Konseli Mkuu Andrew
JF-Expert Member
- May 10, 2013
- 740
- 855
Dereva gari limemshindwa kila kukicha ni kumtupia lawama dereva aliyepita eti ubovu huu wa gari ulisababishwa na yeye pamoja na wasaidizi wake amesahau naye alikuwa ni kondokta wa dereva mkuu, alishindwaje kumshauri.Chaajabu anaendesha gari ovyo ovyo bila hata ya umakini hasikilizi abiria ndani yeye yupo busy kusikiliza madereva anaopishana nao barabarani wakimpa HI.
Gari limekuwa bovu taa haziwaki na zikiwaka basi hatuna uhakika wa kuendelea kuwaka kwa muda wote hali inayopelekea abiria kukaa giza, huduma ya maji ya uhakika ndani bus hakuna tena tofauti na dereva aliyepita alikuwa mkali kwa mkuu wa idara ya ugawaji maji.Dereva aliyepita aliacha mradi wa utengenezaji wa betri ambapo alisema kuzimika kwa taa na kutofanya kazi kwa AC ni kukosekana kwa betri N200 na alituacha katika hatua za mwisho za ununuzi ila baada ya huyu dereva mpya kuja hali imekuwa tete anatamani tuendelee kuazima mabetri toka kwa majirani hataki kabisa tujitegemee.
Cha ajabu haka kondakta wake yupo yupo kazi kuvaa kaundi suti tuu na kupaka piko ameshasahu wajibu wake ni kumkumbusha na kumshauri dereva juu ya mwenendo mzima wa gari.Alikuwa machachari kweli kweli alipokuwa turn boy wakati ule alikuwa mbunifu wa mambo lukuki ila siku hizi kawa kama zoba.
Abiria tunasema dereva achunguzwe je ana leseni halali ya kuendesha ili gari au ana leseni Class D halafu tumempa Bus, hii safari ni ya masafa marefu sio kama ye anavyo fikiri safari hii inaenda kuamua hatma ya watoto zetu na wajukuu zetu.
Fasihi ni kazi ya sanaa.
Nimekuwa mwanafasihi