Diallo amlipua Lowassa

Diallo amlipua Lowassa

Mkuu wangu, huyu Mzee Diallo ana busara sana!! Msome katikati ya mistari utamuelewa!! Anakipenda sana chama chake ndio maana amekipa ushauri "kuntu" usiopepesa macho!! Ccm fuateni ushauri wa huyu Mzee!!

sure mkuu vijana kwanini tuhangaike wakati kuna mapesabya bure kutoka kwa mamvi kweli ushauri wa Dialo ni kuntu.
 
Mkuu wangu, huyu Mzee Diallo ana busara sana!! Msome katikati ya mistari utamuelewa!! Anakipenda sana chama chake ndio maana amekipa ushauri "kuntu" usiopepesa macho!! Ccm fuateni ushauri wa huyu Mzee!!
Dialo ni mzee daa! Kumbe tunafanya mijadala watoto na wetu.
 
Toka lini Waziri uwa anafukuzwa kazi na Karibu Mkuu?kama nyie ndio wapambe wa Lowasa basi ndio maana mnampoteza kuanza kurusha mawe wakati yupo kwenye nyumba ya vioo.
Mwaka huu mtazusha mengi. Lakini mwlisho wa siku mtajua kwamba uwezo mdogo ndiyo unaw
Na hayo ya Diallo ni trailer tu, uchafu wa Lowassa ukianza kusemwa hatatazamwa ata usoni.Lowassa Hasafishiki.
Mwaka huu lazima mtungemimba za uongo.
 
kajiunga jf kwa ajili ya suala hilo tu, kila kitu zero isipokuwa posts ndo 1. JF babalao
 
Nadhani huna kumbu kumbu nakupa hii Dialo baada ya kutapeli Dola Laki moja ngoma ilipelekwa ikulu akaitwa Akiwa ni mteuliwa wa Rais lakini ni mtumishi wa umma boss wake ni huyo huyo unayemdharau, aliposomewa mashitaka yake mbele ya katibu Mkuu akaleta dharau ndipo Uteuzi wake ukatenguliwa , kumbuka Pia wakati mawaziri wanaapishwa katibu Mkuu huwasajiri kwenye utumishi wa umma Mara baada ya kuapishwa , katibu Mkuu ni mtu mkubwa kuliko unavyomfikiria. Najua umejitoa Fahamu endelea kumtetea baba yenu membe na wapambe wake akina Dialo.

Dialo ni academic dwarf na kinara wao is completely weak hauziki. Ni mtu wa kukurupuka akamuombe mzee Kitine msamaha kwa uongo aliyoupika dhidi yake.
 
Je ? Unawajua wana ccm wote waliotangaza nia ? Je? Umejiuliza ni kwa nini Lowasa pekee ndiye anaandamwa ? Hayo unayoyaita Madhambi hayapo kwa hao wengine ?!

Ndio maana tunasema ndani ya CCM hatuamini km kuna mtu anaweza kuivusha hii Nch tunachoshuhudia ni watu kugombania kwenda IKULU kwiba 50yrs watu bado tunazungumzia Ukosefu wa maDAWATI Realy? then watu hao waliokulia kwenye hiyo Serikali wanatudanganya kwamba wanaweza cc wengine hatuna Imani na mwana CCM yoyote,,,,,!!!
 
Kapiga penyewe wapi ? Povu lipi? Hivi kwa Akili yako ndogo Dialo anaweza kumsumbua lowasa ? Acha kuishi kwa mazoea jitambue huu ulimwengu wa Digtal watu Kama Dialo hawana nafasi ya kusikilizwa wanapuuzwa kwa kwenda mbele.
Njaa mbaya sana,minyoo imekujaa hadi kichwani. fanya kazi kijana jitume upate chako acha kushabikia wanaume wenzio, utaolewa!
 
Hadi raha! Mwakani ni burudani tupu kwani kitakacho leta burudani murua ni minyukano ndani ya CCM na hapo siri zote zitafichuka. Ni mwaka wa kuwajua wezi wote wa EPA "waliorudisha" pesa walizoiba na wasio "rudisha" Madhambi yote mpaka ya bosi wao tutayajua. Wavuane nguo tu tuone nani hajatahiriwa!
 
Tuhuma za Kundi la Makuwadi wa EL dhidi yangu hayana msingi wowote na kama ni kweli Edward amewapa waziseme kwangu na kuhusisha Mheshimiwa Rais ni mwendelezo wa EL kumdharau Rais ambaye alimpa madaraka makubwa na kosa likiwa kukubali ajiudhuru baada ya kufanya madudu aliyoyafanya. Huu ni mwendelezo wa kumsumbus Rais ambao ulianza tangu 2008 baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu. Anayoyasema haya sipendi kuyajibu ila kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sawa, imebidi niyajibu lakini nikizingatia kuwa sitaweza kuyajibu yale ninayoyajua chini ya kiapo:

1: Sijamtuma Mzee yeyote kwenda kwa Lowasa kwa sababu sio waziri mkuu tena na hata kama angekuwa bado waziri mkuu nisingeweza kumwambia mtu akaniombee vyeo kwa Lowassa. Hao wazee aliowataja wapo Mwanza na mnaweza kupata namba zao za simu na kuwauliza kama nilishawahi kufanya hivyo. Pili, mwaka 2003/4 haukuwa mwaka wa uchaguzi, ilikuwaje niende kuomba cheo wakati niliingia baraza la Mhe. Rais Mkapa 2001? Wakati huo Lowassa hakuwa waziri mkuu! Tatu, mwaka 2004 sijaonana na JK na Karamagi hajanishawishi kumuunga mkono JK mwaka 2005. Mimi ndiye niliyetumwa kumwambia Lowassa asigombee 2005 kwavile dhambi na tuhuma dhidi yake zilizotolewa na Mwalimu zilikuwa kwenye mioyo ya watanzania na asingeweza kupata kura za ushindi isipokuwa angempunguzia JK kura zake na wote kukosa. Karamagi tumekutana naye bungeni baada ya kuchaguliwa ubunge baada ya kifo cha Mhe. Kinyondo. Mimi nimezaliwa na kukua kwa kuzingatia nidhamu ya Kisukuma, sijalelewa kihuni kufika kumsema mtu kama JK. Namsema EL kwa sababu ni mchafu, na sasa sitayasema yaliyo mazito au machafu zaidi dhidi yake, hadi nitakapoona kweli kachukua fomu kugombea Urais! Mimi sijasema Lowassa alidhulumu CCM kupata hisa Vodacom, nilichosema CCM ilikuwa iwe mbia wa MTN, kampuni iliyonyimwa leseni wakijua fika kuwa ilikuwa ikisaidie chama, badala yake wakafanya njama kuvunja tume ya mawasiliano kihuni, na hapohapo wakaipatia vodacom leseni lowasa kwa kutumia watoto wake, alipata walikipata. Ushahidi kuhusu hili ni kampuni yake kupewa U-Super Dealer wa Vodacom ambayo uliwafanya wanufaike kwa kuuza simu nchi nzima.

Kama wanasema Lowassa ni mzima, naomba akakimbie uwanja wa Taifa azunguke hata mara moja kama hataishia ICU. Na kama ni mzima, anatumia fedha za nchi kwenda kutibiwa nini ujerumani kila wakati au Ujerumani nako siku hizi kuna waganga wa kienyeji? Pili kwanini alikwenda kuombewa kwa Emmanuel Ministries huko Nigeria? Kampeni za Urais zinahitaji afya nzuri, sio mzaha kuweka mgonjwa akatufia kwenye jukwaa! Kuhusu tuhuma ya rushwa toka kwa Kimaro, nina hakika Kimaro bado yupo hai, na kama ni mkweli aseme ukweli. Kimaro ni rafiki yangu na nilimshawishi akawekeza hoteli ya Nyumbani sasa ni JB Belmonte, Mwanza. Sijachukua fedha ili nimpatie kitalu kwavile yeye sio mwindaji na sijasikia kuwa ana hiyo biashara. Ninachofahamu ana mahoteli na ndiyo biashara yake. Rais yupo kama alishaniita kunieleza hilo anaweza akasema, ni mkweli. Tuhuma za mimi kuhongwa na Kimaro alizianzisha Lowassa baada ya mimi kutaka kumuondoa Mkurugenzi wanyama pori wizara ya Maliasili. Mkurugenzi huyo alikuwa na mahusiano naye na baadae walikuja kuoza watoto wao. Hilo kila mtanzania analifahamu, na alimtetea sana abaki wizarani wakati huo. Lowassa yupo kwenye mtandao wa yote yanayosemwa kuhusu wanyama pori. Pia tuhuma za kumtapeli aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Mhe Karume ndio nazisikia leo. Karume sijafika nyumbani kwake Zanzibar na wala hata alipokuwa Ikulu Zanzibar. Yupo na anaweza kuulizwa, ni mkweli atasema yaliyo kweli.

Huyo msichana anayesemekana nilimpa mimba, mhudumu wa Dodoma hotel, ndiyo namsikia leo, na kama yupo aniletee mtoto huyo kwani ndio nasikia kwenye watu wa Lowassa baada ya kuweweseka na machache tu tuliyoyaweka hadharani. Mwisho la kupewa fedha na mtuhumiwa wa IPTL nalo jipya simfahamu, labda Lowassa anamfahamu! Tatizo la huyu Lowassa, ni kupata URAIS, asipoupata sijui kama atabaki na afya ya kuridhisha. Anatuhumu watu tusiounga mkono jitihada zake tu, je wanaogombea watakuwa na hali gani mbele yake? Ushauri wa bure kwa wapambe wa Lowassa: Kuleni fedha yake maana ni halali yenu, fedha za kukwapua kwa njia zisizo halali ni haki ya kila mtu kuzitafuna, ila Urais hatopata.Kidumu Ccm.

WOTE nyinyi mko sawa tuhuma zako za vitalu unatukumbusha ulivyokuwa unatoa majibu ya kibabe bungeni sio wewe na wala huyo unaemtaka mnatufaa nyie mko zizi 1 mnatofautiana MAPEMBE TU, KOSA LA LOWASA NI KUKUBALI KUKAA KIMYA KIPINDI CHA SAKATA LA RICHMOND laiti angejua watamtosa sidhani kama angekubali na leo hii tungekuwa na rais mwingine tangu 2008, kwani alichofanya LOWASA ni kumuokoaJK asianguke ila ndio ivyo tena, JK richmond anaijua, wakati LOWASA anaongea kwenye kikao cha NEC JK alikuwa ameinamisha kichwa chini, MZEE MKAPA akamcheki akajua huyu ndio anahusika akamnong'oneza kwamba twende lunch waliporudi VUA GAMBA YA NAPE ikaishia hapo hawa wote wanaotajwa kuusaka URAIS hakuna msafi, maradhi ya EL kama kweli anaumwa tusiyatumie kishabiki MWENYEZI MUNGU ndie anajua HATUJUI KESHO YETU
 
Masika kwako na wajinga wachache lakini wajanja ni wengi hata uje na Uongo gani Hakuna atakayekusikiliza wala kukuamini kwani wewe si MUNGU , wewe Kesha buni , tengeneza, zusha, chonganisha fanya kila aina ya Uongo lakini mwisho wa siku Pesa za membe zitakuja kukutokea puani baada ya kufeli kazi aliyokutuma.

samahani mkuu! hapo nilimnukuu Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza Bw. Antony Diallo na sio maneno yangu!

  • :wacko:
 
Membe Ni kama popo, sio mnyama, sio ndege. Nani ampe uraisi popo? Akienda arabuni Ni muislam swala tano, akirudi bongo Ni mkristo. Huyu Joka la Mdimu Ni janga la kitaifa

Hapo umenena mkuu membe hafai kabisa kupewa nchi hajulikani kama muislam au mkristo ni hatari sana kwa uwahi wa taifa
 
Hapo umenena mkuu membe hafai kabisa kupewa nchi hajulikani kama muislam au mkristo ni hatari sana kwa uwahi wa taifa

Membe amehakikisha anamgombanisha JK na kila rafiki yake akitegemea urais ataupata kwa mgongo wa familia ya JK huku akisahau kuwa nani alimuweka JK madarakani.
 
Ndugu zangu kuna kitu nimeanza kujifunza na kukielewavizuri, na ukikiangalia au kukifuatilia kwa umakini utakigundua.Wengi wa wanaompingaLowasa katika safari yake ya katumaini kwa watanzania ni wale ambao wanahisi LOWASAakiupata Urais wa nchi yetu basi wao hawatapata nafasi yoyote ya uteuzi kwaniwanahisi LOWASA atakuja na safu ya viongozi yenye 90% watu wapya kabisa naambao hawakuweza kupata nafasi toka kwa viongozi waliopita na waliopo.Sasa hofuyao ni kukosa hizo nafasi ndio maana kila kukicha ni kumsema au kumuandikavibaya mh Lowasa.Wengine wanasubutu hata kupotosha kwa kutoa habari za uongo zaafya yake wakifikili watanzania wa leo hawajui nini kinaendelea katika nchiyetu.Mungu ndio anayejua nani atakuwa Rais na nani hatafika hata hicho kipindicha uchaguzi.
Pia nimegundua kundi linalompinga Lowasawanajaribu sana kuwachonganisha Rais Kikwete na Mh Lowasa kwa kusema maneno manenoili Rais Kikwete awe upande wa kundi lao katika mbio za kuwania uteuzi.Mimi nakumbuka kauli ya JKinayosema “akili za kuambiwa changanyana zako” kabla ya kufanya uamuzi.Dialo alitakiwa kuchanganya na zake iliafanye uamuzi sahihi

Diallo huwa hawezi kufikiri kwa kina yeye ni mwanachama wa ccm halafu ni kiongozi hakutakiwa kutoa kashfa kama hz ambazo hata hajasikia zikisemwa na el.cjui anafanya haya kwa faida ya kukiunganisha chama au kusambaratisha,naona ndo type akina paul makonda na wenzake samuel malchela
 
Back
Top Bottom