Chanzo cha vifo vingi vya uzazi hiki hapa: Si afya mtoto kuzaliwa na uzito mkubwa

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
Hivi karibuni kumekuwa na mjadala mkubwa mitandaoni kuhusiana na watoto wanaozaliwa na uzito mkubwa. Mjadala huu umezuka baada ya Prof. Janabi kuelezea jambo hili wakati wa uzinduzi wa Foundation ya Prof J (Joseph Haule)

Jambo hili limeonekana kuzua taharuki kwa baadhi ya watu ikichukuliwa kuwa sehemu kubwa ya jamii yetu imejijengea dhana kuwa mtoto anayezaliwa na uzito mkubwa (bonge) ndiye mtoto mwenye afya njema na ndugu kumfurahia sana ilihali jambo hilo ni tofauti kabisa kwa wataalam wa afya.

Umakini huu unasababishwa na hofu juu ya yale yanayoweza kutokea wakti wa kujifungua na kuhatarisha afya ya mama na mtoto na afya ya mtoto mara baada ya kuzaliwa na afya yake ajapokuwa mtu mzima.Ili kuepuka hilo ni vizuri kufahamu jambo hili kwa undani na kuchukua hatua stahiki

Mtoto anayezaliwa na uzito mkubwa (Macrosomic baby) ni yule anayezaliwa na uzito wa kilo 4 au zaidi ya hapo bila kujali umri wa mimba.Kwa kawaida watoto wa kiume huzaliwa na wastani wa uzito wa kilo 3.3, wakati wale wa kike huzaliwa na wastani wa kilo 3.2

Baadhi ya sababu zinazopelekea mama kujifungua mtoto mwenye uzito mkubwa ni pamoja na:
1. Mama kuwa na ugonjwa wa kisukari (wa kudumu)
2. Mama kuwa na kisukari kipindi cha ujauzito (Gestational diabetes)
3. Mama mwenye uzito mkubwa
4. Mama kuongezeka uzito kupitiliza kipindi cha ujauzito
5. Mimba iliyopitiliza umri wa kujifungua (overdue), zaidi ya wiki 40.
6. Mama kujifungua akiwa na umri zaidi ya miaka 35
7. Mimba za watoto wa kiume huwa na chance kubwa ya mtoto kuzaliwa na uzito mkubwa kuliko wa kike. Nk

Hatari gani zinaweza kutokea wakati wa kujifungua?
1. Kuongeza uwezekano wa mama kujifungua kwa upasuaji (C/S delivery)
2. Mama kuchanika wakati wa kujifungua na kupoteza damu nyingi
3. Mama kuongezewa njia (Episiotomy) ili kusaidia mtoto kutoka na mama kupoteza damu nyingi.
Tukumbuke kuwa upoteaji wa damu nyingi ndio kisababishi namba moja cha mama wanaojifungua.
4. Mfuko wa uzazi kushindwa kurudi kwenye size yake kwa wakati mara baada ya kujifungua (uterine atony) na kupelekea upotevu wa damu nyingi.5. Kama mama alishajifungua kwa operation hapo awali ni rahisi mfuko wa uzazi kuchanika kabla ya kufikia muda wa uchungu sababu ya mtoto mkubwa (uterine rupture) ambayo ni hali ya hatari sana kwa mama.

Mbali na hatari zilizoko kwa mama wakati wa kujifungua mtoto anayezaliwa na uzito mkubwa ni hatari kwake pia, kwa vipi?
1. Mtoto anaweza kupata ugumu wakati wa kutoka, kicha kimetoka lakini bega la mtoto linakwama kwenye nyonga za mama na hivyo kupelekea kuvunjika kwa mfupa wa bega (clavicle/ colar bone) na kusababisha kitu kinaitwa (Shoulder Dystocia). Hali hii ni hatari kwa mtoto na kwa mama.

2.Hii inapelekea wahitaji kulishwa kwa drip za sukari maana miili yao inahitaji energy nyingi sana lakini kiwango cha maziwa cha mama mara baada ya kujifungua hakitoshi kumlisha mtoto.

3. Ili kumlisha huyu mtoto lazima mishipa itafutwe ili awekewe drip, unene hukwamisha jambo hili.

Na hii inaweza kusababisha mtoto kupoteza uhai haraka sana

4. Mtoto mwenye uzito mkubwa ni rahisi sana kupata manjano (jaundice), hii inatokana na kuvunjwa kwa seli nyekundu za damu ambazo hazitolewi mwilini kwa kasi inayotakiwa kwani ini bado halijakomaa. Bilirubin ikizidi na Kwenda kwenye ubongo huathiri ukuaji wa akili ya mtoto.

5. Mtoto kuwa na uzito mkubwa hata hapo baadae anapokuwa mtu mzima. Hii inampelekea kuwa katika hatari ya kupata magonjwa kama kisukari, presha na moyo ukubwani (Metabolic syndrome).

6. Watoto wengi wanaozaliwa na uzito mkubwa wanapata alama ndogo kwenye dakika 1 na ya 5 baada ya kuzaliwa (Apgar score). Kadiri alama hizi zinavyokuwa ndogo ndivyo mtoto huyu anavyokuwa na ugumu wa kucopy na mazingira mapya ya nje na ukuaji wa akili yake kwa ujumla.

Hivyo ni muhimu sana mzazi kuhakikisha anachukua hatua zote stahiki za kupunguza uzito kupita kiasi kabla ya ujauzito, kuhakikisha uzito hauongezeki kupita kiasi kipindi cha ujauzito na kutumia dawa stahiki ikiwa ni mgonjwa wa kisukari au amepata kisukari cha ujauzito.

Lakini hata mara baada ya kujifungua ni vizuri mama kuepuka vyakula vitakavyomuongezea uzito sana yeye na mtoto aliyezaliwa na kuhakikisha mtoto huyu anapata muda wa kuushughulisha mwili sawasawa ili kutoishia kwenye matatizo zaidi hapo baadae.

crd:dkt mbaga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom