Tangia lini superman akapigwa mawe? Au ndio jina lako halisi.
Nimekusoma. Kimsingi hoja yako kuhusu Bilal ina mashiko, hasa iwapo suala la kuachia Urais baada ya muhula wake mmoja pia itazingatiwa, hivyo makamo wa Rais kuchukua nchi.
Suala la Anna Senkoro kidogo lina utofauti na Dr. Migiro, huyu anatokea CCM lakini kubwa zaidi ni kwamba profile yake ni kubwa sana kiasi cha kuweza kufunika kampeni za upinzani, kwani kasi ya kumrushia madongo mgombea mwanamke itaweza kuwa counter productive. Kwa kifupi, Migiro atawachanganya sana wapinzani hata kama eventually hatoshinda.
Kuhusu suala la muungano kwamba wabara do not care, ni kweli, lakini sidhani kama suala la serikali tatu linakwepeka, do you think so? Katika makosa ya Mwalimu kimantiki, lilikuwa suala hili la serikali mbili vis-a-vis tatu. Serikali tatu haikwepeki, na hii haita-ua muungano ila itaupunguzia nguvu yake kwa kiasi kikubwa sana, hivyo kutoa mwanya kwa foreign capital to exploit kule watakavyo. Na kama unavyojua, sikuhizi hakuna political diplomacy, hiyo ilikuwa enzi za Nyerere. Sikuhizi ni economic diplomacy, na hata mabalozi wetu huko nje hiyo ndio shughuli yao ya msingi.