Diamond Platnumz: Mdee ni Mzigo Jimbo la Kawe

Diamond Platnumz: Mdee ni Mzigo Jimbo la Kawe

Msishangae october ikawa Zari(CCM) vs. Halima Mdee (CHADEMA)...................Brother kaanza kampeni mapeeeeema
 
Kwani Halima Mdee anakusanya kodi kutoka kwa wananchi au ameskia wapi kuwa mbunge ndio mwenye maamuzi ya barabara gani ijengwe? Acha Umbulula wewe

Kwa kweeeeeli acha wale!
Kwa kuwa mdee yupo chadema basi HAKOSEI!
Asipotimiza ahadi zake ASIULIZWE!
Aaaaaaaaa jamani
Mshaambiwa aliahidi kuijenga katika kiwango cha lami.watu wakamuamini.ikawa moja ya sababu wakampa kura zao.
Inamaana wabunge wanaojenga Barbara kwenye majimbo yao wa kampuni za ujenzi?
KWELI NYANI WAPYA ILA MSITU ULEULE.

Napita tu mimi
 
level ya daimond ni wakina wema sepetu, kidoti na wengine wengene kama zari, kwa mdee kaingia chaka bovu yule ni taasisi..
 
Msishangae october ikawa Zari (CCM) vs. Halima Mdee (CHADEMA).......Brother ndo kaanza kampeni nn?
 
Hapo sasa kaka unatafuta kiki kwani halima mdee analalamika mara ngapi kuhusu ubovu wa miundo mbinu lakin kwakua ni upinzan hapewi nyenzo ulitaka ajenge na nn hiyo barabara mpe mshiko wako atajenga na hesabu utapewa siasa na unayofanya yametokea wapi?
 
mbona huduma hizo zikipelekwa mnawasifu wabunge? nakumbuka kuna threads nyingi tu humu zikiwasifu akina nyika dee na wengine kwa miundombinu iliyojengwa na serikali kwa nini pia wasilaumiwe kama haikujengwa? au mnamaana hata zile sifa mnazowapa wabunge wenu ni fake? double standard.
Tupo automatic kama upo manually kapime maleria!!
 
Hapo sasa kaka unatafuta kiki kwani halima mdee analalamika mara ngapi kuhusu ubovu wa miundo mbinu lakin kwakua ni upinzan hapewi nyenzo ulitaka ajenge na nn hiyo barabara mpe mshiko wako atajenga na hesabu utapewa siasa na unayofanya yametokea wapi?

Kama hoja ndio hiyo kwa kuwa yeye ni mpinzani barabara haijengwi basi wananchi hawana budi kumpa mtu wa CCM ili hitaji lao la barabara lifikiwe.

Mdee, time to go!
 
The Red Pen unagongwa na nyani mngese sana.CHAGGADOMO Mtachukia mpaka mama zenu mwaka huu kisa DJ KENGEZA KAHABA MBOWE
 
Last edited by a moderator:
CHAGGADOMO mnamchukia Kila mtu ninyi nani atawapenda.Kila mtu anayehoji kwenu ni ADUI
 
level ya daimond ni wakina wema sepetu, kidoti na wengine wengene kama zari, kwa mdee kaingia chaka bovu yule ni taasisi..

Ha ha ha ha ha kweli kingne asiwe ana ropoka asiyo yajua yata mu cost.
 
Wana Ukumbi,

Msanii maarufu nchini mwenye mafanikio makubwa katika sanaa ya mziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz, amevunja ukimya wake juu ya ubovu wa barabara iendayo Madale ambayo ipo kwenye jimbo la Kawe chini ya Halima Mdee.

Msanii huyo ameelekeza lawama zake kwa mbunge huyo wa kupitia tiketi ya CHADEMA kwa kuwa Halima Mdee aliahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa katika kipindi chake cha ubunge atahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami, lakini hadi hii leo barabara imejaa tope tu!

Diamond alieleza masikitiko yake huyo kupitia katika kituo cha Clouds TV pale alipoulizwa swali kuhusu makazi yake mapya yaliyopo katika jimbo la Kawe na ndipo hapo akafunguka kuhusu suala hilo la kero ya barabara ambalo lina muda mrefu alijashughulikiwa na mbunge Halima Mdee.





Mkuu,hivi wewe na Diamond mnafahamu kazi ya Mbunge,Diwani,serikali au Mahakama?
Wote tunaochangia humu tuulizane,maana imezoeleka kusumbua wabunge,Mbunge anakusanya kodi?
Wakulaumiwa ni ccm iliyopewa mamlaka kukusanya kodi badala ya kujenga barabara inalipa semina,badala ya kuweka umeme vijijini au wilaya zote inanunua magari yenye thamani ya milioni 200, gari moja.
Badala kujenga barabara inaanzisha wilaya mpya ili waliokosa fursa,waliomsaidia mkubwa kunadi sera na kuleta ushindi nao wapate angalau UDC
 
Jinsi Clouds Fm walivyo na mapenzi na CCM,yawezekana hata hicho alichoongea kaelekezwa na wana Clouds wenyewe..
 
kwahiyo km hakukua na lami ndo na mdee kaona asiweke lami? Hebu jifungueni pingu za fikra mbn jambo jepesi hivi mnataka kuwafanya wananchi mbulula! Hata km unakipenda chama ila kikiharibu sema ukweli.

Mdee ni iron lady hilo sikatai ila kwa hili la barabara anapaswa kulaumiwa acheni siasa za maji taka! Ni bora umwambie ukweli aumie kuliko kumwambia uongo acheke! Km ndo huwa mnashauriana hivi mnampoteza mdee kwa kutanguliza uchama mbele na kujifunga macho kana kwamba hamuoni!

Mkuu, nadhani umekurupuka kujibu!
  1. Je kwa uelewa wako ni Mdee ndio anajenga barabara? Na kabla ya Mdee mbona hiyo barabara haikujengwa? Je unaweza kuniambia Rita Mlaki alikuwa mbunge wa jimbo la Kawe- CCM kwa muda gani na bado hiyo barabara haikujengwa??
  2. Kuna mahali popote katika mtundiko wangu nimeonyesha mrengo wangu wa kisiasa?
  3. Thibitisha hizo siasa maji taka unazosema, maana sijatukana mtu zaidi ya kuuliza kama huko alikotokea kuna lami nikijua kuwa hata huko kuna mbunge pia kama Mdee!
  4. Huwa tunashauriana na nani..? Na je unaweza kuthibitisha kama mimi ni mwanachama wa hicho chama?

Usiandike kama uko ndotoni jaribu kufukiria kabla ya kutenda!
Pole kama ntakuboa.
 
Makamanda huyu dogo Diamond akili yake ni ndogo sana kuhusu suala zima la utatuzi wa matatizo ya wananchi ukilinganisha na Mhe,Mdee! Tatizo la dogo ni kwamba amesahau kuwa tatizo kubwa linasababishwa na serikali ya mshkaji wake wa pale Magogoni anayemtumbuiza kwa nyimbo za mapenzi badala ya yeye kutunga nyimbo ambazo zitagusa hali halisi ya maisha yetu sisi watanzania likiwa pamoja na hilo la barabara ya Madale!
 
huyu diamond ni chizi sana, ka collude na Enginer wake kuwa ajenge vibaya ile sehemu ya ukutani ili alipwe na lile shirika la BIMA.
 
We dimondi si unapesa wewe sa kwanini hicho kipande usijenge uwe mfano kwa wengine
 
mbona hata kikwete alihaidi kuijenga hiyo barabara kiwango cha lami!!
Diamond amlaumu kikwete sio mdee
 
Back
Top Bottom