Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 2,209
- 4,706
Wadau hamjamboni nyote?
Tukio husika Inadaiwa limetokea jana Jumanne februari 27,2024 maeneo ya Mbezi Beach Afrikana likihusisha gari la Serikali na Pikipiki ya Dawasco iliyokuwa na wafanyakazi wawili akiwemo wa kiume aliyekuwa akiendesha
Inadaiwa Dereva wa gari hilo aliyekuwa akiongea na simu alipofika Afrikana aliigonga Pikipiki hiyo kisha kuanza kutoka lugha za kebehi kwa madereva wa bodaboda bila kujutia au hata kuomba radhi Kwa kitendo alichokifanya
Inadaiwa kitendo hicho cha kutoka lugha ya kebehi huku akiwa anaendelea kuongea kiliwakera wengi walioshuhudia ajali hiyo
Inadaiwa mfanyakazi huyo wa kike aliyekuwa amekaa nyuma ya Pikipiki iliyogongwa alimfuata dereva wa gari na kumchapa vibao na kumpiga vichwa kabla ya watu kuamua
Mtoa taarifa wetu aliondoka eneo la husika kuendelea na majukumu mengineyo