Dereva gari limemzidi uwezo, Leseni ichunguzwe

Dereva gari limemzidi uwezo, Leseni ichunguzwe

Hili gari wananch walishagoma kulipanda iliyobaki ni kulazimishana tu. Linatembea bila ridhaa yacwananchi. Ninampenda mrithi wa Maalim Seif kule Unguja alisema mpaka kutoa roho za watu kisa utawale utawala maana yake ni nini?
 
Dareva kasema anaongeza gharama za nauli ili apate hela ya kurekebisha gari amesahau wanao mudu hiyo nauli ni watu wachache tu na weng hawaimudu muda si mrefu abiria wanaweza kuisusia gari na kutafuta njia za panya ili wafike waendako huku gari itabak kwenye hali mbaya kutokana na kukosa pesa za uendeshaji, ni Bora nauli ingekua rafiki abiria wangesafiri kwa wingi na yeye aitengeneze gari bila kuwaumiza kiuchumi abiria
 
Dareva kasema anaongeza gharama za nauli ili apate hela ya kurekebisha gari amesahau wanao mudu hiyo nauli ni watu wachache tu na weng hawaimudu muda si mrefu abiria wanaweza kuisusia gari na itabak kwenye hali mbaya kutokana na kukosa pesa za uendeshaji, ni Bora nauli ingekua rafiki abiria wangesafiri kwa wingi na yeye aitengeneze gari bila kuwaumiza kiuchumi abiria
anajua fika kuwa abiria tuliowengi ni masikini ndio tunaopamba magari ya umma hivyo akipandisha nauli analengo la kutuumiza sisi na sio wengine.
 
Eti ,,Alishindwaje kumshauri"?

Ukiwa huna akili tu ndipo utauliza hili swali,,- yaani ikiwa mbongo zako zimelala yoo.
Usiniambie kuwa dereva wa wakati ule alikuwa hashauriki? yule alikuwa mkali si kwamba alikuwa hashauriki na ukali alikuwa nao baada ya kuingia kazini na kuona wasaidizi wake walikuwa wanaendesha mambo kimazoea.Huoni kwa kipindi chake alilitoa gari kutoka Ordinary Class hadi Semi Class na angeleea na udreva basi tungefika kwenye First Class. Udereva ni taasisi ambayo inajumuisha makondakta, turn boys,wakata tiketi, watu wa parcel ,mafundi wa magari na umeme wa magari n.k hao ndio utengeneza neno udereva.
 
Dereva gari limemshindwa kila kukicha ni kumtupia lawama dereva aliyepita eti ubovu huu wa gari ulisababishwa na yeye pamoja na wasaidizi wake amesahau naye alikuwa ni kondokta wa dereva mkuu, alishindwaje kumshauri.Chaajabu anaendesha gari ovyo ovyo bila hata ya umakini hasikilizi abiria ndani yeye yupo busy kusikiliza madereva anaopishana nao barabarani wakimpa HI.

Gari limekuwa bovu taa haziwaki na zikiwaka basi hatuna uhakika wa kuendelea kuwaka kwa muda wote hali inayopelekea abiria kukaa giza, huduma ya maji ya uhakika ndani bus hakuna tena tofauti na dereva aliyepita alikuwa mkali kwa mkuu wa idara ya ugawaji maji.Dereva aliyepita aliacha mradi wa utengenezaji wa betri ambapo alisema kuzimika kwa taa na kutofanya kazi kwa AC ni kukosekana kwa betri N200 na alituacha katika hatua za mwisho za ununuzi ila baada ya huyu dereva mpya kuja hali imekuwa tete anatamani tuendelee kuazima mabetri toka kwa majirani hataki kabisa tujitegemee.

Cha ajabu haka kondakta wake yupo yupo kazi kuvaa kaundi suti tuu na kupaka piko ameshasahu wajibu wake ni kumkumbusha na kumshauri dereva juu ya mwenendo mzima wa gari.Alikuwa machachari kweli kweli alipokuwa turn boy wakati ule alikuwa mbunifu wa mambo lukuki ila siku hizi kawa kama zoba.

Abiria tunasema dereva achunguzwe je ana leseni halali ya kuendesha ili gari au ana leseni Class D halafu tumempa Bus, hii safari ni ya masafa marefu sio kama ye anavyo fikiri safari hii inaenda kuamua hatma ya watoto zetu na wajukuu zetu.

Fasihi ni kazi ya sanaa.
Nimekuwa mwanafasihi
Ulikuwa sahihi sana mkuu
 
Back
Top Bottom