Akalee mtoto... Mtoto akikua naye atakua amekua.. Atachagua mfumo atao ona unafaa akajiendeleze. Ipo mingi...
Usijali,ukiishiwa hoja nenda tu kimya kimya hakuna haja ya samahani!Samahani, siwezi kujibiza na wewe.
😅😅😅,hoja zimekuwa za moto,kwendraaaaa!Mifano yako ya kuokoteza inadhihirisha wewe ni mtu wa aina gani.Tuishie hapo.
😅😅,leo weekend naenda kupata gongo safii kabisa!Huna hoja nenda kanywe komoni.
Wote wako sahihi kulingana na mtazamo na malengo ya mitazamo yao. Wapo wanaowafikiria wanyonge, wakipata mimba wataingiaje private schools? wataendeleaje Vyuo vya elimu ya juu. Wapo Wanafiki wasiojali wengine wanaishije, wanakula nini wajisifiao kutetea wanyonge. Hawa wanakariri maandiko 'kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe, kila mbuzi atakula kulingana na urefu wa kamba yake'. Tuombe mungu atupe busara yasitutokee yaliyowatokea wenzetu pale maskini walipozidi kuwa maskini na matajiri walipozidi kuwa matajiri halafu wakaanza kunyang'anyana.>vitaDr Abbas ambaye ni msemaji mkuu wa serikali anasema wanafunzi wanaopata mimba shuleni hawatarudi kuendelea na masomo katika mfumo rasmi bali wataruhusiwa kupitia mfumo usio rasmi yaani private candidates.
Abdul Nondo boss wa vijana pale ACT wazalendo anapinga vikali yeye anataka wanafunzi hawa baada ya kujifungua warudi katika mfumo rasmi wa masome ili wawe na sifa ya kukopesheka na Bodi ya mikopo watakapochaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu.
Mjadala ni mkali kweli kweli ndani ya kipindi cha Tuongee asubuhi. Star tv.
Nani yuko sahihi?
Maendeleo hayana vyama!
Ulichosema ni sahihi na ndio ulivyokuwa msimamp Wa serikali. Tatizo ni shinikizo la wafadhili. Nadhani umeshaona humu makubaliani ya kupatiwa mkopo Wa eliimu takriban trilioni moja. Moja ya masharti ni watoto Wa kike kuendelea na masomo kwrnye mfumo rasmi baada ya kujifungua. Naomba serikali itafasiri upya maana ya mfumo rssmi. Iwe kwamba kila anayefanya mtihani wa necta ahesabiwe kuwa katika mfumo rasmi. Hao wanafunzi wamama wafanyemtihani wa necta kama private candidate! Hapo hatutakuwa tumekiuka masharti ya mkopo wa wazungu.Kuna mambo ambayo lazima kama jamii yenye upekee wake tuyasimamie hata kwamba tunatofautiana kiitikadi.
Moja ya jambo hili ni mimba kwa wanafunzi. Siafiki mwanafunzi apate Ujauzito kurudi katika mfumo rasmi wa elimu kama wenzake ambao hawajapata.
Hapa tutahalalisha umama, baba na hata ushemeji katika shule/darasa na ile dhana ya uanafunzi kufa kifo cha kawaida.
Kila kitu kinautaratibu wake. Tutambue pia kuwa shule ni ni chombo ambacho jamii inawatengeneza wanajamii wa baadae katika kuiendeleza jamii husika kwa siku za usoni. Na kwamba, ni unapokuwa shuleni basi uzingatie ile miiko ambayo jamii imeona haipaswi kuvunja na watoto wake ndio maana wakapelekwa shule.
Sasa kama huyu aliyepelekwa shule ameona hawezi kufata misingi hiyo ya jamii ya nini kumuendeleza katika jambo ambalo hakulizingatia?
Shule zibaki kuwa shule na taratibu, sheria, utamaduni na majuzi zake zisimamiwe. Ikiwa ikatokea mwanafunzi akapata Ujauzito basi, apelekwe katika mfumo mbadala usio rasmi na ule aliokengeuka ili shule na malengo ya shule katika jamii yabaki kama ambavyo jamii inapenda iwe.
Sio kila atakalo mfadhili ni jambo jema ktk mfadhiliwa.
Mwenye kisu kikali ndiye anayekata nyama
Hana maana hiyo,akili zenu huwa zinakwama wapi?Anazungumzia kama mtoto kapewa mimba na mtoto mwenzake!Je,huyo mtoto wa kiume naye anafukuzwa aende mfumo usio rasmi?
WHERE COMMON SENSE STOPS TO BE COMMONDr Abbas ambaye ni msemaji mkuu wa serikali anasema wanafunzi wanaopata mimba shuleni hawatarudi kuendelea na masomo katika mfumo rasmi bali wataruhusiwa kupitia mfumo usio rasmi yaani private candidates.
Abdul Nondo boss wa vijana pale ACT wazalendo anapinga vikali yeye anataka wanafunzi hawa baada ya kujifungua warudi katika mfumo rasmi wa masome ili wawe na sifa ya kukopesheka na Bodi ya mikopo watakapochaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu.
Mjadala ni mkali kweli kweli ndani ya kipindi cha Tuongee asubuhi. Star tv.
Nani yuko sahihi?
Maendeleo hayana vyama!
Huyu dogo akili ndogo Sana, hajui kuzuia mimba za wanafunzi Ni moja ya population control measure.
By the way, hatuwezi kuwa na wanafunzi wanaozaa na kurudi shuleni watakavyo, utaratibu wa shule ufuatwe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Siasa weka pembeniNani anashida na Population contorol wakati Muheshimiwa Rais anataka tuzae
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu yangu hawatakuelewa hata kidogo. Wao na JPM wao! Wangekuwa wanaunga mkono maagizo ya Mungu hivyo hii nchi ingekuwa ya walokole! Tangu tupate uhuru hizo mimba zipo. Waathirika wapo wengine ni wakurugenzi katika mashirika ya umma na kampuni binafsi. Hilo hushughulikiwa kwa busara. Wote wanaopata ujauzito kwa sababu tofauti tofauti, mimba huwafukuza shule! Haiwekani kuhudhuria masomo na mimba. Hilo haliingii akilini. Wengi wao baada ya kujifungua hurudi shule. Hapa ndipo hutumika busara. Mhusika ataendelea na shule wapi na kivipi halikuwa tatizo.Mkuu anzisha mada hapa watu watoe ushuhuda walivyopatiwa mimba wakiwa shuleni na baadaye wakapambana na kupata fursa ya kurejea shuleni na leo ni watu wakubwa tu!Hilo la kulea ni jukumu lao na ndugu zao,watajua namna ya kufanya,cha msingi wapewe fursa ya kurudi shule katika mfumo rasmi!
Twendeni Kenya na Uganda tukapate uzoefu,wao wanawaruhusu watoto waliojifungua kurudi shule!Niliona siku moja kwenye Tv mtoto akihojiwa ambaye alikuwa amerejea shuleni huko Kenya!Nikasema kumbe inawezekana kabisa,tena wengi wao wanakuwa na juhudi na masomo maana wanakuwa wanajua makosa waliyoyafanya!
Nisema wazi tu,nje ya mfumo rasmi wengi wao huwa hawafanikiwi,yaani huko ni kama dumping area!
Timu ya utungaji sera ya CCM 2015 iliona umuhimu wa kuendelea kuwapa fursa watoto hawa kurudi shule na ikawekwa kwenye ilani,lakini ni maamuzi tu ya JPM binafsi kuwa yeye hawezi kusomesha watoto waliojifungua,anasema hayo utafikiri pesa ni yake na sio kodi za watanzania!
Kwani nani kakataa... Private mbona nyingi.ukiwemo mfumo huu rasmi wa elimu, kama binti amepata mimba akiwa kidato cha 5, akajifungue na arudi shule badae aendelee alipoishia
Sent using Jamii Forums mobile app
Nondo anafata bosi wake Zitto anachotaka waseme, na hii point wanakomaa nayo kwa sababu ndicho wazungu wanataka kusikia.
Otherwise, ukishapata mimba hutakiwi kurudi kwenye mfumo ule wa mwanzo.
Watoto wa kiume wanaowabebesha mimba, watakuwa wanahifadhiwa Korokoroni. Sema nn, na wasichana wapunguze ge.nye.Je watoto wakiume wanaowabebesha mimba wafanyweje?
Ndugu sidhani kama katika hili kuna U CCM na Upinzani, ni swala la Cultural and values za jamii yetu.1.Hili jambo kwanza hakuanza kutaka mfadhili,CCM think tank yao kwa maana ya watunga sera walilijumuisha kwenye ilani yao 2015!Mabadiliko yaliyotokea ni matakwa binafsi ya JPM na sio timu ya CCM na serikali kwa ujumla!
2.Tumepima madhara kama wakirejea?Au tunaendeshwa na hisia binafsi kutokana na kwamba JPM kasema?Kwanini hatujaenda kufanya utafiti Kenya na Uganda ambao wamewaruhusu watoto watakaojifungua kirudi shule?
3.Vipi kwa mtu aliyempa mimba?Je,kama ni mwanafunzi mwenzake,naye kwakuwa anakuwa baba basi naye kikombe kimuhusu na afukuzwe shule?Au mzigo huu tunambebesha mtoto wa kike?
4.Mfumo usio rasmi ni mfumo wa kupunguza ujinga tu,ni kama dumping area,asilimia kubwa huwa wanafeli na hawaendelei na elimu za juu!Nenda vyuoni ukafanye utafiti ni wangapi wametoka nje ya mfumo rasmi!
5.Je,ni kweli wasiokuwa ndani ya mfumo rasmi hata wakifanikiwa,vigezo na masharti ya mkopo chuo kikuu inawaengua kuwa wanufaika?
Ungejiuliza maswali yake na kupata majibu,pengine ungekuwa na mtizamo tofauti!
Nchi kwa sasa tunakosa mijadala kutokana na siasa zilizogubikwa na UCCM na Upinzani!Nyeusi watu wataita nyeupe kisa tu iko upande wao!