Utajiri wa Diamond Platnumz...

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Huu Ndio Utajiri wa Msanii Diamond Platnumz
by Frumence M Kyauke.

Nasibu Abdul Juma Issack,
almaarufu Diamond Platnumz, ni msanii Afrika mwenye kipaji kikubwa cha uimbaji vilevile ni msanii tajiri zaidi.
Umaarufu wake umeanza kuonekana mwaka 2010 baada ya kuachia albamu kwa jina Kamwambie.
Bingwa huyo wa muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania amefanikiwa kuachia vibao vikali na vinavyovuma ikiwemo Tetema, Inama, Sikomi, Marry You, Jeje, Waah, IYO na vinginevyo vingi vinavyokosha mioyo ya shabiki wake.
Kujituma na kutokukata tamaa ameweza kupata tuzo nyingi kama ifuatavyo:

Totals
Awards and nominations
AwardWinsNominations
HiPipo Music Awards10
Top Ten Tube Music Awards10
The Future Africa Awards10
Nzumari Awards10
MTV Europe Music Awards11
MTV Africa Music Awards15
BET Awards02
African Muzik Magazine Awards14
Tanzania Music Awards1711
IRAWMA Awards11
AFRIMMA Awards12
HIRONIMO MHAPA Awards01
Wins22
Nominations28

Anamiliki Record label kubwa ya WCB ambayo inavuna mafanikio makubwa na umaarufu mwingi hapa nchini Tanzania, media ya Wasafi Tv pamoja na Wasafi Fm, na mali nyingi za thamani ya mamilioni ya pesa ikiwemo gari aina ya Rolls Royce yenye thamani zaidi ya $343,350, pamoja na mali nyingine za thamani kubwa nyumba za kifahari nakadhalika. Kutokana na mafanikio yake, mali na deal nyingi, unahisi Diamond Platnumz ni tajiri kiasi gani?

Bila shaka Diamond Platinumz ni kipenzi cha wengi. Kando na kuwa na kipaji, ni mwanamuziki anayeiheshimu kazi yake na anayechapa na kuipenda kazi yake.

Kwa sababu hii pekee, ameweza kupata mafanikio ambayo hakutarajia miaka ya nyuma. Kutokana na mafanikio makubwa tunaweza kutambua kwa nini yeye ndiye mwanamuziki tajiri zaidi Tanzania.

Je, utajiri wa Diamond Platnumz ni wa kiasi gani? Mamilion ya shabiki zake hujiuliza swali hili mara kwa mara. Utajiri wa staa huyu wa Bongo Flava ni mkubwa kulingana na mapato ya kazi zake, anavyoishi, mali na uwekezaji. Mnamo mwaka wa 2014, utajiri wa Diamond Platnumz ulikisiwa kuwa wa thamani ya dola za Marekani $4 milion hivi sasa umeongezeka na kufikia zaidi ya $7 Million.
Diamond Platnumz
ni msanii namba moja kwa mapato mengi nchini Tanzania kutokana na mali anazomiliki.

Diamond Platnumz Net Worth.
Net Worth:$7 Million
Country:Tanzania
Source of wealth:Singer

images - 2021-10-27T201803.513.jpeg
 
Unaonaje ukituwekea na utajiri wako!
Mpaka sasa namiliki 1,000 ambayo nikienda shamba la wakulima wa machungwa naweza kupata machungwa 20 kwa sh 50
Napoyaleta mjini na kuuza 200 nitapata faida ya 150 x 20 = 3,000
Biashara hiyo ikifanyika kwa mwaka pasipo kutumia faida katika maswala mengine nadhani umepata picha halisi
 

Soma hii habari halafu ipimanishe na hiyo habari yako utajua ni wapi pana shida
Sasa tumeweza kuelewa kuwa habari kamilifu ni vyema iwe na chanzo maalumu.
Kama ilivyoambatanishwa na tovuti ya www.dailymail.co.uk na vyanzo vinginevyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom