Habib Mchange kwanini kwenye kila andiko lako lazima umhusishe Zito Zuberi kabwe? Kwa nini kila unapotaka kupumua unataka kumfarakanisha ZZK na Chadema kwa kisingizio cha kumtetea. Sidhani wala siamini kama ZZK anakutuma.
Kwa nini usijitetee wewe mwenye au usiwe huru kuandika bila mtu mwingine kumwingiza kwenye vita vyako??
maandishi na tuhuma zako zinaonyesha hasira ya wazi dhidi ya wafuasi na wanachama pamoja na viongozi wa Chadema. Ila lazima ujue wazi dhambi ya rushwa na makundi uliyoitenda ndiyo inakusakama na kukuumiza roho. ungekuwa mwanasiasa mahiri ungeliona kosa na kutubu dhambi na kuanza kutenda mema.
Sidhani hata huyo ZZK anakuhitaji kwa sasa. Siasa huwezi ukawa na permanent adui wala permanent rafiki. Ndiyo siasa kaka. Uongozi huwezi kuongoza unaowataka tu au kuwapenda,huwezi kufanya kazi na marafiki zako kama ni hivyo ingekuwa rahisi.
Kwa jinsi unavyoutafsiri uongozi huwezi kuwa hata kiongozi kwenye kikundi cha watu kumi na ikiwa hivyo itakuwa Tsunami.
Uongozi ni art, kipaji, hekima, busara, utulivu, ushauri, akili, weledi, uvumilivu , uwezo nk ambavyo vyote huna. Kwanza nataka uje hapa JF na real ID ili watu wenye weledi wakujue sio unatuvurugia chama ukifikiri unamsaidia mtu.
Farakani alipojua kila akiongea wazungu wanampunguzia kura obama alisema maneno yenye busara sana; kwa manufaa mapana ya ushindi wa Obama kwenye historia ya marekani nitakaa kimya ili kijana wetu ashinde.
Kama kweli wewe ni mpiga debe wa ZZK unamharibia vibaya sana kuliko kumsaidia kwenye gwaride la ushindi wa kisiasa kaa kimya. Kwa sasa wewe ni mchafuzi
Hivi kundi lako likishinda uenyekiti wa CDM mnafikiri mtafanya kazi na nani? Mnawanachama kutoka mwezini ambao mtaona ndio wanaofaa??
Kwanini mchukie uongozi wa sasa wakati upo kikatiba?
Mnafikiri mkiingia madarakani huku mmejenga makundi sijui ya hawa wazee wale vijana mnafikiri ninyi mnakuwa kwa kwenda chini au umri unaongezeka? je unajua kwa umri wako wako madogo wanakuita mzee au kwa umri wa huyo unayempenda wako madogo tayari wanamwita mzee au mnafikiri uzee lazima uwe na miaka 60??
Na je akipendwa kijana mwingine mdogo na mwenye hekima kuliko kundi unalosarandia si utakuwa sakala??
Sio wote wanaouwezo wa kuwa viongozi hasa vyeo vya juu, wengi wanaweza kuwa watendaji, watu wa kutumwa na wachache viongozi kwani kiongozi anahitaji ngozi ngumu sio laini kama hizi ninazoziona.
Chadema itaendelea kuwepo kwa umakini wake na uchambuzi wake mahiri hasa kwenye kupata uongozi wake.