhani maisha anayoishi yeye ndo wanayoishi watanzania wote. ASIJISAHAU

Ninatoa wito kwa serikali za mitaa kupambana ili mashuleni watoto wawe wanapata chakula. Wale wazazi/ walezi wapumbavu wanaokataa kuchangia vyakula kwa kisingizio cha ELIMU BURE wakamatwe watupwe tu ndani maana wanaturudisha nyuma. Haihitaji utafiti kujua kama kuna tatizo kubwa la lishe karibu maeneo yote nchini.
 
Statistically unasema ukweli mkuu hawa watu wa world obesity federation wanasema Tanzania hata top 150 haipo, njaa ni kali sana mastaa tool yao ya global obesity obsevatory inasema tanzania ni ya 168 na ina percentage 4.16 kidunia, janabi huwa anatupiga fix alooh…
 
Attachments

  • 53B7B2D2-14DA-4C6D-AC43-FB5BE2C53F44.jpeg
    53B7B2D2-14DA-4C6D-AC43-FB5BE2C53F44.jpeg
    419.5 KB · Views: 4
Shida Janabi nae anataka kutrend kama wakina Umber au wasanii ndio maana sasa amenza kufanya siasa…

Yani Profesa mzima anajiingiza kwenye siasa za kijinga za kutudanganya eti uhaba wa sukari ni fursa kuimarisha afya? Hivi ni nani amemdanganya Janabi kuwa sukari inatumika tuu kwenye chai? Anajaribu kutudanganya kuwa yeye hanywi sukari au familia yake haitumii sukari?

Huyu Profesa Janabi amekuwa Profesa Janaba au Reprofesery….yani ni kama kaanza kuwehuka na ku trend yani kila siku anataka ku trend…..
Yani watu tuko kwenye shida kubwa ya sukari na upatikanaji wake yeye analeta mzaha….
Huyu ni mjinga mjinga kwa sasa
 
Mchawi huyu dokta uchwara, usimuone na koti lake lile la maigizo, he is a manipulative liar, a propagandist and a pawn of the powers that be.

Sauti yake ni ya maigizo. Hasemi ukweli.

Anarembua rembua tu na kutupiga fix za hapa na pale. A WITCH IN HOSPITAL UNIFORMS.
 
Shida Janabi nae anataka kutrend kama wakina Umber au wasanii ndio maana sasa amenza kufanya siasa…

Yani Profesa mzima anajiingiza kwenye siasa za kijinga za kutudanganya eti uhaba wa sukari ni fursa kuimarisha afya? Hivi ni nani amemdanganya Janabi kuwa sukari inatumika tuu kwenye chqi? Anajaribu kutudanganya kuwa yeye hanywi sukari au familia yake haitumii sukari?

Huyu Profesa Janabi amekuwa Profesa Janaba au Reprofesery….yani ni kama kaanza kuwehuka na ku trend yani kila siku anataka ku trend…..
Yani watu tuko kwenye shida kubwa ya sukari na upatikanaji wake yeye analeta mzaha….
Huyu ni mjinga mjinga kwa sasa
Na hizo siasa zake kwenye ishu ya sukari ndo zimenifanya niandike huu uzi.
 
Watanzania kawaida hawapendi kuambiwa mambo yanayokaraisha nafsi zao.....wao wanapenda kusikia mambo mazuri......na ndio maana wamekuwa fursa kwa wachungaji na mitume matapeli wanaowalisha maneno matamu huku wakivuna mamilioni.......

Prof Janabi kwa nafasi yake lazima awahusie watu juu ya madhara ya mitindo mibaya ya maisha kitu ambacho waTanzania hawapendi kukisikia....

Takwimu ziko wazi kuwa kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa maradhi hayo pamoja na mengine yanayohusiana na mitindo mibovu ya maisha.........na bahati mbaya kutokana na vipato vyetu kushindwa kumudu gharama za matibabu............

Sasa kwanini tusichukue tahadhari kabla ya hatari.........

Mkiambiwa na watalaamu mnaanza matusi na kejeli.......

Matumizi makubwa ya sukari, pombe Kali na pombe zingine na vyakula vya viwandani hatari kwa afya zetu.......

Inawezekana takwimu za obesity zisiwe kubwa kulinganisha na mataifa lakini kama taifa tunatakiwa kuchukua tahadhari ili tusifikie huko....kwa kuwa hata hao wenye takwimu kubwa hawapendi hali na wanachukua hatua kupambana na hali hiyo...........

Prof Janabi endelea kuwakumbusha hata kama hawapendi lakini iko siku watakumbuka maneno yako wakiwa vitandani.......
 
Leo ninaandika nikiwa na hasira zilizochanganyikana na huzuni kwa upotoshaji mkubwa unaofanywa na huyu daktari pamoja na madaktari wengine uchwara wanaolazimisha ionekane kuwa nchi ipo kwenye tatizo kubwa la unene uliopitiliza wakati ni kinyume chake.

Tumekuwa tukiwasikia msile wanga mara usikun kuleni tu matunda na maji mengi wakati wananchi wengi wanakula tu ili kuzuia msiba na sio kuzingatia mlo kamili kwasababu ya umaskini.

Hizo nguvu mnazotumia kwa ajili ya kikundi cha watu wachache mngetumia kuonyesha ukubwa wa tatizo la lishe kwa wananchi mngepata thawabu. Dr Janabi huna tofauti na mke wa mfalme wa Ufaransa aliyesema watu kama hawana mikate wale keki.

Kwa mujibu wa mtandao wa STATISTA hadi kufikia November 2021 kulikuwa na 31.8% ya watoto wa chini ya miaka miatno wenye utapiamlo uliokithiri (Chronic Malnutrition). Ni 4% tu ya watoto huzaliwa wakiwa overweight.

Kimsingi hivyo vyakula anavyosema Janabi watu wasile ni ndoto za watanzania wengi kuvipata angalau mara moja kwa siku. Mikoa mingi ya Tanzania inakabiliwa na tatizo la lishe. Ninachoona ni ndugu Janabi kudhani maisha anayoishi yeye ndo wanayoishi watanzania wote. ASIJISAHAU

Ninatoa wito kwa serikali za mitaa kupambana ili mashuleni watoto wawe wanapata chakula. Wale wazazi/ walezi wapumbavu wanaokataa kuchangia vyakula kwa kisingizio cha ELIMU BURE wakamatwe watupwe tu ndani maana wanaturudisha nyuma. Haihitaji utafiti kujua kama kuna tatizo kubwa la lishe karibu maeneo yote nchini.
Hata kwa macho tu ukiangalia utagundua watanzania wengi wamedumaa kwa kukosa mlo kamili na kwasasa ndo kabisaa familia nyingi ni milo miwili kwa siku.

Sema asilimia kubwa ya waTz hawana uzalendo ndo maana sishangai kuona upotoshaji ukishamiri hasa kipindi hiki.
 
Back
Top Bottom