DK. Bilali Chaguo la JK Kumrithi 2015? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DK. Bilali Chaguo la JK Kumrithi 2015?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Superman, Feb 21, 2012.

 1. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Wanajamii;

  Kwa wafuatiliaji wa habari bila ya shaka watakua wamegundua kuwa Makamu Wa Rais Mh. Dk Bilali kwa kipindi kirefu sasa amekuwa katika ziara za kikazi mikoani na wilayani na kupewa kipau mbele katika media za Tanzania. Ziara hizi kwa mtazamo wa haraka japokuwa ni za kikazi lakini zimekuwa ni nyingi sana zaidi ya kiongozi mwingine yoyote wa Kisiasa.

  Ikumbukwe kuwa Dr. Bilali ni Makamu wa Rais na anafanya zile kazi ambazo Rais amemwagiza au yuko aware nazo.

  Yawezekana kabisa kuwa Rais Kikwete ameamua kuchukua uamuzi huo wa kumuandaa na kumtangaza Bilali awe mgombea Urais wa CCM 2015 ili kukinusuru chama chake CCM kutokana na makundi ambayo itake isitake 2015 yatakimega CCM kabisa kwa asilia 100%. Huenda akawa na sababu nyingi lakini chache ni zifuatazo:


  • Safari hii ni zamu ya Wazanzibar kutoa Rais. Kumbuka hii ni hoja rahisi kama walivyoamua kuwa safari hii Spika ni Mwanamke na hivyo kumweka Sita pembeni. K
  ​
  • Dk. Bilali hana Makundi na amekuwepo katika siasa za Bara na Visiwani na anakubalika (Of course ziara za sasa zimam-promote)
  ​
  • Dk. Bilali amekuwa Makamu wa Rais na anakubalika kama Presidential Material
  ​

  • Ili kuzima chokochoko za Wazanzibari kuua Muungano dawa ni kumweka Mzanzibar. JK hawezi kuruhusu Zanzibar iwe Nchi au Dola (Historically na Kikatiba).
  ​

  • JK hataki aonekane kaivuruga Nchi ndo maana kwa mambo yote makubwa nchi hii kaamua bora tu akae kimya kuliko kusema. La kuhusu katiba ameona bora atofautiane na Chama chake ili kuacha Lergacy na kuleta utengamao katika Nchi.

  Ni nini maoni yako binafsi kuhusu Dk. Bilali na harakati zake za kuzunguka mikoani na wilayani in connection na mbio za Urais 2015? Je yawezekana akawa ni Chaguo la JK?

  Nawasilisha.

   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,621
  Trophy Points: 280
  kwa ccm hili linawezekana kabisa why not? na ameshawambia wazanzibar kuwa wautunze muungano.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hiyo point ya tatu: kwamba anakubalika kama presidential material ni very questionable. Anakubalika kwa nani? Nani kafanya utafiti na kuthibitisha kuwa hata kule Ng'wanakitolyo Bilal anakubalika?
   
 4. chubulunge

  chubulunge Senior Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wampitishe tu 2015,slaa atachukua kirahisi
   
 5. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Ukiangalia sasa hivi makundi yanatisha:

  EL kakomaa na ziara za makanisani na misikitini na hafla mbalimbali za kuchangisha na bila ya shaka ndo njia ya kujipromote. Wote tumeona alivyomkomalia JK juu ya sakata la Richmond kuwa anahusika na JK kaufyata. Hatakubali kuukosa Urais na hakuna mwenye ubavu wa kumzuia. Imedhihirika.

  SS aka 6 na kundi lake wana kete ya Mwakyembe na wameshaanza kupaka. It is a matter of time kabla hawajaamua kuwataja wahusika. Wanaendelea pia na kampeni zao za chni kwa chini. Hawa ikishindikana kama liwalo na liwe watakitosa chama. Remember CCJ.

  Akina Sumaye Wanapima Upepo kwa Sasa.

  Mwandosya wameshammaliza.

  Salim Ahmed Salimu - Siasa za maji taka haziwezi.

  Nini nkimebaki tena kwa CCM? only Bilali? Au Shein?
   
 6. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mkuu Logically, ukishakuwa VP unafanya kazi zote za Urais unazopewa. Rais asipokuwepo wewe unakaimu. So with time say 5 years kama kichwa chako kizuri, unakuwa na nafasi nzuri ya kurithi hicho kiti. Ni nini maoni yako?
   
 7. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Anything is possible. Wapinzani waanze kujipanga mapema.

  nashauri waache ubinafsi na waform Alliance ya kuweka mgombea Uraisi na wabunge wanaokubalika ambao hawatagawa kura.
   
 8. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Kamanda tumia lugha ya kistaarabu na andika hoja. Si kuwa hatuwezi matusi. Tukiyafungulia utatafuta pa kujificha.

  Ulikuwepo wakati Anna makinda anachaguliwa Uspika? Was she a better candidate? kama siyo ni nini kilitokea?

  Unaweza kuweka arguments zako zikaeleweka. No need ya matusi unless kama unataka kupata BAN.
   
 9. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Dr. Bilal umri nao unaelekea machweo, sidhani kama hata yeye mwenyewe ana wazo la kugombea. Kwa jinsi watu walivyoichoka ccm, bila kupatikana mgombea kijana basi tutegemee uchakachuaji wa kura kwa mara nyingine.
   
 10. The Mockingjay

  The Mockingjay JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dr. GB anayo makundi!
  Asingekuwa na makundi angekuwa rais wa Zanzibar badala ya Shein.
  Labda atajaribu tena Zanzibar 2015. Anawafuasi wengi wazuri tu.
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,621
  Trophy Points: 280
  wakimuweka Shein nitawaona wana akili sana kuliko kumuweka huyu Bilal...Bilal wamrushie huko Zanzibar
   
 12. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145

  Mkuu JK na Bilali wamepishana miaka 5. Jk alizaliwa 1950 na Bilali 1945. By 2015 Bilali atakuwa 70. Ni kweli umri wake umeenda Kilometres nyingi. Lakini kwa CCM chochote kinawezekana. wakongwe wangapi wa CCM bado wako kwenye siasa mbali na Kingunge?

  Kama CCM watakuja na mgombea makini nayekubalika na watanzania, bado wanaweza kuwa na nafasi, shida iliyopo ni nani?
   
 13. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Tuseme ukweli bilal hana mvuto kwa siasa za bara labda zenji
   
 14. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145

  Mkuu utafute ule uzi hapa JF aliouleta Hutaki Unaacha.

  Inasemekana Bilali yuko Kundi la EL, Shein pia aliwekwa na kundi hili na Karume pia analikubali.

  If that being the case, is it Plan B ya EL kuwa Bilali achukue Nchi na EL awe Makamu wa Rais? Then baada ya Muda Bilali ajiuzulu kwa sababu yoyote ikiwemo Uzee ila EL achukue Nchi?

  Watch out kipengele hicho kitakuwaje katika katiba mpya.
   
 15. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #15
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Scenario zote zinawezekana, ili mradi Mzanzibar ashike Nchi. Both Shein & Bilali are possible Senior Candidate kuliko yeyote Mwingine. karume hawezi kwani hawajawahi kuja katika sisa za bara kwa cheo cha juu.

  In either case akishinda Shein au Bilali na wote ni watu wa EL na wakaja kujiuzulu kumpisha EL bado imekula kwetu.

  JK anaweza akawa anajua zaidi kwa nini kwa sasa anamprote sana Bilali.
   
 16. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #16
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145

  Mkuu wapi Mzee Ruksa au Mzee wa Uwazi na Ukweli walikuwa na Mvuto wakati wanapitishwa?

  Wapi Bi Kiroboto alikuwa na mvuto wa Kuwa Kiongozi wa Bunge?

  Tafakari.
   
 17. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  kile kizee/kibabu yaani nikikaona tu najikia kichefuchefu mbaya...nina alergy sana kile kibabu..dah nisamehewe tu!!
   
 18. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Mkuu hao walipata mvuto enzi hizo ccm haijamshika mkono kipofu mpiga kura ambaye leo anafakari ukali wa maisha anashindwa kunywa biya wala chai wala komoni hata gongo nayo bei imepanda watu wamechoka mkuu tunao ishi uswazi ndo tunajua hali halisi bilal hana mvuto kwa wadanganyika hajafanya lolote la maana kuwafrahisha wananchi kwenye ziara zake zaidi ya kutembea na mkasi mfukoni
   
 19. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #19
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Itabidi turudi idara ya fizikia ya chuo kikuu Dar, kuangalia tabia yake.

  Mbaya sana niliwahi kusikia kwamba jamaa huyu ni mwanchama wa sera za David Cameron! Hili lazima alisemee mwenyewe bila kuwatega sumu wanaolifahamu vizuri kabisa!!!!!
   
 20. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
   
Loading...