Diamond Platnumz ameshinda tuzo ya MTV Msanii Bora Afrika, amgaragaza Burnaboy

Hupo sahihi mkuu, ila sio kujituma tu ni lazima uwe na mipango. Kuna msanii kila mwaka anaachia album 2 na singles 20 ila ata tuzo hana, sasa huyu ndio mfano mzuri wa anayejituma bila mipango
Unachotaka kuleta hapa ni ushabiki mondi ni kweli anajituma sana, lakini bado hana mziki mzuri kama mashabiki wake wanavyo tarajia
 
View attachment 2805428
Msanii Diamond Platnumz ameshinda tuzo ya Msanii Bora kutoka Afrika kwa mara ya 3 katika mashindano ya MTV Europe Music Award 2023 ( MTVEMA2023 )


diamond amewashinda
Asake, BurnaBoy   (Nigeria)
Libianca (Cameroon) na TylerICU (Dj wa Afrika Kusini).

Hongera sana sisi wanaJF tunathamini unavyotupa heshima kama taifa.

Tunasema Diamond ni Greatest of all time hapa East Africa.
Hajashinda category ya msanii bora, ameshinda best African act. Be careful siku nyengine
 
Unachotaka kuleta hapa ni ushabiki mondi ni kweli anajituma sana, lakini bado hana mziki mzuri kama mashabiki wake wanavyo tarajia
Ww muziki mzuri unaujua? Au mmezoea mtu akibana pua akiimba kila siku anateswa ndio muziki mzuri? Mond haimbi tena kwa ajili ya Tz tu bali anaimba kwa ajili ya Africa na dunia na ndio maana unaona shu inahit sana huko ughaibuni, sasa ww nikuulize tafsiri ya muziki mzuri ni nn? Nioneshe msanii mwenye huo muziki mzuri hapa Tz mwenye mafanikio kama au zaidi ya Mond
 
Diamond anafanikiwa kwa sababu anapenda anachofanya, ukipenda unachofanya hutoangalia umaarufu unaopata wala pesa unayoingiza, pesa na mafanikio haviwezi kukupumbaza ukaacha kufanya unachokipenda, ukifanya jambo kwa maslahi lazima utaridhika baada ya mafanikio kidogo kwa sababu hukipendi.

Siri ni moja vijana, penda unachofanya na fanya unachopenda, mafanikio huja kwa kile unachopenda kukifanya. Ni siri ya watu wote waliofanikiwa. Hakuna kazi inalipa kuliko nyingine, penda unachofanya.

hongera Diamond.
Ahsante Sana mkuu kwa kutupa hamasa
 
ifike mahali Rais wa nchi aache upendeleo katika kuinua sanaa na burudani katika hii nchi.

Sio mpira tu unaitangaza hii nchi, hizo Milioni 10 kwa kila goli nadhani ingewekwa vizuri kwamba

Kila Msaniii atakae peperusha bendera ya TAIFA hili basi nae apewe Kibunda.

Msanii sina maana ya Wanamuziki tu,au wacheza mpira tu,au waigizaji, Sanaa ipo pana.

ila hii kutoa hela kwenye Mipira na Magoli yanayofungwa na kuwaacha hawa wasaniii wanaopeperusha Bendera bila kitu si nzuri.

Rais anatakiwa atenge fungu kama alivyofanya kwenye mpira.

Hizi Juhudi zingeongezeka kwa kiasi kikubwa sana.

Diamond ifike mahali Apewe heshima yake na Hili taifa kwenye swala la kuitangaza hiii nchi.

Hongera Kwake, maswala mnasubiri AFE halafu mseme Akaagwe KARIMJEEE ni UNAFKI.

AFE mtoe ndege kwenda kuzika,Mtoe rambi rambi kubwa mgharamie mazishi huo ni ungengema Mpeni Mtu stahiki zake angali yuko macho anaona.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom