DID GIANTS EXIST? Historia ya Majitu ya Kale

DID GIANTS EXIST? Historia ya Majitu ya Kale

Ndo maana nilisema ya kuwa stor ya mtu huyu ni pana sana tena lakini kuna watu wanajua ila waliamua kuipotosha ili Afrika tusiwe na cha kuzungumza kuhusu Biblia na Quran

Utaona hata wao walivyomweleza ni kama hawamfahamu Uj ila wameeleza matukio ya Uj
Bado kuna jambo halipo sawa pahali ila kifupi ndo hivyo ulivyoona Chief na mwingin ajuae basi atusaidie tunaeza pata kitu
kwahiyo mtazamo wako ni upi dhidi ya hivyo vitabu...huoni kama viliweza kupotosha kuhusu historia na inayomuhusu UJ..itkuwa walipotosha mengi tu zaidi ya hilo
alibakari
 
Mkuu umeshawahi ona mtu akiwa na mapepo?? Je yanaingiaje ndani ya mtu anyhow??

Ndio hivyo hivyo kabla mwili hujaweza kutembea duniani ni lazima uwe na roho na roho haiwezi kuishi duniani bila ya kuwa na mwili

Hivyo watoto wadogo wanawekewa roho ndio wanaweza kuzaliwa duniani hivyo hivyo Yesu naye ili aishi duniani ilibidi mwili wa kale kachanga tumboni mwa bikira maria kapewe ROHO ndio kaishi duniani.... Tofauti ni kwamba ROHO aliyopewa kale kachanga ni ya MUNGU-MWANA ambapo kwa duniani alifahamika kma Yesu sijui umepata mwanga

Kwa hao malaika kma walitaka kuzaa na wanadamu ni simple wanaweza kuvaa mwili wa mwanadamu flani au hata wenyewe wanaweza kujubadilisha umbo na kuwa wanadamu au mnyama mfano waliomtembelea Abraham... Wale malaika walikuwa wanaonekana wanadamu kabisa kwa muonekano kumbe ni malaika ndio maana hata walipoenda kwa Ruthu wenyeji waliwatamani sababu ya mauonekano wa kibinadamu!!!

Hivyo kwa ufupi malaika akitaka kutembea duniani either ajibadilishe awe katika mfumo wa mwili au aingie ndani ya mnyama au binadam ili awe kufunction humu duniani otherwise watu watamkimbia wakimuona!!
Kwahyo unataka useme watu wanaoingiliwaga na mapepo wakifanya mapenzi wanazaa wanadamu wa ajabu au mapepo!

Maana kusema roho imemuingilia mtu aliyepo katika mwili inabidi uelezee hiyo roho inabadilishaje vitu kama mbegu za mwanaume hadi kuwa mbegu za hao mapepo(sijui umenipata)..

Maana kusema tuu pepo limemuingilia mtu afanye mapenzi na mwanadamu ndio kiumbe cha ajabu kikazaliwa bado hakijibu swali la msingi kuwa mbegu zilizotoka ni za mwanadamu au za huyo pepo sijui malaika
 
Historia ya UJ ni pana sana tena sana na katika historia hiyo huwezi amini imeanzia Tanzania na ndipo ilipoanza kuonekana lakini kwa sababu tusizozijua historia hii imefichwa na hivyo wengi kuona Uj hakuna anaejua alikotokea.

Uj inaaminika kwamba fuvu lake lipo mexico kwa sababu ni fuvu la mtu mweusi na lilionekana sio la mtu wa kawaida (Giant)

Kwa kuwa ni historia pana juu ya mtu huyu basi kifupi naomba upitie hapa chini nawe waeza kuja nisaidia pale nilipokwama kuhusu mtu huyo ila ukweli ndio huu kwamba historia yake imeanzia hapa Tanzania

Unju bin Unuq (pia: Unju bin Unuku, Unzi Bin Ununuk) ni jina la jitu katika masimulizi ya wakazi wa pwani ya Tanzania. Hadithi zake zasimuliwa kuanzia Bagamoyo hadi Kilwa.

Historia yake inapatikana katika makumbusho ya Kaole huko Bagamoyo.

Moja ya mambo ya ajabu ya mtu huyu ni urefu wake yaani kimo, inasadikiwa alikuwa na urefu mkubwa ulioweza kumfanya atembee baharini na miguu yake kugusa chini.

Pia alikuwa akitembea kutoka nchi hadi nchi kutokana na urefu wake. Inasimuliwa kuwa moja kati ya nyayo zake inapatikana kwenye jiwe alilokanyaga huko Tabora, Tanzania, wayo wa mguu wa kushoto wakati wayo wa mguu wa kulia ulionekana kwenye jiwe alilokanyaga huko Kongo.

Inasimuliwa pia akitaka kula alikuwa akichukua samaki baharini kwa mkono na kuchoma katika jua kisha anakula.

Kuhusu maisha yake inasimuliwa kuwa Unju bin Unuk hakuoa wala kuolewa kutokana na umbo lake.

Sehemu nyingine ya hadithi yake ni alipokufa Unju bin Unuq, aligawanyika vipandevipande kutokana na urefu wake na inasemekana kidole chake chenye urefu wa kilometa moja kasoro ndicho kilichopatikana na kuzikwa pale Bagamoyo, lakini hakuna simulizi mwili wake uliobaki uliangukia wapi.

Unju bin Unuq alikuwa na ndugu yake aliyejulikana kama Geofrey bin Unuk, huyu alipatikana maeneo ya Dodoma. Au kwamba Unuq baada ya kupotea kwa muda wa miaka mingi ndugu zake wa mbali sana wameonekana katika mkoa wa Dodoma.

Asili ya jina la Unju bin Unuq katika Uarabuni na BibliaEdit

Jina lake linatokana na Kiarabu cUdj bin Unuq / ‘Anaq عوج بن عنق anayejulikana katika visa vya nchi nyingi za Uislamu kama jitu kubwa sana. Waislamu walipokea hadithi kutoka kwa Wayahudi anakojulikana kwa jina la Og עוֹג‬.

Asili kabisa ni taarifa za Biblia kuhusu mapigano kati ya Wanaisraeli waliotoka Misri na Ogu mfalme wa Bashani (Hesabu 21,33)[1]; Wanaisraeli walimshinda wakiongozwa na Musa.

Ogu alisemekana kuwa mtu mrefu; Kumbukumbu la Torati 3,11 kinamtaja hivi: "aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho je! Hakiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni mikono kenda, na upana wake mikono minne, kwa mfano wa mkono wa mtu".

Katika masimulizi ya Wayahudi tabia hii iliendelea kuongezeka; katika Kitabu cha Amosi 2,9 anatajwa (bila kusema jina) kama "Mwamori" "nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni".

Wataalamu Wayahudi wa baadaye waliona ya kwamba vipimo vya Kumb. 3 kuhusu kitanda chake chenye urefu wa mikono yaani dhiraa 10, sawa na mita 4-5, vilihusu mkono wa hilo jitu lenyewe, hivyo walimwona mkubwa zaidi tena.

Kwenye kitabu Berakhot cha Talmudi Ogu anasimuliwa ya kwamba aliweza kuinua mlima aliotaka kurusha dhidi ya Wanaisraeli, lakini Mungu alimzuia[2]. Katika kitabu cha Nidah katika Talmudi Ogu anasemekana ni mtu aliyeishi kabla ya gharika ya Nuhu akiwa ni mmoja wa hao ambao walitunzwa.[3]

Katika UislamuEdit

Masimulizi ya Kiyahudi yalipokewa na Waislamu na kupanuliwa tena. Ushahidi uko kwa Al Tabari aliyeandika ya kwamba maiti ya cUdj ilikuwa kama daraja juu ya mto Naili.

Al-Thaclabi aliandika ya kwamba cUdj alikuwa na urefu wa dhiraa 23,333 akiweza kunywa kwenye mawingu, kushika ngumi baharini na kuichoma kwenye Jua. Alitembea mbele ya Nuhu wakati wa gharika kuu lakini maji yalifikia magoti yake tu. Aliishi miaka 36,000. Alipoona kambi la Wanaisraeli na Musa alivunja mlima akashika kipande cha kuangamiza kambi lote kwa pigo moja, lakini Mungu alituma ndege waliokula shimo katikati ya mlima uliomuangukia na kumfunga katikati. Hivi Musa aliweza kumshinda kirahisi

Hii ni picha iliopigwa huko Mexico miongo kadhaa nyuma

Asalaam kudo
nikipitaga dodoma kuelekea Singida hapa katikati najiulizaga..hivi haya mawe sio kuna watu walikua wanayachezea wakayapanga kwa namna hii...
 
Ndo maana nilisema ya kuwa stor ya mtu huyu ni pana sana tena lakini kuna watu wanajua ila waliamua kuipotosha ili Afrika tusiwe na cha kuzungumza kuhusu Biblia na Quran

Utaona hata wao walivyomweleza ni kama hawamfahamu Uj ila wameeleza matukio ya Uj
Bado kuna jambo halipo sawa pahali ila kifupi ndo hivyo ulivyoona Chief na mwingin ajuae basi atusaidie tunaeza pata kitu
wakanda life
 
Ndo maana tukawepo
Tafuta jibu kwanza sio unaquote, roh zinapuliziwa kwenye mwili, kinachozaliwa ni mwili na ndio maana mwili hufa ila roho baada ya mwili kufa hurudi kwa muumba.
Jiulize vizuri usije ukaniuliza nini kufa
 
Biblia inasema yesu alizaliwa japo kwa miujiza, hamna sehemu roho ya yesu iliingilia mtu, bali alizaliwa na mama yake alipata mimba..

Nataka nijue process ya kuupata mwili kwa hao malaika, roho ziliingiaje kwenyr miili na kufanya watakayo??
Majini huwa yanafanyaje kuwa na mwili wa mwanadamu
 
kwahiyo mtazamo wako ni upi dhidi ya hivyo vitabu...huoni kama viliweza kupotosha kuhusu historia na inayomuhusu UJ..itkuwa walipotosha mengi tu zaidi ya hilo
Historia ya Uj ni pana kuliko unavyodhania ila hapa nimejaribu tu kuweka sawa kuhusu huyo huyo Uj kwenye vitabu vya dini na wanavyomzungumzia humo ili nisitoke nje ya msatari wa mtoa Mada

Lakini kuhusu baadhi ya sehemu kufichwa inaeza kuwa ni sehemu ndogo sana ilifichwa lakini imetupotezea uhalali wa stori nzima kumhusu huyu jamaa yani ni kama vile ile fomula ya maji kisayansi ukitoa kale ka mbili ikabaki HO utakuwa umepteza maana kabisa.

So huyu jamaa yaezekana haijwahi kuwapo mtu kama huyo tena na yaezekana bila yeye ile safina isingekuwa na ubora ule hivyo ukianzia hapo tu utaona huyu mtu mweusi kuna haja ya kuficha historia yake kwa maslahi fulani

Au walishindwa kuitambua maana hawakufahamu alikotokea na kifo chake kilikuwa vipi
So yote yawezekana lakini ukiichambua zaidi historia hiyo unaeza leta mkanganyiko wa mambo flani kuhusu dini na baadhi ya maandiko yake kuhusu huyo mtu

So inatosha kwa hapo palipoelezwa Chief mengine tafuta na wew utapaata jambo
 
Kwahyo unataka useme watu wanaoingiliwaga na mapepo wakifanya mapenzi wanazaa wanadamu wa ajabu au mapepo!

Maana kusema roho imemuingilia mtu aliyepo katika mwili inabidi uelezee hiyo roho inabadilishaje vitu kama mbegu za mwanaume hadi kuwa mbegu za hao mapepo(sijui umenipata)..

Maana kusema tuu pepo limemuingilia mtu afanye mapenzi na mwanadamu ndio kiumbe cha ajabu kikazaliwa bado hakijibu swali la msingi kuwa mbegu zilizotoka ni za mwanadamu au za huyo pepo sijui malaika
Ooh sasa nimeelewa swali lako ngoja ntakurudia mkuu
 
Majini huwa yanafanyaje kuwa na mwili wa mwanadamu
ukitaka kujua mapepo/majini wanafanyeje kuwa no mwili wakibinadamu
Hiyo ni elimu nyingine mkuu.

Tunacho kijua ni kwamba wanadamu siyo kale tu, bali hata leo wapo wengi tu wanao dhini na majini/mapepo kwa kujua au kuto kujua.

Amini tu kwamba 20% ya watu unaopishana nao na mda mwingine hata kuongea, kusalimiana nao, na kufanya nao shughuli mbali mbali za kawaida ni majini.

NB: wanaowa na kuolewa.
 
N
nikipitaga dodoma kuelekea Singida hapa katikati najiulizaga..hivi haya mawe sio kuna watu walikua wanayachezea wakayapanga kwa namna hii...
sio huko tu maeneo mengi sana yapo hivyo
Na kwa hapo katikati ya singida na Dom hasa maeneo ya kutoka Bahi kuelekea manyoni kuna pahali juu ya jiwe kuna unyayo mkubwa sana na mawe kupangwa vizuri hako kaeneo Kana stor flan hivi dah basi tu ngoja niishie hapa
 
Mkuu inaonekana unajua mengi sana na una ufaham mkubwa sana kuhusu masuala haya embu funguka mkuu maana ndio mahala pake hapa ili tuongeze maujuzi

Kingine sielewi kwanni watu weusi hatupendi kuandika historia yetu tumejikuta inaelezewa na wazungu!! Kwa mfano hii story ya UJ Tanzania sijaikuta ikiandikwa kabisa mwisho wa siku wazungu na waarabu ndio wanaielezea so sad !!tuna mambo makubwa sana tumefanya waafrika ila kwa kutokuandika tumejikuta historia yetu imepotoshwa kabisa
 
nilichukua mpaka video hilo eneo ,yani nmekaa kwenye gari najiuliza mbona kama haya mawe watu walikua wanayachezea au wanayapasuaga... nikasema ngoja nichukue video
 
ukitaka kujua mapepo/majini wanafanyeje kuwa no mwili wakibinadamu
Hiyo ni elimu nyingine mkuu.

Tunacho kijua ni kwamba wanadamu siyo kale tu, bali hata leo wapo wengi tu wanao dhini na majini/mapepo kwa kujua au kuto kujua.

Amini tu kwamba 20% ya watu unaopishana nao na mda mwingine hata kuongea, kusalimiana nao, na kufanya nao shughuli mbali mbali za kawaida ni majini.

NB: wanaowa na kuolewa.
Mmhhhh umenitisha mkuu hapo kwenye 20% ya binadamu tunaokutana nao...
Sasa tunaweza kuwatambuaje watu wa namna hiyo??
 
N
sio huko tu maeneo mengi sana yapo hivyo
Na kwa hapo katikati ya singida na Dom hasa maeneo ya kutoka Bahi kuelekea manyoni kuna pahali juu ya jiwe kuna unyayo mkubwa sana na mawe kupangwa vizuri hako kaeneo Kana stor flan hivi dah basi tu ngoja niishie hapa
Duh.. Huo unyayo upo juu ya jiwe au?
Yaani ukitaka kuuona ni mpaka upande juu ya jiwe?
 
nilichukua mpaka video hilo eneo ,yani nmekaa kwenye gari najiuliza mbona kama haya mawe watu walikua wanayachezea au wanayapasuaga... nikasema ngoja nichukue video
Mnanitamanisha niende nikajionee huko dohh..
 
Mkuu inaonekana unajua mengi sana na una ufaham mkubwa sana kuhusu masuala haya embu funguka mkuu maana ndio mahala pake hapa ili tuongeze maujuzi

Kingine sielewi kwanni watu weusi hatupendi kuandika historia yetu tumejikuta inaelezewa na wazungu!! Kwa mfano hii story ya UJ Tanzania sijaikuta ikiandikwa kabisa mwisho wa siku wazungu na waarabu ndio wanaielezea so sad !!tuna mambo makubwa sana tumefanya waafrika ila kwa kutokuandika tumejikuta historia yetu imepotoshwa kabisa
Kweli kabisa mkuu hii ni Shida sana kwetu waafrika, ukiacha kuandika tu pia hata kusoma walio tuandikia hao wazungu na waarabu bado nayo ni shida.
 
Back
Top Bottom