DK. Bilali Chaguo la JK Kumrithi 2015?

Superman ngoma nzito hapo, hapatakiwi kamari, uzee na vurugu za vijana ni nyingi ukichanganya na upinzani kiti kitapotea, idadi ya bara si mchezo kwenye kura
 
Slaa alisema kwenye kampeni za 2010......... Kumchagua JK ni janga la kitaifa.................. Kama ni kweli basi naamini kumchagua Bilali utakuwa ni msiba wa kitaifa!!!
 
Zihara ndio neno gani? Yaani humu jf kuna watu kiswahili kinawashinda sana hata sijui wamesoma shule gani. Mtu anatumia h sehemu ambayo haitakiwi kabisa, na hili tatizo limekuwa sugu sana humu jf. Inakera kiasi kwamba hata kama mtu ameandika points za maana lakini ukishaona tu hivyo hata hamu ya kuendelea huna? Kuzuhia, kuhaga, zihara, fulaa.....
kama nimekosea si unanirekebisha tu.
 
Hii ni kuonyesha kuwa wagombea Urais CCM hawapo hivyo Wapinzani njia nyeupeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!
 
Tanzania itaweza kuwahudumia hao ma-first ladies wa Bilal? Kila mmoja atataka kuiba kupitia NGO zao. Tumeona Mama Mkapa alivyokwapua hela kupitia NGO yake, na sasa Mama Kikwete is doing the same thing. Si kwamba nawabagua hao akina mama BUT the Country cannot afford to allow the same S*H*I*T to happen.
 
Superman, kuna tatizo ambalo mimi ninaliona..
(1) Tanzania kwa sasa ni nchi volatile na potential kwa mega riots na bahati mbaya hakuna mtu anayejuwa namna ya kumanage political risk kama Mchonga
(2) Siasa za Tanzania sasa hivi siyo zile za zidumu fikra sahihi za m/k Mao, sasa hivi hata
  • ndani ya chama cha CCM hakuna umoja tena, na hata ule umoja wa kinafiki umetoweka haupo
  • siasa za makundi zilizoanza miaka ya 1995 ni vigumu kuziratibu kwa sababu ya uwepo wa vyama vya upinzani vyenge nguvu na kukubalika na wengi
  • Migawanyiko ndani ya chama sasa imevuka mipaka hadi kufika kwa wananchi na vyombo vya dola
(3) Hali ya umafia inayoendelea ni haileti tija kwa amani na umoja wa kitaifa
(4) Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umefikia climax au point of diminishing returns. Hata wa-Bara sasa hawautaki na kuweka mgombea kutoka Zanzibar ni kuharakisha matokeo ya symptoms ninazoeleza
(5) Hali ya mgawanyiko wa kidini ulioasisiwa na Kikwete is still existant and can now provide the minimum energy for majority of the voters to revolt ... hili mkuu litashangaza wengi kwa sababu lipo na halifutiki kirahisi. Isome vizuri mifano ya mifano ya huko Arusha, Mbeya na kwingine..
(6) Kiwango cha ufisadi kilichojidhihirisha mpaka sasa kinatisha, kukirihisha, na kutia hasira inayoamsha hamasa ya watu wengi kwa haraka kuichukia CCM. Watetezi wa CCM ni wanufaika wa mfumo CCM ambao nao si wengi.
(7) hauchi hauchi kunakucha ... tujiandae kwa matokeo tusiyuyapenda kutokea katika nchi yetu kuanzia sasa

My conclusion:
Wakichagua vibaya candidate wa kumrithi Kikwete utakuwa ndiyo mwisho wa CCM, mwisho wa Tanzania, mwisho wa Muungano, mwisho wa kisiwa cha amani.... I keep my fingers closed
 
Wakati mwingine lazima tukae chini tujiulize, tutafakari mambo yafuatayo:
Kwanza: Tunaambiwa Tanzania ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Pili: Tunaambiwa kuna nchi inaitwa Zanzibar
Tatu: Tunaambiwa kuna watu wanaitwa Wazanzibari. Kwa hiyo kimantiki tu ni kuwa kuna Watanzania ambao sio Wazanzibari. Hao ni wa Tanganyika
Nne: Zanzibar ina serikali yake, bendera yake
Tano: Haiwezekani kwa mtu asiye Mzanzibari kuwa Rais wa Zanzibar
Sita: Tunaambiwa Serikali ya Muungani wa Tanzania ndiyo inayosimamia masuala ya Tanganyika ndani ya Muungano
Kwa mantiki hiyo ni kuwa Rais wa Tanzania pia ndiye kiongozi wa Tanganyika.
Sita: SASA INAKUWAJE MZANZIBARI AWE RAIS WA TANGANYIKA?

Tukijuliza hayo, tutaona kwambani vigumu Mzanzibari kuwa Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania ambayo pia inasimamia Tanganyika.

Tusubiri katiba mpya tuone.

Ilulu.jpg
 
ama kweli kazi ipo. hapo ndio tutajua kama kweli mfuko wa cement unauzwa super market.
 
Hivi president anachuguliwa na CCM au wananchi? Mbona hatuzungumzi wananchi wana mtazamo gani?

Nimewahi kusema CDM wanafanya kusudi kabisa kuamsha "Tanganyika nationalism feelings", this is big trouble for CCM. Ukiachana na wale wazee wa G55, hakujawahi kutokea watu wa kuitetea Tanganyika kama ambavyo Znz imekuwa ikitetewa katika muungano.

Mainlanders are becoming more hostile to islanders + the change in the political landscape, I can assure you Dr Bilal haiwezi mikiki mikiki ya kina Lissu, Mnyika, Zitto et al. Mmeona alivyopata tabu huko Mbeya, people are tired with "soft spoken peace and tranquillity preaching politicians" people want someone who commands authority, kuanzia anavyoongea na kila kitu. Huyu jamaa awekwe jukwaa moja na mtu kama Liss kuomba kura Tarime!! I dont know if you get the picture.
 
Uchumi wa dunia unashikiliwa na vijana, nini kimetokea? Huyu anayelaumiwa ss kuangusha uchumi c alichaguliwa akiwa kijana? Sarkozy, obama, cameroon, angalia Lula da Silva, Mkapa, moi, Manmohan, kinachotakiwa mi naona ni intergrity na wala sio umri, ndoa zenyewe vijana cku izi daily divorce. Slaa ana forty ngapi vile?, Lipumba je? Nani tn mgombea uRais Tz? Ana umri gani? Tafakari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom