Watanganyika hatuwezi kukubali Kamwe kukabidhi Nchi hii kwa Wazanzibar, Lile ni Koloni letu hata Jussa anajua
Hakuna kiongozi bora anayeweza kutoka CCM sasa. Aje Bilal, Halal na Hilal yote ni magamba. Heri tuwape wapinzani nao wajaribu vitu vyao. Otherwise we are doomed. Tuna kaugonjwa kaitwako Ammaglobulinemia kisiasa.
Inaonekana Jk anawakosesha usingizi kabisaa!! Mara eti anamuandaa migiro,mara membe,mara bilal.achen kuweweseka,jk anae mgombea wake na ndio ataeshinda,jk alimpeleka zenj karume akiwa hana mvuto kupitia mtandao wake akiwa waziri wa mambo ya nje,akampeleka shein akiwa hana mvuto,kawasaidia wabunge wengi wa ccm kuingia bungen na pia kawasaidia wapinzan wengi tu kuingia bungeni,mkitaka kujua nguvu zake muulizeni yule padri muasi asiewahi kuvaa pete ya ndoa!
Wanajamii;
Kwa wafuatiliaji wa habari bila ya shaka watakua wamegundua kuwa Makamu Wa Rais Mh. Dk Bilali kwa kipindi kirefu sasa amekuwa katika ziara za kikazi mikoani na wilayani na kupewa kipau mbele katika media za Tanzania. Ziara hizi kwa mtazamo wa haraka japokuwa ni za kikazi lakini zimekuwa ni nyingi sana zaidi ya kiongozi mwingine yoyote wa Kisiasa.
Ikumbukwe kuwa Dr. Bilali ni Makamu wa Rais na anafanya zile kazi ambazo Rais amemwagiza au yuko aware nazo.
Yawezekana kabisa kuwa Rais Kikwete ameamua kuchukua uamuzi huo wa kumuandaa na kumtangaza Bilali awe mgombea Urais wa CCM 2015 ili kukinusuru chama chake CCM kutokana na makundi ambayo itake isitake 2015 yatakimega CCM kabisa kwa asilia 100%. Huenda akawa na sababu nyingi lakini chache ni zifuatazo:
​
- Safari hii ni zamu ya Wazanzibar kutoa Rais. Kumbuka hii ni hoja rahisi kama walivyoamua kuwa safari hii Spika ni Mwanamke na hivyo kumweka Sita pembeni. K
​
- Dk. Bilali hana Makundi na amekuwepo katika siasa za Bara na Visiwani na anakubalika (Of course ziara za sasa zimam-promote)
​
- Dk. Bilali amekuwa Makamu wa Rais na anakubalika kama Presidential Material
​
- Ili kuzima chokochoko za Wazanzibari kuua Muungano dawa ni kumweka Mzanzibar. JK hawezi kuruhusu Zanzibar iwe Nchi au Dola (Historically na Kikatiba).
- JK hataki aonekane kaivuruga Nchi ndo maana kwa mambo yote makubwa nchi hii kaamua bora tu akae kimya kuliko kusema. La kuhusu katiba ameona bora atofautiane na Chama chake ili kuacha Lergacy na kuleta utengamao katika Nchi.
Ni nini maoni yako binafsi kuhusu Dk. Bilali na harakati zake za kuzunguka mikoani na wilayani in connection na mbio za Urais 2015? Je yawezekana akawa ni Chaguo la JK?
Nawasilisha.
Dr. Bilal umri nao unaelekea machweo, sidhani kama hata yeye mwenyewe ana wazo la kugombea. Kwa jinsi watu walivyoichoka ccm, bila kupatikana mgombea kijana basi tutegemee uchakachuaji wa kura kwa mara nyingine.
Ni maneno ya Ukweli Ndugu Yangu Superman.Nami nimesikia kutoka vyanzo vya Uhakika kuwa Dr Bilal anatayarishwa kuwa Mgombea wa Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.Dr.Bilal ni mzoefu wa siasa za Tanzania Bara kuliko Visiwani ukichukulia kuwa amewahi kufanya kazi kwa karibu na marais wote toka Mwalimu mpaka sasa Kikwete pia ana ushawishi wa kutosha Zanzibar,Wale wafuatiliaji wa siasa za huko kumbukeni kinyanga'nyiro cha Urais kati ya Rais mstaafu wa Zanzibar Mzee Aman karume na Dr Bilal mpaka kumuondoa Dr Bilal kugombea nafasi hiyo kwa kupitia vikao vya Chama,kumbukeni pia Uchaguzi wa Rais wa sasa wa Zanzibar,Dr Bilal alikuwa na ushawishi mkubwa,na pengine kapewa nafasi hii ya Umakamu wa Bara ili kutuliza lile vurugu lililokuwepo alipoenguliwa na kumpisha Dr Omar.
Dr Bilal ni msomi na mzoefu wa Utendaji kuliko siasa za Majukwaani,kinachoniogopesha Mimi ni Afya yake na umri ambao unaonekana hautoweza kuhimili mikikimikiki ya Kampeni na baadaye Uongozi katika Taifa hili ambalo linahitaji Kiongozi Makini na mwenye Afya isiyo na migogoro.CCM wanatumia nafasi hii kumtembeza Dr kila pande ya Nchi ili apate popularity,kwa lolote litakalokuwa kutakuwa na mgawanyiko mkubwa ndani ya Chama Tawala.Kwa sababu jinsi hali ilivyo sasa,kila mwanasiasa anajiona anaweza kuikwaa kazi hiyo......"Kama kaweza Kikwete,kwa hakika hakuna atakayeshindwa!".Katika list ndefu kuna akina Membe,Lowassa,Nchimbi,Magufuri na hata Mama Migiro.
Vyama vya Upinzani viangalie kwa makini nyendo za huyu Mzee,kwani siasa ya kweli inaanza katika ushindani wa kujadili Hoja za kumjenga Mtanzania.......Wapambane nae kihoja nao wapite mikoani na kila pande anayopita huyu Mzee kuzima Hoja zake na kuwapa wananchi nafasi ya kuona upande wa pili wa serikali hii dhalimu!
Mkuu, maoni yangu ni kwamba kweli Bilal analo jukwaa lakini hatimaye atashindwa kung'ara. Kwa nini nasema hivyo? Bilal hawezi kujiuza kwa Watanzania bila kufarakana na CCM. Idadi kubwa ya Watanzania hata vijijini hivi leo wanaelewa kuwa ufisadi ndilo tatizo kubwa lililotufikisha hapa tulipo. Bilal atawashawishije hawa Watanzania kama kweli atapambana na ufisadi? Kumbuka Mwalimu Nyerere alituasa kuwa kiongozi akisema anapinga ufisadi hata ukimwangalia usoni lazima ionekane kweli kwamba huyu anapinga ufisadi. Bilal ataanzia wapi? Hiyo ndiyo changamoto ya Bilal na yeyote yule atakayesimama ndani ya CCM kutaka ridhaa ya Watanzania kuwaongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano.Mkuu Logically, ukishakuwa VP unafanya kazi zote za Urais unazopewa. Rais asipokuwepo wewe unakaimu. So with time say 5 years kama kichwa chako kizuri, unakuwa na nafasi nzuri ya kurithi hicho kiti. Ni nini maoni yako?
Yawezekana kabisa kuwa Rais Kikwete ameamua kuchukua uamuzi huo wa kumuandaa na kumtangaza Bilali awe mgombea Urais wa CCM 2015 ili kukinusuru chama chake CCM kutokana na makundi ambayo itake isitake 2015 yatakimega CCM kabisa kwa asilia 100%. Huenda akawa na sababu nyingi lakini chache ni zifuatazo:
​
- Safari hii ni zamu ya Wazanzibar kutoa Rais. Kumbuka hii ni hoja rahisi kama walivyoamua kuwa safari hii Spika ni Mwanamke na hivyo kumweka Sita pembeni. K
​
- Dk. Bilali hana Makundi na amekuwepo katika siasa za Bara na Visiwani na anakubalika (Of course ziara za sasa zimam-promote)
​
- Dk. Bilali amekuwa Makamu wa Rais na anakubalika kama Presidential Material
​
- Ili kuzima chokochoko za Wazanzibari kuua Muungano dawa ni kumweka Mzanzibar. JK hawezi kuruhusu Zanzibar iwe Nchi au Dola (Historically na Kikatiba).
- JK hataki aonekane kaivuruga Nchi ndo maana kwa mambo yote makubwa nchi hii kaamua bora tu akae kimya kuliko kusema. La kuhusu katiba ameona bora atofautiane na Chama chake ili kuacha Lergacy na kuleta utengamao katika Nchi.
Inawezekana kuna connection,lakini binafsi sioni zaidi ya kuwa ni matokeo ya kukosa kazi kwani cheo cha makamu wa rais huko nyuma kilikuwa kinabebwa na uwaziri mkuu and/or urais wa zanzibar. Bilal ni makamo wa kwanza wa rais per se, ambae anatokana na tume ya Bomani kupendekeza Tanzania kuiga mfano wa Marekani wa running mate, ambae hata nchi marekani anaonekana anapwaya na kuna baadhi ya watu wanajenga hoja kwamba ni ubadhirifu tu wa kodi wa wananchi kuwa na nafasi kama hiyo.Ni nini maoni yako binafsi kuhusu Dk. Bilali na harakati zake za kuzunguka mikoani na wilayani in connection na mbio za Urais 2015? Je yawezekana akawa ni Chaguo la JK?
Unaweza kuwa sahihi kwa manufaa ya taifa na kwa fikra nje ya Boksi. Bilal si chaguo sahihi kwa CCMau Nchi
Lakini "Ki CCM"( Makundi) na kujaribu kuunga unga muungano amabao siku zinavyozid kwenda nyufa zinazidi Huyo mzee ndiyo anaweza kuwa best option ya CCM kutusogeza tu . Sio kwamba ni option ya kutatu matatizo ya UCHUMI UFISADI, Mungano etc
Hata fanya chochete kuhusu Muungano lakini uwepo wake ni sawa na Vidonge ARV kwa mgonjwa wa ukimwi. Kuchelewesha madhara ya tatizo....
Zaidi ya muungano Bilal inaweza kuwa option nzuri kwa ksingizo cha zamu "yao" lakini lengo kuu ni kumpiga chini EL ambaye wameshindwa na hawana nguvu za kumkatalia kavu kavu.
So mpaka hapo nadhani bilal ni chaguo bora kufunika/kufukia matatizo halisi na muda uende lakini sio chaguo bor kutatua na kushghulikia matatzio. iwe ni ya muungano au mengineyo.
Sana sana atachofanya kama akiwa rais atachemsha zaidi ya Kikwete. Hiyo itatufanyat umukbuke JK kwa sifa kama tulivyosahau mabaya ya Mkapa sababu ya underpefromnce ya ya JK..... ....
Huo ni mtazamo wangu.
Mkuu, maoni yangu ni kwamba kweli Bilal analo jukwaa lakini hatimaye atashindwa kung'ara. Kwa nini nasema hivyo? Bilal hawezi kujiuza kwa Watanzania bila kufarakana na CCM. Idadi kubwa ya Watanzania hata vijijini hivi leo wanaelewa kuwa ufisadi ndilo tatizo kubwa lililotufikisha hapa tulipo. Bilal atawashawishije hawa Watanzania kama kweli atapambana na ufisadi? Kumbuka Mwalimu Nyerere alituasa kuwa kiongozi akisema anapinga ufisadi hata ukimwangalia usoni lazima ionekane kweli kwamba huyu anapinga ufisadi. Bilal ataanzia wapi? Hiyo ndiyo changamoto ya Bilal na yeyote yule atakayesimama ndani ya CCM kutaka ridhaa ya Watanzania kuwaongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Ndo hapo tutajua EL ni noma na unstoppable. kama si hivyo may be Bilali anweza kudumu kipindi kimoja.
Na mimi nimeshaona hivyo na kwa kweli mada yako imesaidia kunifungua zaidi macho na akili. Nilikuwa najiuliza hizi safari za mara kwa mara za Bilal mikoani zina tija gani? Mara leo anakagua miradi, mara anapokea kadi ya mwana Chadema aliyeamua kurudi nyumbani CCM. Nina hakika ujumbe kwa upinzani umeshafika.Kiongizi Jasusi,
Kilichonifanya nilete hoja hii hapa ni kasi ya bilali huko vijijini, wilayani na mikoani ambapo feedback za media, picha nk zinaonyesha kuwa anagain umaarufu. Sasa akiendelea hivyo for next 3 years na hana record mbaya, basi bidhaa ya kichina si ajabu kuonekana ni bidhaa bora.