Dhihaka ya karne: Eti wanataka kuhama CHADEMA

Kuna wafia chama wanasema UKUTA umefanikuwa maana yake udikteta umeondolewa na mikutano na maandamano yameruhusiwa kama ni hivyo hongereni Chadema
Kitulo hao watakuwa mataahira kama ni kweli usemayo
 
Baada ya jana kuahirishwa maandamano ya UKUTA kwa mwezi mmoja zimefumuka post za kukejeli hiki kitendo

Kila mtu kasema lake, lakini wengi wakijikita kwenye kusema kuwa eti

-CHADEMA ni vigeugeu
-CHADEMA ni mabingwa wa kubadili gia angani
-CHADEMA inapoteza mwelekeo chini ya Lowassa (utafikiri ndio mwenyekiti)

Kejeli ni nyingi kweli na hili halina tatizo kwakuwa wale waliokuwa wamejiandaa kuumiza wananchi wasio na hatia hawataweza tena kufanya hivyo! Maandalizi yalikuwa mengi na kabambe mno ya kukipaka damu chadema kama maandamano haya yangefanyika
Kichekesho na dhikaha ya kukera sana ni wale wanaojifanya kutaka kuihama CHADEMA eti tu kwakuwa wameahirisha maandamano! Hilo tu likufanye uhame chama? Maandamano yangefanyika wewe ungeenda? Uhame Chadema uende chama gani? CCM? kama kuhama chama kungekuwa rahisi hivyo Lipumba asingeng'ang'ania cuf....unazi wetu uko nyuma ya keyboard tuu lakini waandamanaji wa kweli wasioogopa chochote iwe virungu iwe maji ya kuwasha ile jela, hawapo hapa na hawa wamekubaliana na maamuzi! Hakuna haja ya kutishia kuhama FANYA SASA

Dhima ya CHADEMA haikuwa kuandamana!maandamano huwa silaha ya mwisho kabisa kwenye nchi ya kidemokrasia kama njia zote zikishindikana

CHADEMA kwenye hili wamefanikiwa sana tena sana, harakati za ukuta zimeleta matunda mengi

Maamuzi mengi ya kibabe yamepungua ama kubatilishwa

Kupayuka payuka kumepungua

Utawala wa sheria unaanza kurejewa

Utawala ulioanza kujisahau umekuwa makini zaidi sasa

Viongozi wengi wameamua kuingia kwenye mazungumzo

CHADEMA SASA IMEANZA KUSIKILIZWA NA ITASILIKOLIZWA..hii ndio ilikuwa dhima ya yao KUSIKILIZWA

CHADEMA itasikilizwa bila kusababisha madhara kwa wananchi bila uharibifu wa mali na kwa gharama bei chee kabisa

CHADEMA imepiga hatua kumi zaidi mbele waliokamatwa kwa mashtaka ya kutunga na kunjuka ni viongozi tuu raia hawafiki watano! Huu ni ushindi mkubwa sana
Kama unahama CHADEMA Salam zao huko uendako

Mshana !!!!!!!!
WAAACHE WAONDOKEEEEEEEEE, WAMEINGIA CDM WAKATI IKIWA NA SPEED YA 80K/H , WANAONDOKA CDM IKIWA NA SPEED YA 120K/H
 
Chama Cha Matamko, endeleeni kujifariji kwa maneno hayo.
 
Hivi Tanzania idadi kubwa ya watu ni mwana CHADEMA hadi wasijikie vibaya kiasi hicho baada ya maandamano kuhairishwa..??
Hongereni sana CHADEMA... Mmekuwa wabunifu kiasi cha kupata promo bila kutumia gharama zenu..!!
 
Hata hao viongozi wa serikali waliokuwa wana msimamo mkali nape, makonda, mwigulu, wote hawakuwa na nia njema na Rais wao. Kuna kilichokuwa kimejificha cha kiccm lakini kitendeke kwa mgongo wa chadema 🙂 🙂 🙂 sorry imekula kwenu. All chadema wanted wa "mesage sent" and that was done 100 and 50% 🙂 🙂 🙂
 
Kamanda umenena vema,,,ntarudi badaye,ila kwa ufupi walioumia ni wale wenye maslahi binafsi na wenye kuvizia vyeo vya kisiasa....CCM ndo wameumia zaidi
 
kwa wengi ambao hawaelewi falsafa ya liberation naomba muwemnasoma hata historia za waasisi kama hawa,leo naona comment nyingi sana wengi kabla ya siku ya jana na leo walikuwa kimya leo naona wanaibuka na unabii..!!
thomas-sankara-you-cannot-kill-ideas-e1433349587780.jpg
 
CHADEMA ni chama cha wapinzani maarufu.
lakini viongozi na wanachama wa ngazi za juu wa CHADEMA sio wapinzani sahihi wa CCM..
kama mtashindwa kuunda chama kingine bora zaidi na viongozi bora zaidi
basi bora Baadhi ya viongozi wakiache Chama Kwenye mikono salama..
Hapo ndipo tutakapokuwa na matumaini na upinzani kwa CCM.

vinginevyo ni sawa na kutoa boriti jichoni kwa mwenzio, wakati una kibanzi jichoni pako.
au kung'ang'ania nyumba inayovuja kisa, kwako kuna ufa wa kubomoka..
 
GHANI TAFADHALI
Maneno umeyasema, hakika umeyapanga,
Hekima tumeisoma. Wala sii ya kutunga,
Ukuta pambo la uma, Lumumba wanasimanga
Ada ya mja kunena, kwetu muungwa vitendo.
 
CHADEMA ni chama cha wapinzani maarufu.
lakini viongozi na wanachama wa ngazi za juu wa CHADEMA sio wapinzani sahihi wa CCM..
kama mtashindwa kuunda chama kingine bora zaidi na viongozi bora zaidi
basi bora Baadhi ya viongozi wakiache Chama Kwenye mikono salama..
Hapo ndipo tutakapokuwa na matumaini na upinzani kwa CCM.

vinginevyo ni sawa na kutoa boriti jichoni kwa mwenzio, wakati una kibanzi jichoni pako.
au kung'ang'ania nyumba inayovuja kisa, kwako kuna ufa wa kubomoka..
wapinzani sahihi wako vipi,unaweza kutoa ufafanuzi kidogo labda na mimi nikuelewe katika point yako ulitaka kumaanisha nini
 
Kuna watu wa ajabu sana!! kuna watu walitaka kuona kwenye TV na Magazeti picha za maiti na watu walio jeruhiwa vibaya. Some people have evil and delvish mind.
 
CHADEMA ni chama cha wapinzani maarufu.
lakini viongozi na wanachama wa ngazi za juu wa CHADEMA sio wapinzani sahihi wa CCM..
kama mtashindwa kuunda chama kingine bora zaidi na viongozi bora zaidi
basi bora Baadhi ya viongozi wakiache Chama Kwenye mikono salama..
Hapo ndipo tutakapokuwa na matumaini na upinzani kwa CCM.

vinginevyo ni sawa na kutoa boriti jichoni kwa mwenzio, wakati una kibanzi jichoni pako.
au kung'ang'ania nyumba inayovuja kisa, kwako kuna ufa wa kubomoka..
Mnacho TLP mnataka nn tena??
 
Baada ya jana kuahirishwa maandamano ya UKUTA kwa mwezi mmoja zimefumuka post za kukejeli hiki kitendo

Kila mtu kasema lake, lakini wengi wakijikita kwenye kusema kuwa eti

-CHADEMA ni vigeugeu
-CHADEMA ni mabingwa wa kubadili gia angani
-CHADEMA inapoteza mwelekeo chini ya Lowassa (utafikiri ndio mwenyekiti)

Kejeli ni nyingi kweli na hili halina tatizo kwakuwa wale waliokuwa wamejiandaa kuumiza wananchi wasio na hatia hawataweza tena kufanya hivyo! Maandalizi yalikuwa mengi na kabambe mno ya kukipaka damu chadema kama maandamano haya yangefanyika
Kichekesho na dhikaha ya kukera sana ni wale wanaojifanya kutaka kuihama CHADEMA eti tu kwakuwa wameahirisha maandamano! Hilo tu likufanye uhame chama? Maandamano yangefanyika wewe ungeenda? Uhame Chadema uende chama gani? CCM? kama kuhama chama kungekuwa rahisi hivyo Lipumba asingeng'ang'ania cuf....unazi wetu uko nyuma ya keyboard tuu lakini waandamanaji wa kweli wasioogopa chochote iwe virungu iwe maji ya kuwasha ile jela, hawapo hapa na hawa wamekubaliana na maamuzi! Hakuna haja ya kutishia kuhama FANYA SASA

Dhima ya CHADEMA haikuwa kuandamana!maandamano huwa silaha ya mwisho kabisa kwenye nchi ya kidemokrasia kama njia zote zikishindikana

CHADEMA kwenye hili wamefanikiwa sana tena sana, harakati za ukuta zimeleta matunda mengi

Maamuzi mengi ya kibabe yamepungua ama kubatilishwa

Kupayuka payuka kumepungua

Utawala wa sheria unaanza kurejewa

Utawala ulioanza kujisahau umekuwa makini zaidi sasa

Viongozi wengi wameamua kuingia kwenye mazungumzo

CHADEMA SASA IMEANZA KUSIKILIZWA NA ITASILIKOLIZWA..hii ndio ilikuwa dhima ya yao KUSIKILIZWA

CHADEMA itasikilizwa bila kusababisha madhara kwa wananchi bila uharibifu wa mali na kwa gharama bei chee kabisa

CHADEMA imepiga hatua kumi zaidi mbele waliokamatwa kwa mashtaka ya kutunga na kunjuka ni viongozi tuu raia hawafiki watano! Huu ni ushindi mkubwa sana
Kama unahama CHADEMA Salam zao huko uendako
Mkuu pokea like yangu kwanza .
Umeongea point sana natamani wale wapenzi vindakindaki wa chama teule waelewe haya ulioyaelezea hapa.Dhima ya uongozi wa CHADEMA imefanikiwa ingawa wanataka kuthibitishiwa zaidi ndio maana wakasema wanatoa tena mwezi mmoja baada ya hapo ndio kitaeleweka .
 
CHADEMA ni chama cha wapinzani maarufu.
lakini viongozi na wanachama wa ngazi za juu wa CHADEMA sio wapinzani sahihi wa CCM..
kama mtashindwa kuunda chama kingine bora zaidi na viongozi bora zaidi
basi bora Baadhi ya viongozi wakiache Chama Kwenye mikono salama..
Hapo ndipo tutakapokuwa na matumaini na upinzani kwa CCM.

vinginevyo ni sawa na kutoa boriti jichoni kwa mwenzio, wakati una kibanzi jichoni pako.
au kung'ang'ania nyumba inayovuja kisa, kwako kuna ufa wa kubomoka..

Utasemaje wenzio si wapinzani sahihi wakati wewe si mpinzani...??
Kama umevimbiwa nenda panapokustahili..
 
Hivi nyie watu mnawafikiliaje watu wenzenu. Mnawafikiria kuwa ni mambumbu kiasi cha kuwaongopea namna hiyo?

Kwani ni nani alisema atafanya maandamano na mikutano tena isiyo na kikomo kuanzia tarehe mosi september?

Kama ilijuwa kuwa maandamano si kitu kizuri kitamwaga damu kwanini hawKughairisha tangia zamamni au kwanini waliamua kutumia njia hoyo wakati njia za amani zipo kutatua mogogoro?

Makamanda wenu wangapi wako Rumande hadi sasa?

Utawala upi wa sheria ulioanza kutumika ambao zamani haukutumia?

Chedema gani imeanza kusikilizwa, tena imeanza kusikilizwa na nani? Wakati mtaalamu wako wa kubadili gia angani jana kasema kanpbisaaa wazi kuwa Raisi alishakataaga kuongea na chadema...

We unayemuona kuwa ni mbumbu kama wewe ni nani hasa?

Acha kupenda sana kijana. Usipokubali kumshauri kiongozi wako na ukawa ni mjumbe ndiyooooo hautakuwa na tofautii sana na ccm.

Mlishasema tatzo la wanzania ni kusherehekea kila kitu kinachosemwa na kufanywa na Magufuri, na ndio maana anafanya mambo pasipo kushauriwa...

Sasa na wewe na wenzio msipomshauri kiongozi wenu ( mataalamu wa gia) naye ataendelea kufanya mambo ya kijinga na kukurupuka kama mkuu wa kaya na hatimaye chama kitakosa watu na wafiasi kila uchwao...
Amka wewe...
Umeandika vizuri sana kiongozi. Wamesikilizwa na nani?(labda viongozi wa dini wasio na majina). Demokrasia ipi imeanza kutamalaki? Wanawasema hao maccm kwa kuwa watu wa "ndiooooo" huku nao wanakuwa watu wa ndio kwa uongozi wao bila kuhoji.

Hivi walivyoweka ukuta wao, hawakujua kuwa kuna hatari ya kumwaga damu, au waliiona jana? Walishaambiwa jamaa hajaribiwi, I believe yote ni woga tu.
 
Back
Top Bottom