Dkt. Abbas na Abdul Nondo watofautiana namna watoto wa kike wanaopata mimba shuleni watakavyoendelea na masomo

Sasa ukiona mtu kama Sarungi na Fatuma Karume wanavyo jishaua na takataka zingine kule twitter huwq nashangaa sana!

Alafu mtu kama Zitto tulifikiri msomi atoe mawazo chanya kwa jamii lakini lenyewe lipo tu kutetea ujinga halina tofauti kabisa na ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
Think tank ya CCM ilikuwa inatetea ujinga kwa kuweka kipengele hicho kwenye ilani ya uchaguzi 2015?
 
Kuna dada alipata ujauzito nikiwa darsa la 4 yeye la 6 enzi za mkapa,nilishangaa kukutana naye chuo tukiwa kozi moja pale CoET!Nikamuuliza ilikuwaje maana baada ya kupata ujauzito sikumuona tena mpaka hapo tulipoonana!Alinieleza alilazimika kukatisha masomo na kwenda kujifungua,akakaa nyumbani na baadaye akajiunga na shule nyingine akamaliza la 7 na kufaulu,alichaguliwa kwenda kidato cha kwanza na akaendelea na masomo mpaka hapo tulipokutana!Leo hii ni Engineer na yuko huko serikalini na tunawasiliana mara moja moja!Nawaza tu asingepata fursa kwenye mfumo rasmi,angeweza kufika huko?Achilia mbali 100% mkopo aliopata chuo kipindi cha JK maana CoET wote tulipata 100%!
Nikiona mjadala huu huwa namkumbuka rafiki yangu huyo na nashindwa kuwa mnafiki bali kusimama kwenye ukweli!

Unaweza kujibu swali nililokuuliza?

Kwamba kabla ya tamko la Magufuli utaratibu ulikuwaje?
 
Sasa ukiona mtu kama Sarungi na Fatuma Karume wanavyo jishaua na takataka zingine kule twitter huwq nashangaa sana!

Alafu mtu kama Zitto tulifikiri msomi atoe mawazo chanya kwa jamii lakini lenyewe lipo tu kutetea ujinga halina tofauti kabisa na ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
Think tank ya CCM ilikuwa inatetea ujinga kwa kuweka kipengele hicho kwenye ilani ya uchaguzi 2015?Wengi mnaotetea hoja ya kuwaondoa kwenye mfumo rasmi ni kwasababu ya JPM kasema,hamuangalii uhalisia!Mngeenda Kenya na Uganda kujifunza,mbona wao wanafanya na je kuna madhara gani?
 
Hujui akibainika anakula miaka 30, na wa kike anabaki nyumbani? Au na wewe unajitoa ufahamu?
Hana maana hiyo,akili zenu huwa zinakwama wapi?Anazungumzia kama mtoto kapewa mimba na mtoto mwenzake!Je,huyo mtoto wa kiume naye anafukuzwa aende mfumo usio rasmi?
 
haiwezekani ukapata mimba ukarudi tena kwenye mfumo rasmi je? si itakuwa kuruhusu mapenzi shuleni kila msichana atajiachia na kuzaa akijua atarud tena kuendelea na shule

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo mnaongea kwa hisia tu na mambo mnayoaminishwa na JPM!Nenda Kenya na Uganda,wanawaruhusu kurudi shule lakini namba za watoto wanaopata ujauzito ni ndogo kuliko sisi ambao tunawazuia kurudi shule!
Tanzania wastani kila mwaka wanafunzi 5500 wanaacha masomi kutokana na ujauzito!
 
Kati ya taka taka huwa sipendi kujihisisha zano basi ni zile za aina ya Nondo.... huyo huwa ni mtafuta kiki kama Zitto! Kwanza ni dhambi kumuhusisha Dr Abbasi na taka taka kama Nondo


Sent from my iPhone using Tapatalk
Kama na dr. Abbas naye katolewa jalalani atakuwa takataka kumzidi Nondo! Dr. Abbas ni wa Saut? Nondo ni biwi bado jalalani linatengenezwa! Je, na Ruttashobolwa ni takataka la jalala lipi? Halikosi kuwa takataka licha ya kunyanyapaa takataka nyingine!
 
Watu tunaongea kana kwamba Watoto wa kike ni jamii kutoka sayari nyingine.

Hizo mimba wanapewa na kina nani?

Kwa nini mnataka wakishapata mimba waingizwe kwenye kundi tofauti kabisa na jamii? kana kwamba wameshatoka kwenye ubinaadamu wa kawaida na sasa wao hawafai tena?.

Ningetamani sana nao wabaki na heshima ile ile hata baada ya kupata mimba na kujifungua. Kama tuliwaheshimu awali sioni kwa nini tuwapotezee heshima hiyo baada ya kuzaa.

Kwa upande mmoja tutajifanya ni jamii yenye kumuheshimu Mwanamke na upande mwingine tunamnyanyapaa Mwanamke huyo huyo kwa kisingizio cha kuzaa mapema, ili hali aliyempa mimba ni huyo huyo Mwanaume.

Hizi vita na mabavu yetu dhidi ya Mabinti hawa Wadogo, ni bora tungeelekeza kwenye kuhakikisha Wanaume Mabazazi hawawapi Wanawake hizo mimba.

Tuheshimu Wanawake na tuheshimu karama yao ya uzazi...Mama ni Mama hata kama alikuzaa akiwa anasoma, tena wapo wanaoongea hovyo ili hali nao wamezaliwa na Mama aliyekuwa bado anasoma.
Mungu akuongezeee hekima na busara, wallah upo sahihi san mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu yetu inahujumiwaje?

Unaweza kusoma michango bora, kutoka kwa wanachama wengine, inayobainisha namna hoja za wapinzani, wanaharakati na asasi za kiraia zinavyoweza kufanya hivyo.

Hili si suala la kufanya mzaha, wala si muafaka kulitumia kwa maslahi finyu ya kisiasa na serikali imekataa kushiriki kufanya mizaha katika elimu.
 
Tofauti na wewe, kwangu mimi, mtumishi wa Umma anayehudumu kama Katibu Mkuu, kwa kutambua mamlaka na nguvu zinazotokana na wajibu na majukumu yake, siwezi kumwona kama mtu wa kawaida.
Obama akiwa Rais USA alishawahi kuacha kuhutubia na kuanza kujibishana kwa hoja na mtu aliyekuwa anapiga kelele akidai njia anayopitia Obama si sahihi!Obama akamtuliza akamsikiliza na yeye akatoa hoja zake,jamaa naye akajibu na Obama naye akaendelea kujibu ikawa kama dialogue flani hivi amazing!Mwisho wa siku ukumbi ukanyenyuka na kumshangilia Obama kwa uwezo wake wa kupambanua hoja na kuzitetea!
Angalia CNN au BBC,unakuta watu wazito serikalini wanaunganishwa kwenye mdahalo kwa video conferense na waalikwa wengine wanakuwa wachambuzi wa kawaida tu!
Sasa hapa unaniambia katibu mkuu ni mtu wa kuogopwa kiasi hicho?Mawazo yako yatakuwa mgando na huenda tatizo liko kwako maana yeye hajaona huo uspecial ndio maana akakubali kuwa sehemu ya mjadala!
 
Hoja yangu haikuwa hiyo uliyoileta wewe. Badala yake, mzizi wa hoja yangu ulikuwa katika itifaki. Huyo kiongozi wa ACT halingani kihadhi na Katibu Mkuu.

Hoja za kijana wa ACT zingeweza kujibiwa na kiongozi wa UVCCM anayeuelewa vizuri msimamo wa serikali au raia huru yeyote anayeweza kutoa hoja kinzani.

Kwa meneno mengine, pengine kwa uwazi zaidi, katika mjadala husika, wanaharakati, asasi za kiraia na wapinzani wana hoja dhaifu mno zisizohitaji kujibiwa na Katibu Mkuu.

Hata kama tungejitahidi kudunisha nafasi ya Katibu Mkuu, hatuwezi kuondoa ukweli kwamba hiyo ni nafasi nyeti na muhimu serikalini.
Inamaana katibu Mkuu Abbas hajitambui mpaka kakubali kualikwa?
 
Obama akiwa Rais USA alishawahi kuacha kuhutubia na kuanza kujibishana kwa hoja na mtu aliyekuwa anapiga kelele akidai njia anayopitia Obama si sahihi!Obama akamtuliza akamsikiliza na yeye akatoa hoja zake,jamaa naye akajibu na Obama naye akaendelea kujibu ikawa kama dialogue flani hivi amazing!Mwisho wa siku ukumbi ukanyenyuka na kumshangilia Obama kwa uwezo wake wa kupambanua hoja na kuzitetea!
Angalia CNN au BBC,unakuta watu wazito serikalini wanaunganishwa kwenye mdahalo kwa video conferense na waalikwa wengine wanakuwa wachambuzi wa kawaida tu!
Sasa hapa unaniambia katibu mkuu ni mtu wa kuogopwa kiasi hicho?Mawazo yako yatakuwa mgando na huenda tatizo liko kwako maana yeye hajaona huo uspecial ndio maana akakubali kuwa sehemu ya mjadala!
Mifano yako ya kuokoteza inadhihirisha wewe ni mtu wa aina gani.Tuishie hapo.
 
johnthebaptist, .

Kingine anaposema warudi shule baada ya kujifungua pia afikirie hao si watoto pekee ata hao waliozaliwa na hao wazaziwatoto ni watoto na wanahizaji matunzo nani atawajibika nao?
.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hivi watu wazima wakiwa makazini au wanasoma Masters tena full time huwa hawapaswi kuzaa sababu hawatokuwa na muda wakuwajibika na watoto??

Naomba unisaidie hapa kidogo
 
Back
Top Bottom