Diamond Ushakosa Tuzo, Jua Nafasi yako. Achana na Washamba

Atasema ni haters uone ulimbukeni ulivyo mbaya
Diamond angekua na ustaarabu angetakiwa amuombe Roma na familia yake msamaha kwa kitendo Cha msanii mwenzake kuwa kwenye mateso huku mke wake akienda hadi mortuary alafu akaamua kutoka nyimbo kwa msisitizo kwamba anakaa kimya kilikuwa sio kitendo Cha ubinadamu

Ila kwa sababu sio mstarabu hataomba msamaaa
 
Nyie watu mnamuandama sana huyu kijana, aandamane na fikra zenu. Kwani hajaingia kwenye siasa, si kaingia na kachagua upande anaotaka.

Hata marekani kipindi cha vuguvugu la uchaguzi wasanii wengi walichagua pande zao, weusi wengi walimpinga trump lakini wapo baadhi yao waliomuunga mkono pia, haijarishi ni upande mbaya kwako ama ni mzuri kwa maono yake kaona hivyo.

Jamii imegawanyika mkuu, tukio moja linaweza kuonekana tofauti kwenye macho ya kila mtu eidha kutokana na uelewa au matakwa ya mtu binafsi. Kwahiyo huwezi kuiridhisha jamii yote. Nikupe mfano Ney wa mitego nae anaimbaga sana nyimbo uzipendazo(za kiharakati) angalia mapokeo ya nyimbo izo kwenye jamii, sia ajabu hata wewe huzifatilii na ile ni biashara so inabidi nae amix kidogo apate chochote.
 
Diamond angekua na ustaarabu angetakiwa amuombe Roma na familia yake msamaha kwa kitendo Cha msanii mwenzake kuwa kwenye mateso huku mke wake akienda hadi mortuary alafu akaamua kutoka nyimbo kwa msisitizo kwamba anakaa kimya kilikuwa sio kitendo Cha ubinadamu

Diamond ni kiwakilishi cha waliowengi ndani ya jamii.
Simshangai sana
 
Nyie watu mnamuandama sana huyu kijana, aandamane na fikra zenu. Kwani hajaingia kwenye siasa, si kaingia na kachagua upande anaotaka.

Hata marekani kipindi cha vuguvugu la uchaguzi wasanii wengi walichagua pande zao, weusi wengi walimpinga trump lakini wapo baadhi yao waliomuunga mkono pia, haijarishi ni upande mbaya kwako ama ni mzuri kwa maono yake kaona hivyo.

Jamii imegawanyika mkuu, tukio moja linaweza kuonekana tofauti kwenye macho ya kila mtu eidha kutokana na uelewa au matakwa ya mtu binafsi. Kwahiyo huwezi kuiridhisha jamii yote. Nikupe mfano Ney wa mitego nae anaimbaga sana nyimbo uzipendazo(za kiharakati) angalia mapokeo ya nyimbo izo kwenye jamii, sia ajabu hata wewe huzifatilii na ile ni biashara so inabidi nae amix kidogo apate chochote.

Ukiambiwa ueleze ujumbe wa huu Uzi utaeleza??
 
Eti "ili diamond awe msanii mkubwa Africa inabidi aache ulimbukeni"..unafiki wa Hali ya juu.Awe msanii mkubwa Africa mara ngapi?

Km kofia hata harmonize na alikiba walivalishwa,mbn nao waliimba majukwaa yote ya CCM? Hapo uwanja wa uhuru bongo muvi na bongo flavour karibia wote walikuwepo

Hivi ktk hili mnalomshututumu diamond,ukitoa Ney wa mitego na Roma mkatoliki kuna msanii mwingine yeyote anaweza kutoka hadharani akasema 'mimi nilikuwa mbele kupinga madhalimu ya utawala wa magufuli'

Mpoto aliwahi Kusema 'kama mnataka kuwafukuza wafukuzeni wote kisha majengo tufugie kuku'
Nami nakuambia ndugu mwaandishi Kama unakemea kemea wote ili km tunaanza upya tuanze upya pamoja_lkn km unamsema diamond peke yake na wengine unawaacha basi kauli yako ya kumsema diamond ni limbukeni na msanii mdogo na kuzidi kumpa ushauri wa sijui afanyaje ili awe msanii mkubwa,kauli hiyo ni upuuzi' na ya kinafiki

Mnasahau mapema sn; enzi ya magufuli kila aliyethubutu kukosoa hadharani chamoto alikiona,chadema wenyewe kibao walipambana mwwnzoni,baadae wakasanda wakaunga juhudi kinafiki,mnasahau?
 
Mleta mada unaonekana wewe ni mjuaji wa kila kitu,haya tuambie wewe umelifanyia nini taifa au jamii iliyokuzunguka,au wewe ni mtaalamu wa maandishi tuu?

Naona unawakejeli watu kua kununua sijui simu wanaona wao ni kutusua maisha,mara kununua tv sio kutusua! nini maana ya kutusua kwa tafsiri yako? kama mtu alijiwekea malengo ya kununua kitu fulani na akafanikiwa kukinunua kwanini asione hayo ni mafanikio kwake? mafanikio ni safari isiyo na mwisho,

Uandishi wako umejaa chuki za kijinga dhidi ya jamii iliyokuzunguka,unayo nafasi ya kurekebisha uandishi wako,unamshauri Diamond huku nawe upo kwenye giza totoro!
 
Back
Top Bottom