NakuliliaTanzania
JF-Expert Member
- Sep 24, 2007
- 555
- 7
Naona kumekucha wandugu!
Dk Bilal: Waliotuhumiwa kwa ufisadi wajiuzulu
*Asema hakuna sababu ya wao kubakia madarakani
*Ashauri viongozi kuacha ubinafsi kwenye mikataba
*Atahadharisha hali hii ikiendelea vurugu zitatokea
*Asema CCM upande wa Zanzibar imedorora
Na Salma Said, Zanzibar
WAZIRI Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Mohammed Gharib Bilal, amesema kiongozi anayetuhumiwa kwa ufisadi anapaswa kuchukua uamuzi wa kujiuzulu ili kutoa nafasi ya uchunguzi kufanyika juu tuhuma zinazomkabili.
Alisema uamuazi wa kujiuzulu ni muhimu hasa kama tuhuma hizo zinahatarisha amani katika nchi.
Dk Bilal alisema hivi karibuni wakati wa mahojiano maaluum na Mwananchi nyumbani kwake Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema iwapo tuhuma zinazoelekezwa ni kubwa ambazo zinaweza kuhatarisha usalama na amani ya nchi basi hakuna sababu ya kiongozi kubakia katika madaraka.
�Kwenye tuhuma kubwa ambazo zinahatarisha hata amani ya nchi, ni bora kiongozi akachukua uamuzi wa kisiasa wa kujiuzulu ili atoe nafasi ya kuchunguzwa tuhuma hizo,� alisema Bilal.
Alisema endapo kiongozi amepatikana na hatia katika suala la rushwa basi sheria ifuate mkondo wake na sio kuwekewa kinga kwa sababu aliyepatikana na tuhuma hizo ni mtu mkubwa.
�Kiongozi achunguzwe na akibainika kama amefanya vitendo vya kupokea au kutoa rushwa, nadhani sheria ndio iachiwe ichukue mkondo wake na isiingiliwe,� alishauri.
Alisema iwapo sheria zitafuatwa bila ya upendeleo zitawasafisha wanaotuhumiwa na kurejesha imani ya wananchi kwa viongozi hao.
Hivi karibuni, Mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa alitaja majina 11 ya viongozi wa serikali ambayo alidai kuwa wanatuhumiwa kwa ufisadi.
Dk Bilal aliwatahadharisha viogozi wa serikali kuwa makini na mikataba wanayosiani kwani inaweza kusababisha mifarakano katika nchi kama inavyojitokea hivi sasa, ambapo baadhi ya mikataba inadaiwa kuwa na matatizo.
Alisema lazima tahadhari ichukuliwe kuweza kuepukana na matatizo kama hayo yanayojitokeza na kudai kuwepo kwa udhaifu katika baadhi ya mikataba.
�Inaonekana udhaifu upo, hata kushutumiwa kwa baadhi ya viongozi wa CCM kuwa wametoa rushwa wakati wa uchaguzi huko ni kukiri kuwa kuna tatizo maana lisemwalo lipo na kama halipo laja, basi lishughulikiwe�,� alisema huku akitumia methali za kiswahili.
Waziri Kiongozi huyo Mstaafu alishauri kurekebishwa kwa mfumo utaoaji maamuzi ili kuongeza idadi ya watu wanaotoa maamuzi ili kupanua demokrasia ya kweli badala ya kuachiwa wachache kuwaamulia walio wengi.
Alisema hali hiyo inaweza kusaidia kuondoa malalamiko kwa wananchi kutokana na maamuzi yanayoamuliwa na watu wengi tofauti ya maamuzi yanayotolewa na wachache ambayo mara nyingi husababisha migogoro na kutoelewana.
Dk Bilal alisema Tanzania ina wataalamu wengi wa fani mbalimbali tangu zamani, lakini jambo la kusikitisha ni kuwa wataalamu hao hawatumiki ipasavyo.
Kuhusu nguvu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bilal alisema bado kina nguvu kutokana na kufanya vizuri katika chaguzi zote zinazofanyika nchini na kudai kuwa CCM Zanzibar imedorora.
Alisema kwamba tatizo kubwa linaloikabili Zanzibar ni tofauti ya uongozi na kwamba hivi sasa Zanzibar hakuna mwamko katika chama na kusababisha kidorore.
�CCM Zanzibar imedorora na inatokana na kuuliwa kwa maskani, hivi sasa hakuna maskani kama zilivyokuwapo. CCM kilikuwa kinapata msukumo kutoka uongozi wa juu, lakini sasa aina ya uongozi imechangia kwa kiasi kikubwa kudorora kwa chama,� alisisitiza Dk Bilal.
Dk Bilal alisema ingawa baadhi ya wana CCM Zanzibar hawapendi kuisikia kauli hiyo, alisisitiza kuwa huo ndiyo ukweli. "Hakuna mwamko wowote wa kuhamasisha vijana katika chama...," alisisitiza.
Aliahidi baada ya kumalizika Uchaguzi wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) wataanza kuhamasisha wanachama.
�Ukija uchaguzi kunakuwa na mwamko kidogo, lakini kukiwa hakuna chaguzi, chama kinalala watu wanasahau kama chama kipo, tukimaliza chaguzi tutaanza kuhamasisha wanachama,� alisema.
Dk Bilal aliwahi kutoa kauli kama hiyo ya kudorora kwa CCM Zanzibar wakati alipokuwa akijaza fomu ya kuwania nafasi ya Rais wa Zanzibar na kwamba kauli hiyo ilizusha gumzo kubwa visiwani hapa na kusababisha makundi mawili ndani ya chama hicho, moja likiwa nyuma yake na lingine kwa Amani Abeid Karume ambaye kwa sasa ni Rais wa Zanzibar.
Kuhusu maoni yake juu ya uongozi wa Dk Salmin Amour, alisema mara zote alikuwa tayari kukubali kushauriwa licha ya kuwa maamuzi ya mwisho kuwa yake mwenyewe.
Akizungumzia hali ya maisha, alisema sasa yamekuwa magumu zaidi na kumekuwapo na kasoro nyingi katika serikali ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi licha ya kuwepo mafanikio kadhaa.
�Hapo nje kuna mfereji (bomba la maji) mwaka wa nne huu hautoi maji, hata hivyo maji hapa kwetu tunapata kwa njia nyingi. Mafanikio yapo katika baadhi ya mambo, lakini matatizo yapo mengi na yanahitaji kurekebishwa. Kwa mfano huduma za afya bado ni mbaya ...,� alisisitiza Dk Bilal.
http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=2460