Nimeshangazwa sana na muitikio wa wana CHADEMA baada ya
Juliana Shonza kuhama akitokea Cdm kwenda CCM.
Pro CDM wengi wameishia kumshambulia kwa matusi na kejeli nyingi,bila kutilia maanani kuwa katiba ya JMT inamruhusu raia yeyote kuwa mwanachama wa chama chochote,almradi hajavunja sheria za nchi.
Jambo kubwa ambalo CDM wangejiuliza hapa ni:
1/Juliana Shonza na "Masalia" wengine walipata fursa ya kuelezwa tuhuma zao,kujitetea na kusikilizwa?
2/Kuna ukweli kiasi gani dhidi ya tuhuma za ukanda na ukabila katika chama cha CDM?
3/Kuna ukweli kiasi gani kuhusu tuhuma za ubadhirifu wa rasilimali za chama unao daiwa kufanywa na viongozi wakuu?
Kumbukeni lisemwalo lipo,na mficha maradhi kifo humuumbua!
Ni wakati wa cdm kama chama kujitathmini sasa,na kuondoa uozo na udhaifu wowote kama upo.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.