hivi wewe, unadhani maandamano ni mazuri! Hivi unajua ni watu wangapi waliumizwa na kupoteza maisha yao kwa hicho unacho msifia dr slaa?
Kuwa kiongozi wakati mwingine inahitaji kutumia Busara katika kutafakari na kufanya maamuzi na siyo kukurupuka.
Wewe ungefurai kuona watanzania wenzako leo wakichezea kichapo na taifa kugeuka uwanja damu?
Hakuna mwenye Akili timamu Atakaye wadhiaki viongozi wa chadema kwa uamuzi wa busara waliouchukua wa kusitisha zoezi lao.
Pia nichukue fursa hii kumpongeza sana Ndugu Saimon Siro, kamanda wa kanda maalum, kwa kuwapongeza viongozi wa chadema kwa kuonyesha uzalendo wa kusitisha Maandamano yao.
Niukweli usiopingika kwamba hata polisi hawapendi kupiga raia wao maana wao wamewekwa kuwalinda raia na siyo kuwaumiza.
Mungu Ibariki Tanzania.