Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA

Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA

ikiwa ni mwaka wa pili sasa baada ya slaa kushindwa kuingia ikulu katika uchaguzi mkuu uliopita, mbinu mpya aliyokuja nayo ni kutoa matamko yanayowatia hofu wananchi juu ya hali ya usalama wa maisha yao na mali zao...hawezi kutoa tamko kuwambia watanzania jinsi walivyojipanga kutengeneza ajira kwa vijana na kuonyesha njia jinsi watakavyojenga uchumi bora.
sl

slaa hkushindwa, bali alifanya kile alichotumwa na ccm. Ukweli kuwa slaa hakushindwa uchaguzi upo kwa tume ya uchaguzi, ambao hadi sasa hawatangaza matokeo kwenye web yao.

Nasema slaa alitumwa na ccm kufanya shughuli hiyo, kwani ni moja kati ya usalama wa taifa ambao si usalama wa taifa, bali ni usalama wa ccm. Slaa alisema hataki kupinga matokeo eti kuepuka kumwaga damu. Kwani mpaka kieleweke maana yake nini?

Slaa ni kati ya wanaohakikisha ccm kutawala, japokuwa kila siku amekuwa ni mtu wa matamuko.
 
Wanabodi. Pamoja na CHADEMA kufanya ziara katika baadhi ya mikoa ya Tanzania na kutangaza kauli mbiu ya M4C Watanzania wanahoji kwa nini CHADEMA hawasemi wana mipango gani yenye tija kwa taifa letu na watawakomboa vipi kama wanavyojinadi kuwa wao ni wakombozi? Moja ya kauli ya viongozi wa CHADEMA ni ile hakuna kulala mpaka kieleweke pamoja na ile tunataka kuwakomboa Watanzania, hawaelezi mambo yanayohusu maendeleo ya taifa lao. Watanzania wanataka CHADEMA wangekuwa wanawaeleza Watanzania ni kipi watafanya wao ambacho CCM kimeshidwa kuwafanyia, waseme ni barabara zipi ambazo watazijenga na waeleze vyanzo Vya fedha watakazotumia kujenga barabara hizo. Kwenye mikutano ya CHADEMA huwezi kusikia wanaelezea Watanzania kuwa watawajengea hospital au watafanyaje katika kuboresha elimu hiki ndio kipindi cha kuwafafanulia Watanzania juu ya utekelezaji wa sera yao waliyosema wakati wa kampeni 2010 kuwa CHADEMA watatoa elimu bure chekechea hadi chuo kikuu kwa fedha kutoka wapi na kwa uchumi upi wa nchi. Wananchi wanasema wanaofika kwenye mikutano ya CHADEMA wanachokisikia kutoka kwa viongozi wa CHADEMAa kauli mbiu zao 'Mpaka kielekewe hakuna kulala' 'Ukombozi unakaribia' Wao wana pesa siye tu Mungu' Nchi haiwezi kuongozwa mithiri ya kampuni ya biashara au familia ya watu wa damu moja.
magamba wamezoea kutoa sauti kwa niaba ya watanzania; Mhhh! Wewe Ritz umekuwa msemaji wa watanzania tangu lini?? Hayo ni mawazo yako binafsi. Mtanzania mwenye akili timamu hahitaji elimu ya chuo kikuu kujua kuwa hii nchi inahitaji UKOMBOZI wa kweli.
 
​@ritz, Kimbunga

1.Kujenga nchi isiyo na ufisadi
2.Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
3.Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
4.Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
5.Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
6. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
7. Kutoa huduma bora za afya bure
8. kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
9. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
10. Kubana matuzi Ikula (Yuko tayari kula mihogo
)

Mungi...​hizi nyingi siyo sera ni maamuzi na malengo...sasa wanahitaji sera za kuyafanikisha haya. 1-3 ni malengo, 4,5,6,9,10 ni maamuzi tarajiwa. 7 pekee naweza kusema ni sera.
 
Jamani mimi sioni tatizo. kweli hawa CDM kwa upande wanafanya vizuri lakini si mara zote.
Hili la kueleza mipango mikakati nikweli lazima kwenye mikutano yao waeleze.

Mimi ningeshauri kama kweli ni wakombozi wachukue japo kijiji kimoja tu hapa tanzania kiwe cha mfano.
Watoe maendeleo tuone. Kunawabinge wapo wa chadema je wamefanya nn kwenye majimbo yao?

Mimi sipendi kuongea ongea tu nataka vitendo kama unasema wewe una MUNGU nani hapa Duniani asie na MUNGU. acheni bwana kutetea ubovu hawa chadema hata ukiwapa nchi wataboronga sana tena zaidi ya CCM. Tambua kua CCM nichama kilichokomaa. Chadema bado wachanga.

Kumbe unajua dhahiri kwamba CCM wameboronga,sasa unataka waboronge mpaka lini?na ni kigezo gani umetumia kuwapima CHADEMA kuwa wataboronga wkt hujawapa dola?
 
Hakuna ubishi Chadema kama jina lake lilivyo ni chama cha Demokrasia kimefanikiwa kueneza Demokrasia kwa kutumia mikakati iliyozaa matunda kama Operation Sangara, M4C, mikutano, midahalo kwa ushiriki wa makada wake kikamilifu kueneza chama na kuwasemea wananchi.

Ni wakati muafaka kwa chama kama jina lake lilivyo kujihusisha au kuwa mstari wa mbele kwa shughuli za kuwaletea maendeleo, "Chama cha Demokrasia na MAENDELEO.

Utasema hakijashika dola kwani mtu binafsi anaendelea kwa kushika dola si zaidi sana taasisi kuleta maendeleo.
Wafanye yafuatayo kuleta maendeleo:-

1. Wabunge watumie mfuko wa jimbo kuwapatia wananchi maendeleo katika majimbo yao isisike matumizi kama ya fedha za serikali za maendeleo kuliwa.
Watambue kero za kila mtaa, kata, tarafa na kuona ni kwa jinsi gani mfuko huo unaweza kuwakutanisha wananchi na wadau wa maendeleo kufanya hata harambee ya kuchangia maendeleo kwenye mtaa, kata zenye kero.
2. Mikutano na viongozi wa mitaa na kata wa chadema kufanya serikali imeshindwa makufanya
 
Maendeleo au mipango ya maendeleo hupangwa na serikali iliyoko madarakani. Kama serikali ya Kikwete imeshindwa kuleta maendeleo si jukumu la Chadema kujaza nafasi hiyo. Kazi ya Chadema ni kuonyesha udhaifu wa serikali ya CCM na kuwapa raia matumaini kuwa we can and we will do better. Hatuwezi kuanzisha mipango ya maendeleo na kuwaachia mafisadi wakiendelea kushikilia usukani wa dola.
 
Hakuna ubishi Chadema kama jina lake lilivyo ni chama cha Demokrasia kimefanikiwa kueneza Demokrasia kwa kutumia mikakati iliyozaa matunda kama Operation Sangara, M4C, mikutano, midahalo kwa ushiriki wa makada wake kikamilifu kueneza chama na kuwasemea wananchi.
Ni wakati muafaka kwa chama kama jina lake lilivyo kujihusisha au kuwa mstari wa mbele kwa shughuli za kuwaletea maendeleo, "Chama cha Demokrasia na MAENDELEO.
Utasema hakijashika dola kwani mtu binafsi anaendelea kwa kushika dola si zaidi sana taasisi kuleta maendeleo.
Wafanye yafuatayo kuleta maendeleo:->
1. Wabunge watumie mfuko wa jimbo kuwapatia wananchi maendeleo katika majimbo yao isisike matumizi kama ya fedha za serikali za maendeleo kuliwa.
Watambue kero za kila mtaa, kata, tarafa na kuona ni kwa jinsi gani mfuko huo unaweza kuwakutanisha wananchi na wadau wa maendeleo kufanya hata harambee ya kuchangia maendeleo kwenye mtaa, kata zenye kero.
2. Mikutano na viongozi wa mitaa na kata wa chadema kufanya serikali imeshindwa makufanya

Wameacha kufanya shughuli halali za chama cha siasa na badala yake wamejikita kuhamasisha maandamano,.
 
Wana JF,
Naomba leo tugeukie kwenye uhalisia wa demokrasia ndani ya vyama vyetu hasa vya upinzani hasa katika nyakati za chaguzi na mfumo mzima wa kubadilishana uongozi ndani ya chama.
Kwa tanzania nitapenda kutumia mfano maalumu(case study) toka chama kikuu na chenye nguvu kubwa ya ushawishi kwa wananchi CHADEMA.
Pia nitaomba kuoanisha demokrasia halisi ya CHADEMA na chama cha upinzani cha nchi jirani tena rafiki ya UGANDA ambayo kimsingi watu wake,level ya siasa na uwezo kiuchumi tunakaribiana sawa.
Wana Jf,CHADEMA ni chama kikuu cha upinzani nchini na kwamaana hiyo tunategemea kuwa kinatakiwa kutekeleza demokrasia kama chama chenyewe kinavyojipambanua kuwa nicha kidemokrasia .
Lakini kila mmoja wetu anaweza kukili wazi kwamba hiki chama si chakidemokrasia ni chama chenye jina linaloitwa demokrasia.
Kwa yeyote anayefuatilia siasa za ndani na nje ya nchi atakili wazi kwamba Forum for Democratic Change-FDC nchini UGANDA ni chama kikuu na chenye nguvu kubwa sana ya ushawishi kwa wananchi hasa baada ya kiongozi wake Kiiza Besigye kuonekana kuwa msumari wa moto kwenye serikali ya mseveni.
CHAMA HIKI CHA FDC NI SAWA NA CHADEMA KWA TANZANIA utofauti wake ni katika uelewa na utekelezaji wa demokrasia ndani ya chama.
Naanza kwa kuonesha huyu kiongozi mkuu wa chama cha FDC
DR.KIIZA BESIGYE mara kadhaa ameonekana akikamatwa,akiandamana na watu kupinga udhalimu wa serikali ya mseveni,Kiiza ameonekana akivunjwa mikono na hata kufungiwa asitoke kwake anakoishi kwa sababu amekuwa na upinzani mkali sana kwa serikali ya MSEVENI.
Bila shaka Dr.slaa au Mbowe wanakaribia kwa kiasi kidogo sana kwa uwezo wa kiongozi huyu kushawishi wananchi,anashawishi kwa sababu anauwezo wa kujenga hoja,pia hana hoja moja tu ya kuiinanga serikali ya mseveni.

LAKINI HIVI MAJUZI DR.KIIZA BESIGYE ametangaza kuachia ngazi mapema kama kiongozi wa chama cha Forum for Democratic Change.
Dr Besigye alisema anataka kujiunga na harakati pana zaidi za kijamii zinazoipa changamoto serikali ya Rais Yoweri Museveni.Amepuuzilia mbali pendekezo kuwa kuondoka kwake kutauacha upinzani bila uongozi thabit.
0,,15033269_4,00.jpg

Kiongozi wa FDC Kizza Besigye

Hatua aliyoifikia Kiiza Besigye si kwamba tu ni uanasiasa bora bali ameonesha kuwa Uongozi sio mali,Uongozi sio familia,Uongozi sio kiti cha milele.
Dr.Kiiza Besigye leo hii angekuwa(just imagine) ndiye kiongozi wa CHADEMA hapa Tanzania na kwanamna alivyofanya ushawishi mkubwa kama ule pale uganda,Kwa namna alivyokuwa bega kwa bega na wanau ganda kumtikisa Mseveni,WATANZANIA WENGI TUNGEISHIA KUSEMA AAAAAH HUYO KIIZA BESIGYE NI CCM,Ooooh Huyo Kiiza ni MAMLUKI,Oooooooh Huyu Kiiza Besigye amekula hela za Kikwete.Oooooh Huyo Kiiza Besigye ni shushu anatakiwa achomwe moto n.k yaani maneno mengi mbofu mbofu yangekuwa juu yake.
Hii inatufundisha nini,Ni kwamba watanzania tuliwengi tunaendeshwa na (emotion)yaani hatuna uvumilivu,wavivu wa kuchambua mambo.Wepesi sana wa kutaka mema haraka kuliko kutoa jasho.

BAADA YA BESIGYE KUACHIA NGAZI DEMOKRASIA ILICHUKUA MKONDO WAKE


Wajumbe wa Chama cha Siasa cha Upinzani nchini Uganda cha Forum for Democratic Change (FDC) wakiwa wanapiga kura kumchagua rais mpya wa chama hicho atakayechukua nafasi ya Dkt. Kiiza Besigye.
TOFAUTI NA CHADEMA chama kinachofanya CHAGUZI zake kinyemela na kwa so called nepotism zaidi
NDANI YA FDC(FORUM FOR DEMOCRATIC CHANGE) KUNA TUME HALALI YA UCHAGUZI WA NDANI YA CHAMA(electoral commision) Tume ya uchaguzi ni halali,Huru na yaina mgusano na kiongozi yeyote aliyopo ndnai ya chama.Ni tume ya watu makini waliopo nje ya Chain of command ya chama).Hawa wanasimamia haki na usawa kwenye uchaguzi bila upendeleo,Hii tume inafanya kazi zake kwa misingi ya sheria za uchaguzi za kichama.
WAKATI CHADEMA swala la uchaguzi wa ndani ya chama tena wa kitaifa lipo chini ya katibu mkuu wa chaama(DR.SLAA) yaani mgombea yeyote unachukua fomu ya uchaguzi kwa Dr.slaa ndipo ugombee.
KIMSINGI haiingii akilini kabisa KATIBU mkuu naye akiwa anagombea uenyekiti wa chama au nafasi yoyote ndani ya chama itakuwaje?YEYE MWENYEWE NI MSIMAMIZI WA UCHAGUZI,YEYE MWENYEWE NI MGOMBEA WA NGAZI YA UONGOZI NDANI YA CHAMA???KUNA DEMOKRASIA HAPA AU MAIGIZO?
Pili kwa namna hivi CHADEMA kulivyokuwa na makundi,mpasuko wa uongozi unadhani DR.SLAA yeye ndiye mzimamizi wa uchaguzi nini kitatokea kwanye kupitisha na kuhesabu kura za wagombea ambao hawashabihiani naye kimawazo na kimuono??
KWA HIYO CHADEMA SI CHAMA CHA KIDEMOKRASIA kama kinavyojipambanua bali ni chama kinachojifunika mwavuli wa neno demokrasia huku kikitenda kile kitu kinaitwa NAZISIM(A SOCIALIST PARTY KILICHOKUWA KINATEKELEZA U-DECTETASHIP chini ya adolf Hitler).
WE POLITICIAN WE ARGUE THAT DEMOCRACY IS A GAME IN TOWN,WE CAN HAVE DEMOCRACY WITHOUT ELECTION BUT NOT ELECTION WITHOUT DEMOCRACY.
Hatakama Africa hatuna demokrasia ya KWELI lakini katika mambo ya wazi na yakufedhehesha chama kama haya ni lazima CHADEMA iangalie muundo wake wa mfumo wa uchaguzi.
WANAJF nimetumia CHADEMA kama mfano kwa sababu ndicho chama kkuu cha upinzani nchini,Na FDC ndio kikuu kwa huko UGANDA.
Nawasilisha:
Ndimi Tuntemeke Mwenekilunga
 
sijawahi kukutana na kitu cha maana kutoka kwenye postings za TUNTEMEKE toka niwe mwana chama wa jf. kwanza unaharibu jina la babaangu mkubwa kwani yeye hajawahi kutumika so cheaply like that. He was a true Great thinker and never let us down in any way.R.IP in peace Tuntemenke originanal.
 
Tuntemeke..! Wakati mwingine amini kukaa kimya huficha ujinga uliomjaa mtu.
Unaifahamu historia ya TANU-CCM ya Nyerere?
Mbona kama ni u analyst still uko mweupe sana, maana si kweli CDM hakitambui nafasi na haki za wanachama wake
Bt kutoa kwako povu kuna sababu ya msingi
By the way
Kumbuka kisa cha mzee Malecela pale Chimwaga 2005
 
sijawahi kukutana na kitu cha maana kutoka kwenye postings za TUNTEMEKE toka niwe mwana chama wa jf. kwanza unaharibu jina la babaangu mkubwa kwani yeye hajawahi kutumika so cheaply like that. He was a true Great thinker and never let us down in any way.R.IP in peace Tuntemenke originanal.
Taabu kweli kweli yaani wewe hili jambo la kuangalia mfumo wa uchaguzi ndani ya chama si la msingi?Tafadhali tunapojadili mambo serious kama haya weka uanzi pembeni,jadili kilichopo na kama hakikuhusu kaa pembeni
 
mleta mada umekuja na hoja nzuri tena yenye nguvu ila unachotaka CHADEMA wafanye ni kucopy na kupaste kutoka FDC, je swala la kuchukua form kwa katibu mkuu Dr. Slaa lina tatizo gani? Wakati kura ndizo zitakazo amua na wala sio form uliochukua kwa katibu.

Vilevile ujue hapo CHADEMA ilipofikia katika demokrasia ni kwa ubunifu wake mwenyewe na wanachama wake,ni lini ulimfuata kiongozi wa CHADEMA na kumueleza haya yote,je unafikiri wataota usiku ili wayajue haya? Wanahitajika watu kama nyie wakutoa ushauri ili kukuza demokrasi iwe rahish,kwa jinsi ulivyo yaandika haya ni kana kwamba viongozi wa CHADEMA wanajua kila kitu,it will never happen wakajua each and everything within politics and leadership they also need an extra help from you and me.
Usipende kutupa lawama peleka mawazo yako kwao,wanasema wao ni viongozi makini basi ushauri wako utakua considered!
 
Amegilizia makala ya johnson mbwambo ya raia mwema toleo liliopita, hana hoja zaidi ya unafiki, je lipumba alishandana vipi kuupata uenyekiti wa CUF , majungu yatawamaliza baadhi ya vijana wa kitanzania ambao wamenyimwa fursa za kuwa wezi na mafisadi.
 
Ungewafundisha magamba hili kwani ndo nafasi zao wanazogombea anajitokeza mwenyekiti ama makamu anapambana na kivuli.POOR YOU Tuntemeke.
 
Hili genge la wakina Mchange, Mtela na Juliana Shonza ipo siku litapukutika kama manyoya ya mwewe na si tupo tunasubiria mwisho wao kwani baada ya kushindwa chaguzi ndani ya chama wameamua kuja na style yao hii ya kutumia fake ID jF but wajue sisi tunawajua ila wao hawajijui and why viongozi wa chama kuwafumbia macho hawa wavuta bangi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu samahani,ukiona una maada ambayo unataka kuileta hapa lakini wewe mwenyewe huna uhakika hakika kama imekaa vema, nashauri jaribu kumwomba hata rafiki yako aliyejirani akusaidie kuiweka vizuri ionekane imetoka kwa mtu anayefikiri, kuliko kama hivi ulivyofanya. Ni wazi hii mada umeiweka hapa kwa kukurupuka tu. Please do not expose your bottom.
 
mbugabire Mkuu umetoa maoni mazuri lakini niseme tu labda kama hujui kilichoko nyuma ya TUNTEMEKE, prejudice being out of spite he has a mission which was once known only to him but now he is as naked as nothing, busara unazomshauri anazo sana ila zinakinzana na malengo yake
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom