NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
Kwa kipindi kirefu nimekuwa nasita kuoa, kwa umri wangu wa miaka 28 nimeona ni wakati sasa niwe na ndoa official, Si mara ya kwanza kufikiria hili jambo, ni tangu nipo 25 nafikiria ila sheria za ndoa za kikristo zilikuwa zikinipa hofu kubwa mno hasa kwa tunayojionea kwa wahanga, Ni lazima tukubali wanawake wa sasa sio kama mama zetu wa enzi zile ambao tayari walikuwa wamefundwa kuishi maisha ya ndoa na mwanaume na ndio maana hakukuwa na vimbwanga vingi kama sasa. Ndoa za kikristo kwa sasa zimekuwa mtihani jamani.
Ndoa za kikristo ni ngumu kusuluhisha matatizo
Kwa mama zetu miaka hiyo ahsafundwa majukumu ya ndoa, kuishi na mwanaume, n.k. lakini siku hizi hali ni tofauti yani ukiongezea mambo ya usawa, wanawake walioelimika, ushauri wa mashosti watukutu, n.k. ndoa zimeingia kwenye matatizo mengi sana, Huko kanisani usuluhishi unaotumika ni ule wa kina mama zetu ambao angalau walikuwa waelewa ila kwa hawa wanawake wa sasa ni kama kumpigia mbuzi gitaa, na hapo ndipo watu wanakimbilia mahakamani wanaona kanisani ni kupoteza muda tu, kwa hili tu unaona ni wazi kabisa usuluhishi wa kikristo umefeli, Kwanini wakimbilie mahakamani na sio kwa wachungaji ?
Kuoa upya ni ngumu kwenye ukristo
Ndoa ya kikristo imejaa bureacracies nyingi sana, mnaweza kauchana hata miaka miwili hurusiwi kuoa upya mpaka kanisa litoe kibali chao, ukilazimisha kuoa upya shoka la sheria linakukata, what is ithis ?
Ndooa ya kikristo inampa mwanamke kiburi cha usawa
Mwanamke anajua ukishamvisha pete ashakubana hapo kuchomoka ngumu, Anajua fika kabisa hata afurukute mtaenda kanisani kwa wachungaji wataokuwa wanawabembeleza kila siku mkayamalize, anajua huna uhuru wa kuoa upya kirahisi, anajaua mkiachana ana mali zako pasu kwa pasu, n.k.
Ndoa za kikristo zinaleta tamaa ya mali
Pia katika suala la wale majambazi wanaoingia kwa nia ya kula timing muachane ili wapate mgao wa mali katika ndoa za kikristo ni rahisi sana, katika uislamu mwanaume hana wajibu huo, hapa pia adabu inaongezeka kwa mwanamke, hata mwanamke akikaza waweza kumpiga biti utaongeza wenzake watatu asiingilie mgao wao
.........................................................................
Binafsi nimekata shauri kwamba tamaduni za ndoa za kiisalamu ndio zitanipa ahueni zaidi ya kuishi maisha ya ndoa, mwanzoni nilikuwa nikisita kwa kuunganisha imani na dini kuwa kitu kimoja lakini kwa sasa nimeweza kukubali imani na dini ni vitu viwili tofauti nimeona ni sawa tu kuoa kwa misingi ya dini ya kiislamu, lakini kwa imani bado mimi ni mfuasi ya Yesu / Mkristo,