Diamond Ushakosa Tuzo, Jua Nafasi yako. Achana na Washamba

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,050
50,989
DIAMOND ACHANA NA WASHAMBA/MALIMBUKENI. TAMBUA NAFASI YAKO.

Na, Robert Heriel

Kitu ambacho kinakwamisha Watanzania tuliowengi ni USHAMBA/ULIMBUKENI.

Ulimbukeni ni like kitendo cha mtu kupata kitu Kwa kizuri au cha thamani Kwa mara ya kwanza, kitu kile kikamfanya atende kinyume na desturi na maadili yanayomzunguka mtu huyo.

Kwa Kiswahili cha kisasa neno Limbukeni ni USHAMBA.

Watanzania wengi ni MALIMBUKENI.
Wengi hatuna Exposure ya mambo yalivyo.

Tuna ulimbukeni karibu kwenye kila Nyanja za maisha.

Yapo malimbukeni ya Madaraka, unakuta jitu likipata uongozi tuu linafanya mambo ya hovyo kabisa. Tumeshayaona hayo malimbukeni, Washamba wa Madaraka.

Wapo Malimbukeni wa Michezo Kama mpira, hayo tumeyaona hata kwenye mashindano ya Club bingwa.
Maneno mengi uwezo mdogo, sifa moja wapo ya Limbukeni au mshamba utaiona kwenye maneno.
Limbukeni hujiinua zaidi kwenye mdomo kuliko vitendo.

Yapo malimbukeni wa Muziki na Umaarufu, haya mengi tunayaona kwa hawa Wasanii WA muziki na maigizo.
Kwa vile mtu hajawahi kuwa Maarufu haya alipokuwa shuleni basi akiwa mkubwa akiwa Maarufu sio ajabu akafanya mambo ya ajabu.

Sio ajabu jitu kuonyesha uchi wake mitandaoni, huo ndio ushamba WA umaarufu, sio ajabu mtu kuvujisha video za uchi au akinyonya denda akiwa anajirekodi. Huo ni Ulimbukeni.

Yapo Malimbukeni ya Fasheni, hawa wengi wao ni Wale waliotoka kijijini kwenda mjini, au waliotoka Tanzania wakaenda ng'ambo huko Ughaibuni.
Hawa wanajikuta wakitoboa masikio na pua ilhali wao ni wanaume.
Wengine wakitoa Marinda Kama Fasheni.

Diamond ni Msanii wa kawaida Kwa wanaoijua Dunia. Ila hapa Nchini ni Msanii Mkubwa.
Diamond ili awe Msanii Mkubwa Duniani lazima aache Ulimbukeni na ushamba.

Asifuate maneno ya Malimbukeni na Washamba ambao Kwa hapa TANZANIA ni zaidi ya 80% ambao ni Washamba.

Ogopa kushabikiwa au kufuata maneno ya watu ambao wanaona kuwa na simu Janja kamaiPhone ndio ujanja.

Ogopa kuwasikiliza watu wanaoona kuwa na Ghetto lenye Flat screen ya inchi 32 ndio kutusua maisha.

Ogopa kushabikiwa na kusikiliza maneno ya washabiki ambao kuwa na Gari ndio kutusua maisha.

Ogopa kushabikiwa na Mashabiki ambao hawataki kununua kazi zako Kwa njia Halali isipokuwa wanaenda Kuburn CD au kurushiwa kwenye muziki library ambazo hazijasajiliwa.

Ukitaka ujue Watanzania wengi ni Limbukeni ni siku uonekane kwenye TV utashangaa ndugu zako na marafiki watakavyokupigia simu na kukusifu.

Ulimbukeni unaitesa nchi hii karibu kwenye kila Nyanja za maisha.
Kiongozi akijenga Ka-Flyover utaona atakavyopiga kelele. Ulimbukeni mtupu!

Limbukeni hatajuagi nafasi zao ndani ya jamii.

DIamond huenda alikuwa hana interest za kutetea Haki za watu ndani ya jamii lakini Nafasi aliyonayo kimuziki ndani ya nchi unanilazimisha kutetea Haki za jamii Apende asipende.

Sasa unakuta jitu Limbukeni linakuambia sio lazima Diamond ajiingize kwenye mambo ya Siasa na uanaharakati hapo ndio unajua mtu huyo Hana Uelewa wowote wa jinsi Dunia inavyoenda.

Mtu unaweza usiwe na interest ya mambo ya Siasa lakini Nafasi yako ndani ya jamii ikakulazimisha kuingia huko.

DIamond wewe ni Msanii Mkubwa hapa Afrika Mashariki, bado unatakiwa ujitahidi uwe Msanii Mkubwa Afrika, ndipo uende Duniani.

Diamond ulichofanikiwa ni katika Propaganda Kwa Limbukeni wa TANZANIA kuwaaminisha kuwa wewe ni Msanii Mkubwa Duniani nao wanaamini hivyo.

Lakini unaowaaminisha ni watu ambao hata hawajui Duniani ni wapi licha ya kuwa wanaishi sehemu ya Dunia.

Hata hivyo sitaacha kukupongeza Kwa hatua uliyoipiga kimuziki kwani sio haba. Ila zingatia kuwa bado unasafari ndefu kuwa Msanii Mkubwa wa Afrika na hatimaye Msanii wa Dunia.

Ulimbukeni ndio kikwazo kikubwa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Mvomero, Morogoro
 
Kote sawa, ila hapa sijakuelewa,
Msanii ana nafasi katika siasa au katika matokeo ya siasa bila kujali chama?
 
Nafasi ya Msanii Mkubwa kwenye Siasa haiepukiki kutokana na nafasi yake ndani ya jamii.

Panapotokea uonevu Msanii Kwa nafasi ya Diamond Kama anajielewa lazima asimame na jamii kupinga uonevu.

Hivyo ndivyo Wasanii wakubwa wafanyavyo.

Nafikiri bado hajafikia level ya ukubwa Kama anavyojitangaza
 
DIAMOND ACHANA NA WASHAMBA/MALIMBUKENI. TAMBUA NAFASI YAKO.

Na, Robert Heriel

Kitu ambacho kinakwamisha Watanzania tuliowengi ni USHAMBA/ULIMBUKENI.

Ulimbukeni ni like kitendo cha mtu kupata kitu Kwa kizuri au cha thamani Kwa mara ya kwanza, kitu kile kikamfanya atende kinyume na desturi na maadili yanayomzunguka mtu huyo.

Kwa Kiswahili cha kisasa neno Limbukeni ni USHAMBA.

Watanzania wengi ni MALIMBUKENI.
Wengi hatuna Exposure ya mambo yalivyo.

Tuna ulimbukeni karibu kwenye kila Nyanja za maisha.

Yapo malimbukeni ya Madaraka, unakuta jitu likipata uongozi tuu linafanya mambo ya hovyo kabisa. Tumeshayaona hayo malimbukeni, Washamba wa Madaraka.

Wapo Malimbukeni wa Michezo Kama mpira, hayo tumeyaona hata kwenye mashindano ya Club bingwa.
Maneno mengi uwezo mdogo, sifa moja wapo ya Limbukeni au mshamba utaiona kwenye maneno.
Limbukeni hujiinua zaidi kwenye mdomo kuliko vitendo.

Yapo malimbukeni wa Muziki na Umaarufu, haya mengi tunayaona kwa hawa Wasanii WA muziki na maigizo.
Kwa vile mtu hajawahi kuwa Maarufu haya alipokuwa shuleni basi akiwa mkubwa akiwa Maarufu sio ajabu akafanya mambo ya ajabu.

Sio ajabu jitu kuonyesha uchi wake mitandaoni, huo ndio ushamba WA umaarufu, sio ajabu mtu kuvujisha video za uchi au akinyonya denda akiwa anajirekodi. Huo ni Ulimbukeni.

Yapo Malimbukeni ya Fasheni, hawa wengi wao ni Wale waliotoka kijijini kwenda mjini, au waliotoka Tanzania wakaenda ng'ambo huko Ughaibuni.
Hawa wanajikuta wakitoboa masikio na pua ilhali wao ni wanaume.
Wengine wakitoa Marinda Kama Fasheni.

Diamond ni Msanii wa kawaida Kwa wanaoijua Dunia. Ila hapa Nchini ni Msanii Mkubwa.
Diamond ili awe Msanii Mkubwa Duniani lazima aache Ulimbukeni na ushamba.

Asifuate maneno ya Malimbukeni na Washamba ambao Kwa hapa TANZANIA ni zaidi ya 80% ambao ni Washamba.

Ogopa kushabikiwa au kufuata maneno ya watu ambao wanaona kuwa na simu Janja kamaiPhone ndio ujanja.

Ogopa kuwasikiliza watu wanaoona kuwa na Ghetto lenye Flat screen ya inchi 32 ndio kutusua maisha.

Ogopa kushabikiwa na kusikiliza maneno ya washabiki ambao kuwa na Gari ndio kutusua maisha.

Ogopa kushabikiwa na Mashabiki ambao hawataki kununua kazi zako Kwa njia Halali isipokuwa wanaenda Kuburn CD au kurushiwa kwenye muziki library ambazo hazijasajiliwa.

Ukitaka ujue Watanzania wengi ni Limbukeni ni siku uonekane kwenye TV utashangaa ndugu zako na marafiki watakavyokupigia simu na kukusifu.

Ulimbukeni unaitesa nchi hii karibu kwenye kila Nyanja za maisha.
Kiongozi akijenga Ka-Flyover utaona atakavyopiga kelele. Ulimbukeni mtupu!

Limbukeni hatajuagi nafasi zao ndani ya jamii.

DIamond huenda alikuwa hana interest za kutetea Haki za watu ndani ya jamii lakini Nafasi aliyonayo kimuziki ndani ya nchi unanilazimisha kutetea Haki za jamii Apende asipende.

Sasa unakuta jitu Limbukeni linakuambia sio lazima Diamond ajiingize kwenye mambo ya Siasa na uanaharakati hapo ndio unajua mtu huyo Hana Uelewa wowote wa jinsi Dunia inavyoenda.

Mtu unaweza usiwe na interest ya mambo ya Siasa lakini Nafasi yako ndani ya jamii ikakulazimisha kuingia huko.

DIamond wewe ni Msanii Mkubwa hapa Afrika Mashariki, bado unatakiwa ujitahidi uwe Msanii Mkubwa Afrika, ndipo uende Duniani.

Diamond ulichofanikiwa ni katika Propaganda Kwa Limbukeni wa TANZANIA kuwaaminisha kuwa wewe ni Msanii Mkubwa Duniani nao wanaamini hivyo.

Lakini unaowaaminisha ni watu ambao hata hawajui Duniani ni wapi licha ya kuwa wanaishi sehemu ya Dunia.

Hata hivyo sitaacha kukupongeza Kwa hatua uliyoipiga kimuziki kwani sio haba. Ila zingatia kuwa bado unasafari ndefu kuwa Msanii Mkubwa wa Afrika na hatimaye Msanii wa Dunia.

Ulimbukeni ndio kikwazo kikubwa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Mvomero, Morogoro
Msanii wa kimataifa mameneja na washairi babu tale, mama dangote na unle shamte😀😀😀😀
 
Mshamba ni yeye anayeng'ang ania kuimba matusi tu!

😃😃😃😃

Wasanii wengi ni Washamba na Limbukeni sio hapa Nchini hata Duniani.

Ndio maana kazi ya muziki bado ipo kwenye kundi la kazi zisizoheshimika na utaendelea hivyo hivyo Kwa kipindi kirefu
 
Similar Discussions

17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom