Diallo amlipua Lowassa

Diallo amlipua Lowassa

hivi lowassa ameshaanguka mara ngapi jukwaani?majizi mkija kuacha kulumbana mtaikuta chadema ikulu...

Hahahahahaha mkuu umenikumbusha mbali sana ya 2005 na 2010.....hahahahahahaha lakini mpaka sasa jamaa yuko fiti
 
Bado mengi tutayajua ,chadema tujipangeni

Mengi yapi utayajua ? Yale Yale ya kuishikwa Akili zenu na Membe au mengi yapi? Hivi ukiujua Uongo unajifunza nini? Je? Wajua Kuwa membe akijua amekulisha Uongo umeumeza na kusadiki kwa kasi pasipo kutafakari hujifariji sana. Kumbuka hayo mengi hayapo ccm tu yapo kila kona hata huko Upinzani siku wakitangaza nia napo wataibuka watu sampuli za akina membe watausambaza Umembe kila kona na Kuwa majanga kote.usishabikie usiyoyajua kwa kiina.
 
Uzuri ni kwamba Lowassa anawapuuza watu kama hawa wakina Diallo hana muda wa kubishana nao, maana siyo level zake wataangaika sana ila mwisho wa siku time will tell mwakani siyo mbali

Ukimya wa EL Kwa ma snitch kama hawa ni njia bora na sahihi, watahangaika sanaa wanachokifanya ni kama kupiga ngumi kinyago.

Yeye akse kimya lakini wapiga kura ndio tumeshapata taarifa sahihi.
 
2015 CHADEMA inachukua nchi....

Diallo kasema, Mengine hawezi kusema sasa, ANASUBIRI LOWASSA ACHUKUE FOMU. Huyu ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza mwenye ushawishi mkubwa sana. CCM imeficha siri nyingi sana za utafunaji wa hii nchi, kumbe haya makapuni ya mitandao ni mali za mafisadi.
 
nchi hii haiwezi kuongozwa na fisadi naikiwa hivyo mimi narudi kwetu Ukerewe.
Pi hatuwezi kuongozwa na familia moja tena kwa miaka 10, kwa hakika Membe hana lake....akawe rais wa WAMA , mama salma akistafu mwakani
 
Diallo kasema, Mengine hawezi kusema sasa, ANASUBIRI LOWASSA ACHUKUE FOMU. Huyu ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza mwenye ushawishi mkubwa sana. CCM imeficha siri nyingi sana za utafunaji wa hii nchi, kumbe haya makapuni ya mitandao ni mali za mafisadi.

Hana nguvu kabisa huyu jamaa msijidanganye mkuu......
 
Uzuri ni kwamba Lowassa anawapuuza watu kama hawa wakina Diallo hana muda wa kubishana nao, maana siyo level zake wataangaika sana ila mwisho wa siku time will tell mwakani siyo mbali

Ukimya wa EL Kwa ma snitch kama hawa ni njia bora na sahihi, watahangaika sanaa wanachokifanya ni kama kupiga ngumi kinyago.

Akae Kimya tu ale hela, aachane na mambo ya Urais atakufa kwa Pressure buree.
 
Wewe inaelekea Upeo wako ni mdogo Kama punje ya Ulezi, upo Nchi gani? Kwa haujui Kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais utumishi ndio mwajiri wa Utumishi wa Umma ,mawaziri na watumishi wote wa Serikali wapo kwenye Anga zake. Umemwabudu Dialo mpaka umecopy ujinga pasipo kujiongezea maarifa Binafsi .

Wewe kweli chizi..kama ata hujui mamlaka ya uteuzi na ubadilishaji wa mawaziri ipo kwa nani sijui utajua kipi??bure kabisa..

Kwa kukusaidia mamlaka ya uteuzi wa waziri na naibu wake ni ya Rais mwenyewe akishauriana na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, katu Katibu Mkuu Kiongozi hawezi kumfuta kazi Waziri wala Naibu Waziri.

Kama una mtoto aliye shule ya msingi basi muulize atakufundisha vizuri, jinga wewe..
 
Yeye akse kimya lakini wapiga kura ndio tumeshapata taarifa sahihi.
Kama tulivyopata taarifa ya mama salma kutaka kutuletea Membe, walai kitu kama hicho hakitakaa kitokee duniani eti mke wa rais atuchaguliye president.....never on earth na msahau kabisa
 
..........Namsema EL kwa sababu ni mchafu, na sasa sitayasema yaliyo mazito au machafu zaidi dhidi yake, hadi nitakapoona kweli kachukua fomu kugombea Urais!..........kumbe hii ni rasharasha, masika bado!

Masika kwako na wajinga wachache lakini wajanja ni wengi hata uje na Uongo gani Hakuna atakayekusikiliza wala kukuamini kwani wewe si MUNGU , wewe Kesha buni , tengeneza, zusha, chonganisha fanya kila aina ya Uongo lakini mwisho wa siku Pesa za membe zitakuja kukutokea puani baada ya kufeli kazi aliyokutuma.
 
DIALO KAJIBU HIVI;

J
"Tuhuma za Kundi la Makuwadi wa EL dhidi yangu hayana msingi wowote na kama ni kweli Edward amewapa waziseme kwangu na kuhusisha Mheshimiwa Rais ni mwendelezo wa EL kumdharau Rais ambaye alimpa madaraka makubwa na kosa likiwa kukubali ajiudhuru baada ya kufanya madudu aliyoyafanya. Huu ni mwendelezo wa kumsumbus Rais ambao ulianza tangu 2008 baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu. Anayoyasema haya sipendi kuyajibu ila kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sawa, imebidi niyajibu lakini nikizingatia kuwa sitaweza kuyajibu yale ninayoyajua chini ya kiapo:

1: Sijamtuma Mzee yeyote kwenda kwa Lowasa kwa sababu sio waziri mkuu tena na hata kama angekuwa bado waziri mkuu nisingeweza kumwambia mtu akaniombee vyeo kwa Lowassa. Hao wazee aliowataja wapo Mwanza na mnaweza kupata namba zao za simu na kuwauliza kama nilishawahi kufanya hivyo. Pili, mwaka 2003/4 haukuwa mwaka wa uchaguzi, ilikuwaje niende kuomba cheo wakati niliingia baraza la Mhe. Rais Mkapa 2001? Wakati huo Lowassa hakuwa waziri mkuu! Tatu, mwaka 2004 sijaonana na JK na Karamagi hajanishawishi kumuunga mkono JK mwaka 2005. Mimi ndiye niliyetumwa kumwambia Lowassa asigombee 2005 kwavile dhambi na tuhuma dhidi yake zilizotolewa na Mwalimu zilikuwa kwenye mioyo ya watanzania na asingeweza kupata kura za ushindi isipokuwa angempunguzia JK kura zake na wote kukosa. Karamagi tumekutana naye bungeni baada ya kuchaguliwa ubunge baada ya kifo cha Mhe. Kinyondo. Mimi nimezaliwa na kukua kwa kuzingatia nidhamu ya Kisukuma, sijalelewa kihuni kufika kumsema mtu kama JK. Namsema EL kwa sababu ni mchafu, na sasa sitayasema yaliyo mazito au machafu zaidi dhidi yake, hadi nitakapoona kweli kachukua fomu kugombea Urais! Mimi sijasema Lowassa alidhulumu CCM kupata hisa Vodacom, nilichosema CCM ilikuwa iwe mbia wa MTN, kampuni iliyonyimwa leseni wakijua fika kuwa ilikuwa ikisaidie chama, badala yake wakafanya njama kuvunja tume ya mawasiliano kihuni, na hapohapo wakaipatia vodacom leseni lowasa kwa kutumia watoto wake, alipata walikipata. Ushahidi kuhusu hili ni kampuni yake kupewa U-Super Dealer wa Vodacom ambayo uliwafanya wanufaike kwa kuuza simu nchi nzima.

Kama wanasema Lowassa ni mzima, naomba akakimbie uwanja wa Taifa azunguke hata mara moja kama hataishia ICU. Na kama ni mzima, anatumia fedha za nchi kwenda kutibiwa nini ujerumani kila wakati au Ujerumani nako siku hizi kuna waganga wa kienyeji? Pili kwanini alikwenda kuombewa kwa Emmanuel Ministries huko Nigeria? Kampeni za Urais zinahitaji afya nzuri, sio mzaha kuweka mgonjwa akatufia kwenye jukwaa! Kuhusu tuhuma ya rushwa toka kwa Kimaro, nina hakika Kimaro bado yupo hai, na kama ni mkweli aseme ukweli. Kimaro ni rafiki yangu na nilimshawishi akawekeza hoteli ya Nyumbani sasa ni JB Belmonte, Mwanza. Sijachukua fedha ili nimpatie kitalu kwavile yeye sio mwindaji na sijasikia kuwa ana hiyo biashara. Ninachofahamu ana mahoteli na ndiyo biashara yake. Rais yupo kama alishaniita kunieleza hilo anaweza akasema, ni mkweli. Tuhuma za mimi kuhongwa na Kimaro alizianzisha Lowassa baada ya mimi kutaka kumuondoa Mkurugenzi wanyama pori wizara ya Maliasili. Mkurugenzi huyo alikuwa na mahusiano naye na baadae walikuja kuoza watoto wao. Hilo kila mtanzania analifahamu, na alimtetea sana abaki wizarani wakati huo. Lowassa yupo kwenye mtandao wa yote yanayosemwa kuhusu wanyama pori. Pia tuhuma za kumtapeli aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Mhe Karume ndio nazisikia leo. Karume sijafika nyumbani kwake Zanzibar na wala hata alipokuwa Ikulu Zanzibar. Yupo na anaweza kuulizwa, ni mkweli atasema yaliyo kweli.

Huyo msichana anayesemekana nilimpa mimba, mhudumu wa Dodoma hotel, ndiyo namsikia leo, na kama yupo aniletee mtoto huyo kwani ndio nasikia kwenye watu wa Lowassa baada ya kuweweseka na machache tu tuliyoyaweka hadharani. Mwisho la kupewa fedha na mtuhumiwa wa IPTL nalo jipya simfahamu, labda Lowassa anamfahamu! Tatizo la huyu Lowassa, ni kupata URAIS, asipoupata sijui kama atabaki na afya ya kuridhisha. Anatuhumu watu tusiounga mkono jitihada zake tu, je wanaogombea watakuwa na hali gani mbele yake? Ushauri wa bure kwa wapambe wa Lowassa: Kuleni fedha yake maana ni halali yenu, fedha za kukwapua kwa njia zisizo halali ni haki ya kila mtu kuzitafuna, ila Urais hatopata.Kidumu Ccm."
n
Nawashangaa hawa mabwana na makuwadi wa WAMA. Naona maji yamewafika shingoni. Karam
 
Siamini kama kweli ni Dialo aliyeandika haya, Nimesoma na kuishi kwa muda na wasukuma, ni watu smart sana . Kama ndiye aliyeandika haya amepotoka sana na hana pa kuficha uso wake.
Ni kweli kuu......ila kwa akili za Diallo mimi sishangai ingawa wasukuma ni watulivu na smart kama unavyonena......amefanya hili kwa msukumo wa makundi kumbe hajui anazidi kujichafulia, na mpaka issue zake za ubakaji, mauhaji, na ulawiti sasa tunazisoma humu jamvini.
 
Wote hawa ni ccm!??? Sasa katika mazingira haya wanapata wapi muda kupanga mustakabali wa taifa?

Sawa ni vita ya panzi.... na nadhani yeyote atakayepitia hapa, kusoma gazetini, kusikia redioni au kuambiwa na jamaa yake basi ataona umuhimu wa kuchagua watu au chama kisicho hata na ofisi lakini kina watu waadilifu kuliko chama chenye watu najisi kama ccm.
 
Mh! I always wondered how Rostam and Lowassa got into Vodacom but now I see the connection!!! Aisee Mamvi ni hatari yangu macho! Nilishawahi kusema huyu jamaa hasafishiki labda wamsafishe na bati lakini si maji wala mafuta yatamfaa.
 
n
Nawashangaa hawa mabwana na makuwadi wa WAMA. Naona maji yamewafika shingoni. Karam
hahahahaha wanatapa tapa sana mkuu.....nasikia kule ujerumani walipoenda kufatilia ripori ya afya ya Lowassa wamefukuzwa kama mbwa...hahahahaha nimecheka sana aisee, ndio mambo ya akili ndogo hizi mkuu, wenyewe walifikiri unaweza kupata data kama hizo nchi za ulaya hahahahahaha hawa majamaa wanachekesha sana
 
hii ni kali na kama ni kweli tutaona mengi sana mpaka 2015.Mimi naona wanamwonea lowasa bure tuu na hii ni kwa sababu wanamjua ni mpambanaji mzuri akiingia madarakani itakula kwa wengi,sasa wanaanza kumwogopa.
 
1.Alphatel
2.Alpha Schools
3.Alpha house

Mwaka huu tongotongo zitatutoka sana machoni sababu ya hizi mbio zao
 
Sijui kama kuna uchafu zaidi ya kuuza unga (madawa ya kulevywa), au pembe za ndovu......je ni Lowassa au kambi yake waliokamatwa China na madawa ya kulevya? nakuachia ujibu mwenyewe

Pili yule mzungu aliyekufa juzi MayFair Plaza kabla ajafa tarehe 18/9/2014, saa kumi na moja jioni alionekana na nani maeneo ya Sea Cliff ? jibu mwenyewe....KUMBUKA ALIKUFA NA MADAWA YA KULEVYA AKIWA ANAOGA......DETAILS ZIKO WAZI na soon mtaona washirika wake wa sembe humu humu, just stay tuned


Vita ya kuchafuana itamuathiri zaidi Lowassa kuliko yoyote mwingine maana hakuna mchafu kati ya wagombea kuliko Lowassa, Lowassa ni mzizi wa uchafu na ufisadi hapa nchini.
 
Ushauri wa bure kwa wapambe wa Lowassa: Kuleni fedha yake maana ni halali yenu, fedha za kukwapua kwa njia zisizo halali ni haki ya kila mtu kuzitafuna, ila Urais hatopata.Kidumu Ccm.​

Mzee Diallo, tatizo wakishakula hela ya EL wanacheua cheua hovyo na kuhara hovyo mitaani na mitandaoni JF..
 
..........Namsema EL kwa sababu ni mchafu, na sasa sitayasema yaliyo mazito au machafu zaidi dhidi yake, hadi nitakapoona kweli kachukua fomu kugombea Urais!..........kumbe hii ni rasharasha, masika bado!

Hii trailer tu...Lowassa ni mzizi wa uchafu wa kifisadi hapa nchini kwa sasa.
 
Back
Top Bottom