Ukaaji mbaya kama Chura au Kobe kwa muda mrefu husababisha Maumivu ya Mgongo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
DAKTARI Bingwa wa Mifupa wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Tanga (Bombo), Dk. Said Nondo, amesema chanzo cha matatizo ya watu kuugua mgongo ni ukaaji mbaya kama chura na kobe kwa muda mrefu.

Dk. Nondo aliyasema hayo wakati akitoa elimu kuhusu maumivu ya mgongo yanayotokana na ukaaji mbaya kwa muda mrefu.

Alisema matatizo hayo huwakumba watu mbalimbali wakiwamo watoto wa shule, wafanyakazi ofisini na viwandani. Alisema kama wanafanyakazi kwa saa tano au sita wakiwa wamekaa, wanapaswa kusimamama kila baada ya saa tatu ili kunyoosha misuli.

“Unapokaa muda mrefu bila kuinuka unasababisha misuli kuanza kubana taratibu. Ukaaji uliosalama na uliobora ni ambao unaliwezesha umbo la ute wa mgongo kuendelea kuwa kwenye hali yake ya uhalisia ya wima bila kupinda mgongo kuelekea mbele,” alisema Dk. Nondo na kuongeza kuwa:

“Unapokaa wima unaupa urahisi ute wa mgongo kuendelea kubaki kwenye hali yake ya uhalisia na kwa watu wa ofisini kuna viti maalumu ambavyo mbele yake kumetengenezwa umbo maalumu ambalo linasaidia kukaa katika hali iliyosalama zaidi.”

Aliendelea kusema kuwa kukaa kwa kutoa mgongo kama chura au kobe kunasababisha misuli ya mgongo kutoka kwenye kisogo mpaka kwenye kiuno kukaza taratibu kisha kuleta maumivu makali.

Dk. Nondo, alisema endapo maumivu machache ya mara kwa mara yataendelea kwa muda mrefu, yatasababisha umbile la mgongo kubadilika kutoka kwenye la asili la C na kunyooka na kuwa kama rula, kuminya pingili laini, kutanuka, kuminya misuli ya fahamu inayopasuka kwenye miguu.

Alisema misuli hiyo inatoka kwenye matundu madogo kati ya pingili moja na nyingine ikipitia kwenye makalio, nyuma ya paja na kushuka kwenye miguu.

Alisema hali hiyo inaweza kusababisha maumivu kushuka kutoka kwenye kiuno, makalio, miguu na inapozidi kwa muda mrefu inaambatana na ganzi, miguu kuwaka moto, kukosa nguvu au kukaza hasa usiku.

“Ni sababu moja inayoongoza kuleta maumivu ya mgongo kwenye rika zote kawaida ni umbile la mgongo halikuumbwa lenye kunyooka bali limeumbwa likiwa na mipindo mitatu, mifupa ya mgongo ambayo unaweza kugawa maeneo matatu la kwanza ni shingo, kifuani kuna upinde unaangalia mbele na chini kuna S inaangalia chini sasa katika ukaaji watu wengi wanakaa kwa kuinua mgongo lakini kifua chake kinakuwa kimekwenda mbele,” alisema.

Dk. Nondo alitoa ushauri ili kuzuia matatizo ya mgongo, maumivu ambayo yanatokana na ukaaji mbaya ni watu kuzingatia ukaaji salama ambao haupindishi mgongo ili kuweka ute wa mgongo kwenye umbo lake asili.
 
Dr Nondo
20240114_155653.jpg
 
Desa langu linaniambia unatakiwa kusimama na kutembea tembea walau kila baada ya 20 minutes.
 
DAKTARI Bingwa wa Mifupa wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Tanga (Bombo), Dk. Said Nondo, amesema chanzo cha matatizo ya watu kuugua mgongo ni ukaaji mbaya kama chura na kobe kwa muda mrefu...
Tuone hizo style Sasa za ukaaji kama chura au Kobe, Ili tusikae..au ni Makasiriko..🤔🤔
 
Back
Top Bottom