Dkt. Abbas na Abdul Nondo watofautiana namna watoto wa kike wanaopata mimba shuleni watakavyoendelea na masomo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,780
141,667
Dr Abbas ambaye ni msemaji mkuu wa serikali anasema wanafunzi wanaopata mimba shuleni hawatarudi kuendelea na masomo katika mfumo rasmi bali wataruhusiwa kupitia mfumo usio rasmi yaani private candidates.

Abdul Nondo boss wa vijana pale ACT wazalendo anapinga vikali yeye anataka wanafunzi hawa baada ya kujifungua warudi katika mfumo rasmi wa masome ili wawe na sifa ya kukopesheka na Bodi ya mikopo watakapochaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu.

Mjadala ni mkali kweli kweli ndani ya kipindi cha Tuongee asubuhi. Star tv.

Nani yuko sahihi?

Maendeleo hayana vyama!
 
Hao wabebaji mimba warudi kama watu wazima, hivyo watumie utaratibu wa QT yaani wakajisajili kwenye centres ambazo zitawapa mafunzo na kusajiliwa kufanya mtihani.
 
johnthebaptist, Huyu Nondo kwanza aliwahi kuona bodi ya mikopo inabagua kutoa mikopo kwa kigezo hicho, kimsingi bodi ya mikopo inakooesha Mtanzania yeyote vigezo vidogo ni kwa sababu ya kiwango kidogo cha pesa iliyopo.

Kingine anaposema warudi shule baada ya kujifungua pia afikirie hao si watoto pekee ata hao waliozaliwa na hao wazaziwatoto ni watoto na wanahizaji matunzo nani atawajibika nao?

Mimba nyingi za utotoni ni maisha duni na ukosefu wa elimu ya uzazi kwa watoto wetu, watoto wanaozaa mara nyingi huingia katika majukumu ya kuwalea watoto wao sasa hayo majukumu watayawezea wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dr Abbas ambaye ni msemaji mkuu wa serikali anasema wanafunzi wanaopata mimba shuleni hawatarudi kuendelea na masomo katika mfumo rasmi bali wataruhusiwa kupitia mfumo usio rasmi yaani private candidates.

Abdul Nondo boss wa vijana pale ACT wazalendo anapinga vikali yeye anataka wanafunzi hawa baada ya kujifungua warudi katika mfumo rasmi wa masome ili wawe na sifa ya kukopesheka na Bodi ya mikopo watakapochaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu.

Mjadala ni mkali kweli kweli ndani ya kipindi cha Tuongee asubuhi. Star tv.

Nani yuko sahihi?

Maendeleo hayana vyama!
Hapo ndio kumaanisha wametofautiana? Au msimamo wa serikali upo palepale? Maana Abdul Nondo anataka warudi shuleni baada ya kujifungua kama nani?
 
Kati ya mada huwa sipendi kujihusisha nazi basi ni zile za aina ya Nondo.... huyo huwa ni mtafuta kiki kama Zitto! Kwanza ni dhambi kumuhusisha Dr Abbasi na Nondo

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kuna mambo ambayo lazima kama jamii yenye upekee wake tuyasimamie hata kwamba tunatofautiana kiitikadi.

Moja ya jambo hili ni mimba kwa wanafunzi. Siafiki mwanafunzi apate Ujauzito kurudi katika mfumo rasmi wa elimu kama wenzake ambao hawajapata.

Hapa tutahalalisha umama, baba na hata ushemeji katika shule/darasa na ile dhana ya uanafunzi kufa kifo cha kawaida.

Kila kitu kinautaratibu wake. Tutambue pia kuwa shule ni ni chombo ambacho jamii inawatengeneza wanajamii wa baadae katika kuiendeleza jamii husika kwa siku za usoni. Na kwamba, ni unapokuwa shuleni basi uzingatie ile miiko ambayo jamii imeona haipaswi kuvunja na watoto wake ndio maana wakapelekwa shule.

Sasa kama huyu aliyepelekwa shule ameona hawezi kufata misingi hiyo ya jamii ya nini kumuendeleza katika jambo ambalo hakulizingatia?

Shule zibaki kuwa shule na taratibu, sheria, utamaduni na majuzi zake zisimamiwe. Ikiwa ikatokea mwanafunzi akapata Ujauzito basi, apelekwe katika mfumo mbadala usio rasmi na ule aliokengeuka ili shule na malengo ya shule katika jamii yabaki kama ambavyo jamii inapenda iwe.

Sio kila atakalo mfadhili ni jambo jema ktk mfadhiliwa.
 
Well said!
 
Mada imeisha mwenye sikio na asikie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom