Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Raia Fulani, Nov 23, 2010.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Tunapokizungumzia Chadema tunazungumzia mambo mawili makuu; Demokrasia na Maendeleo. Ni imani yangu kuwa waasisi wa chama hawakukurupuka katika kutafuta hayo maneno mawili ili yawe mwongozo katika kile viongozi, wanachama na wananchi kwa ujumla wanaanimi. Ni vyema basi kujua kwa muhtasari nini maana ya maneno haya.

  Demokrasia
  Neno Demokrasia linatumika kijamii pamoja na kisiasa. Linatumika katika nyanja nyingi za maisha kama katika kazi, ndoa, dini, elimu, kiuchumi n.k. Ila neon hili linatumika zaidi katika siasa.

  Demokrasia inaweza kutafsiriwa katika misingi yake toka lugha ya Kigiriki. Demos = the people, Kratos = power. Hivyo basi demokrasia ni mfumo wa kiutawala ambapo nguvu ya kisiasa inatoka kwa wananchi. Au ni mfumo wa kisiasa ambampo nguvu za kiutawala zinatoka kwa wananchi.

  Kadhalika demokrasia inaweza kuwa ya moja kwa moja ama ya uwakilishi. Katika mazingira yetu hatuwezi wote wananchi mil 40 kufanya maamuzi kwa niaba na kwa ajili yetu. Hivyo umuhimu wa demokrasia ya uwakilishi ndipo inapohusika. Demokrasia ya uwakilishai ni pale ambapo watu wachache wamechaguliwa ama kuteuliwa kuwakilisha mawazo ya wengi, na kwa usawa na haki katika vyombo vya maamuzi kama serikali, bunge na mahakama.

  Maendeleo
  Umoja wa mataifa kitengo cha maendeleo kinafafanua maendeleo kuwa ni kuwa na maisha marefu nay a afya, kuwa na ufahamu, kuwa na uwezo wa kuzifikia rasilimali zinazohitajika kwa maisha bora na kuweza kushiriki katika maisha ya kijamii kwa ujumla. Kwa lugha nyingine maendeleo ni kuwajengea watu uwezo katika nyanja zote za kimaisha kama siasa, uchumi, kijamii, kiutamaduni ili watu waweze kudhibiti maisha yao, kuelezea mahitaji yao na kutafuta ufumbuzi kwa matatizo yao.

  Demokrasia na Maendeleo ni dhana mbili zinazoelekea kufanana na wakati huo huo kutofautiana. Zinafanana kwa misingi kuwa dhana zote mbili ni hitimisho la maisha bora kwa wananchi husika. Zinatofautiana kwa misingi kuwa kipi kianze na kipi kifuate . wakati mwingine ili pawepo na maendeleo, nguvu ya ziada inabidi kutumika. Tuliona hili katika utekelezaji wa Azimio la Arusha. Tunaona hili kwa wenzetu kama ilivyokuwa kwa Ujerumani, USSR na mataifa mengine. Demokrasia kwa upande wake inataka maridhiano na maamuzi ya wengi ama uwakilishi wa hayo maamuzi, kitu ambacho kinaweza kuchelewesha utekelezaji kisa tu mawazo ya mtu/watu Fulani yaheshimiwe.

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA
  Tunapoangalia katika ngazi ya chama tunaona kuwa Chadema kikiwa na dhana zake mbili kinashindwa aidha kuwa na kauli moja ni dhana gani ifuatwe kwanza, ama mawazo ya nani yapewe kipaumbele. Inawezekana mambo kuwa shwari ndani ya Chadema ila ni media na Dola kutaka kuchafua tu hali ya hewa ya chama. Inawezekana pia kuwa ndani ya chama hali si shwari hivyo kusababisha mivutano ya utekelezaji wa dhana hizo mbili-kwamba nani anatekeleza demokrasia na nani anatekeleza maendeleo.
  Labda tujadili kuanzia hapa. Ndani ya Chadema kuna wanaoamini katika demokrasia na kuna wanaoamini katika maendeleo ila mwisho wa siku wana kauli ya kikasuku ya People's Power! Kuna uwezekano wa kubeba dhana hizi mbili kwa wakati mmoja? Kuna haja ya kuchelewesha moja ili iliyobaki ifanye kazi ili mwisho wa siku lengo litimie? Tuyajadili haya kwa manufaa ya chama chenyewe, pamoja na imani na matumaini ambayo tumeyaweka juu ya chama kwa mustakabali wa maisha bora kwa kila mtanzania


  Yajue pia ya CCM kwa ufupi hapa

  Soma uchambuzi wa wengine hapa
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Wanabodi.

  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)..

  Kimejikita zaidi kwenye vurugu na watanzania sasa wameamini maneno ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dr Slaa..

  Akiapa kwa uchungu kwamba watahakikisha nchi haitawaliki.

  Hata kwenye majimbo ya uchaguzi ambayo Chadema imeshinda aidha ubunge au udiwani, wabunge na madiwani hao walioshinda kwa tiketi ya Chadema..

  Hawafanya lolote chanya la kuwaletea wananchi maendeleo badala yake wanaendesha mivutano isiyoisha wakipinga hata yasiopingika..

  Wabunge wa majimbo ya Kawe (Halima Mdee), Ubungo (John Mnyika). (Tundu Lissu) Singida, (Lema) Arusha (Wenje) Mwanza..

  Hawakai majimboni mwao wala hawana mpango wowote na wapiga kura wao, badala yake wamejikita kuteleza mikakati ya Chadema makao makuu wanazunguka nchi nzima kuhamasisha watanzania wasigane na serikali ili hatimaye nchi isitawalike..

  Huko Mbeya nako moto umewaka lakini kwa staili ile ile ya watu kusigana na serikali pasipo sababu za msingi..

  Mbunge wa Mbeya mjini anaitwa kwa jina la sifa Mr. Sugu, amepewa sifa nyingine ziada inayozidi cheo cha ubunge, anaitwa Rais wa mkoa wa Mbeya, je, huu sio uhaini?

  Upinzani wa Godbless Lema, na Tundu Lissu, Dr Slaa, Freeman Mbowe, haufai na unadhirisha wazi kwamba wahusika hawakupitia darasa la urai..

  Uko wapi uzalendo wa Watanzania wenzetu!
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Huna hadhi ya kuanzisha thread coz hauna mawazo huru bora ubaki kuchangia tu.
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  umesahau kule nyamongo sijui nako ni chadema, kimwagara nae ni chadema
   
 5. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Unachuki binafsi na cdm leta mifano uslete hoja jumla jumla kama nape, mfano mbunge wa ccm jimbo la geita kafanya mambo gani ukilinganisha na wa chadema kawe? ili tuwe huru kuchangia
   
 6. tikatika

  tikatika JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,672
  Likes Received: 2,207
  Trophy Points: 280
  Tatizo sio mwili wako ni akili ambayo ikipenda inakula nyama mbichi! Yaani wewe huoni matatizo ya CCM na serikali yako unaisema CHADEMA! TUME YA MADINI ILIVYOIBUA MADUDU YA SERIKALI YA CCM, YA JAIRO NA RAISI WAKO KUTAKA KUMFICHA KUPITIA LUHANJO HUONI?

  YA KAGODA, EPA, RICHIMOND, KUVUANA MAGAMBA MPAKA BOSS WAKO NAPE ANAKANA KATAKATA HAJAWAHI KUWASEMA MAFISADI KWA MAJINA?

  WAMEMTISHA AKIENDELEA ANAWAFUATA WAFU. MWEEE POLE!!
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mimi nimeanza kuandika Thread humu JF wewe bado uijui JF
   
 8. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Naona leo mpo wengi sana...hata wewe umeanzisha thread....duh!!
  Ndo resolution za kkao cha chama chenu jana??

  kweli nazi haiwezi kuchagua kupikiwa maharage au ubwabwa!
   
 9. m

  mcheshi JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 769
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Kichwa chako kimelemazwa na magamba yaliyo kithiri kwa wizi usio fichika. Unatamani uone kila mtu amekuwa mwizi.

  Unawezaje kumtetea mwenye makosa yanayo onekana wazi na kumshutumu asie na makosa, utakua unatawaliwa na pepo kichwani mwako.

  Mhukumu kwanza mwenye magamba ya makosa kwanza ndio upate uhalali wa kuongea.
   
 10. m

  marembo JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyo ritz ni nanii kwani? Hana hata chembe ya haya. Na wachangiaji wengine humu JF wapimwe akili. Mtu anajitoa kimasomaso kueleza pumba akidhani anachangia. Si bure wanasema msafara wa mamba hata kenge wanajificha humo humo.

  Huyu hana chochote chanya kwa CDM ila wana fujo nchi haitawaliki. Kama huna cha kuchangia chapa lapa waaachie watu wafanye mijadala ya maana. Hao uliowataja wote wana contributions nyingi tu katika majimbo/kata zao tangu wapewe fursa hiyo na wananachi.

  Afanye utafiti kabla ya kufoka. Kama unafuatilia mijadala hata bungeni unbajua ni chama kipi kina vichwa au la. Wabunge wa CDM walivyotoka nje ya Bunge waliobaki kule ndani walikuwa wanajadili mswada au wanajadili watu (Lissu) na Chama? S

  i bure CCM imesahau elimu kwa watu wake kwa hiyo sishangai hata ule uwiano kuwa mbunge mmoja wa CDM ni zaidi ya wabunge 20 wa CCM.
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  umesahau kule nyamongo sijui nako ni chadema, kimwagara nae ni chadema
   
 12. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  mbona mnauza utu wenu kwa bei ndogo hivyo? angalia impact yake miaka 100 ijayo siku kesho kutwa.
   
 13. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  Masaburi at work
   
 14. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  tatizo sio kuandika
  je?unaandika kitu gani?
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Katika nukta hii nawataka wana Chadema wa Arusha Mjini, Mbeya Mjini, Ubungo na Singida Mashariki wayaangalie majimbo ya Hai, Moshi Vijijini na Kigoma Kaskazini..

  Kwa kina Zitto Kabwe, Philemon Ndesamburo, na Freeman Mbowe watagundua tofauti na hila zilizoko ndani ya chama hicho..

  Katu Mchagga hawezi kuitifua barabara ya Kilimanjaro, wala kuchoma jengo wala kuacha shughuli za kuzalisha mali akashiriki maandamano..

  Ndio maana maeneo yao yametulia. Tukiangalia fujo za Mbeya tunaona wazi kwamba ziliandaliwa..

  Na uharibifu mkubwa ulipangwa na kuratibiwa kwa umakini na Chadema
   
 16. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Huyu RITZ anafikili kutangulia kuwepo ndo kujua au ndo wingi wa hoja, unaweza kutanguliwa kama tai wakati umeningia tu.
  Nilikwenda Ban kwa sababu zako mkuu nipo radhi kurudi tena bani.
  Ungekuwa na hoja bado unaangaika na JF Senior Expert Member

  Vita vikianaza wewe ni halali yangu
   
 17. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Kwako nchi kutawalika ni wakuu wa mihimili ya Dola yaani Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Spika wa Bunge Mhe Anna Makinda wanaposhirika kutafuna fedha zilizochangishwa kiharamua na Ndg David Jairo, ambapo hata Kamati ateule ya Bunge imebaini zilichangishwa kiharamu na matumizi yake yalikuwa haramu? Wakuu hao kila mmoja alifafuna Shilingi 280,000/= (Laki Mabili na Themanini tu) kwa kama posho ya kikao cha dakika 40 tu ilihali wakilipwa mishahara, na posho za kujikimu kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya bunge Dodoma. Source Mwanahalisi na Raiamwema
   
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Chadema haijali kwamba Arusha ni mali ya wakazi wa Arusha, badala yake wanataka wawakillishi wa wananchi Arusha (Madiwani) wawe mateka wa kuteleza kila kisemwacho na makao makuu yaliopo Kinondoni mtaa wa ufipa Dar es salaam
   
 19. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Huna andika nini humu.kila siku hupo
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Wenzetu Chadema mmedhamiria vilivyo kuhakikisha nchi haitawaliki na Rais hamalizi salama kipindi cha pili
   
Loading...