Dereva gari limemzidi uwezo, Leseni ichunguzwe

Konseli Mkuu Andrew

JF-Expert Member
May 10, 2013
740
855
Dereva gari limemshindwa kila kukicha ni kumtupia lawama dereva aliyepita eti ubovu huu wa gari ulisababishwa na yeye pamoja na wasaidizi wake amesahau naye alikuwa ni kondokta wa dereva mkuu, alishindwaje kumshauri.Chaajabu anaendesha gari ovyo ovyo bila hata ya umakini hasikilizi abiria ndani yeye yupo busy kusikiliza madereva anaopishana nao barabarani wakimpa HI.

Gari limekuwa bovu taa haziwaki na zikiwaka basi hatuna uhakika wa kuendelea kuwaka kwa muda wote hali inayopelekea abiria kukaa giza, huduma ya maji ya uhakika ndani bus hakuna tena tofauti na dereva aliyepita alikuwa mkali kwa mkuu wa idara ya ugawaji maji.Dereva aliyepita aliacha mradi wa utengenezaji wa betri ambapo alisema kuzimika kwa taa na kutofanya kazi kwa AC ni kukosekana kwa betri N200 na alituacha katika hatua za mwisho za ununuzi ila baada ya huyu dereva mpya kuja hali imekuwa tete anatamani tuendelee kuazima mabetri toka kwa majirani hataki kabisa tujitegemee.

Cha ajabu haka kondakta wake yupo yupo kazi kuvaa kaundi suti tuu na kupaka piko ameshasahu wajibu wake ni kumkumbusha na kumshauri dereva juu ya mwenendo mzima wa gari.Alikuwa machachari kweli kweli alipokuwa turn boy wakati ule alikuwa mbunifu wa mambo lukuki ila siku hizi kawa kama zoba.

Abiria tunasema dereva achunguzwe je ana leseni halali ya kuendesha ili gari au ana leseni Class D halafu tumempa Bus, hii safari ni ya masafa marefu sio kama ye anavyo fikiri safari hii inaenda kuamua hatma ya watoto zetu na wajukuu zetu.

Fasihi ni kazi ya sanaa.
Nimekuwa mwanafasihi
 
Dereva alipewa ushauri akapuuza, baada ya kupata leseni ya kuendesha lile basi ilitakiwa afanye yafuatayo;
~major engine overhaul, ilitakiwa abadilishe kila kitu kuanzia PM, IGP, Ministers na wengine ili apate timu nzuri ya kuendana nayo
~ilitakiwa basi lipigwe rangi nyingine ili kuendena na route aliyoichague
~ kuimarisha usafi wa basi, kuwapa abiria uhuru wa kutoa mawazo yao, na kuwa na lugha nzuri na dereva wenzake na kuruhusu ushirikiano na ushindani na mabasi mengine
~ kuzuia gharama za ovyo za kupandisha nauli, maana tangu apate leseni nauli kila siku inapanda
~atafute vijana wapya, na wenye uwezo wa kumuongoza, achane na hawa wa kila siku akina Mwigulu
~afute kesi kesi ya Mbowe
 
Gari linaenda kumuangusha kama unavyojua fahamu dereva ni mmoja kwa sasa Ila gari likianguka mashuhuda na miongoni mwa abiria atakuwa dereva wa hilo gari.

Kwa sasa waendelee kumshauri na kumtazama dereva huyo.

Miaka ya zamani kuna dereva wa hilo gari lilimuangusha ila abiria wakabaki katika hali tofauti tofauti.

Dereva ushauri wangu kwako ongeza umakini na daraja katika uendeshaji.
 
Si walisema alikuwa hashauriki?. Kwamba ukimshauri ndio umeharibu kabisaaa. Kama huyu dereva mpya analalamikia mwenendo wa dereva aliyepita basi malalamiko yake sio ya kuyapuuza kichwa kichwa.

Kwa mfano yule dereva aliyepita alikuwa anawafinya abiria wake tena kwa makusudi kabisa na wanapolia vilio vya uchungu yeye ndio anacheka kweri kweri na akiona abiria wanataka kunyamaza hata kama kwa kujikaza kisabuni(kuugulia maumivu moyoni) basi anawafinya tena ili yeye afurahi zaidi.

Dereva asiyejali utu wa abiria wake kuwabamizia bondeni mfe wote ni kugusa tu. Kwangu mimi dereva mwenye utu huyo nampa big blue tick.
 
Fasihi yenyewe mbona kama michambo ya kwenye nyumba za kupanga,, hizi ni taarabu kwenye nyumba za kupanga yani hata mtoto mdogo anajua nani anasemwa,, alafu kuwa na adabu hata kama humpendi mtu usimuatack personal, hayo mambo ya kupaka wanja yanahusiana vipi na kazi! Na ulimuona kipindi anapaka huo uwanja? Au kila kazi anayoifanya we ulitaka auze sura kwenye tv ndo ujue kuwa anafanya kazi! Hizi I'd fake zisikufanye ukakosa adabu.
 
shukrani mkuu, nilichokiandika ni tofauti na ulivyoelewa .Pia ninauchukua ushauri wako
 
Dereva alipewa ushauri akapuuza, baada ya kupata leseni ya kuendesha lile basi ilitakiwa afanye yafuatayo;
~major engine overhaul, ilitakiwa abadilishe kila kitu kuanzia PM, IGP, Ministers na wengine ili apate timu nzuri ya kuendana nayo
~ilitakiwa basi lipigwe rangi nyingine ili kuendena na route aliyoichague
~ kuimarisha usafi wa basi, kuwapa abiria uhuru wa kutoa mawazo yao, na kuwa na lugha nzuri na dereva wenzake na kuruhusu ushirikiano na ushindani na mabasi mengine
~ kuzuia gharama za ovyo za kupandisha nauli, maana tangu apate leseni nauli kila siku inapanda
~atafute vijana wapya, na wenye uwezo wa kumuongoza, achane na hawa wa kila siku akina Mwigulu
~afute kesi kesi ya Mbowe
Angebadili timu nzima kwa mkupuo huoni kwamba watu wangehoji mbona ulisema wewe na yule ni kitu kimoja?. Halafu "ndugu zake" wa dereva aliyepita wangezidisha chuki zaidi kwa huyu dereva mpya?
 
Back
Top Bottom