Tuntemeke ana hoja, na haigusi Chadema pekee bali NCCR, CUF, na CCM; Vinginevyo tafiti nyingi sana (hata uki google) zinaonyesha kwamba, moja ya changamoto kubwa sana ya vyama vya siasa barani afrika ni weaknesses kwenye internal democracy; Hili lipo Chadema, CUF, CCM, NCCR, na orodha inaendelea...;
what is internal democracy?? Swala sidhani kama ni hilo nafikiri swala labda liwe katiba za vyama. Na kama sababu ni hiyo leteni vyama vya siasa duniani na katiba zake zenye demokrasia amabayo wewe na Tuntemeke mnataka CDM iwe nayo ndio muipende.
Swala la mtu kuacha kazi au kukimbia cheo lisiwe kigezo hapa. Tuanze na katiba inayopigiwa mayowe na huyu Tuntemeke mgombea wa kibaha. ni wapi katiba ya CDM inatakiwa irekebishwe ili nyote muipende. Kwa vyama vya siasa nchini ambavyo vimefanikiwa kuifuata katiba yake bila matatizo na kuwa na chaguzi na kubadili viongozi bila mikwaruzo kwa kipindi cha miaka zaidi ya ishirini ni CDM.
Ila changamoto zinakaribishwa na katiba inaweza badilika kama kuna sababu za msingi. Na kila mara katiba inafanyiwa marekebisho.
Mchambuzi, usije jikuta unaingia kwenye train lisilo na dereva, Ukumbuke CDM inakuwa mpaka hapo unapoandika kuna sehemu ya nchi tunahitaji watu wa kugombea vyeo mbali mbali ndani ya chama. Tukikamilisha kukisambaza chama kwa kila raia na kila kona ya nchi utaona CDM yenye furaha kubwa. Kwa sasa tunajua wapo watu wanaolipwa na Nape wakiongozwa na CCM ili kuimaliza CDM. Ila wajue CDM sio mtu mmoja mmoja ni taasisi na wananchi wenye maisha magumu na maonevu ya watawala wa seriali ya CCM.
Tuntemeke alikamatwa akitoa rushwa kwenye chaguzi za ndani za chama, sasa wewe mchambuzi ulitaka katiba ya chadema isemeje ili imfae mtoa rushwa?? Ni wazi huyu anafaa CCM sana ndiko kimbilio la watoa rushwa, wezi, wahujumu, wazembe, walafi, mafisadi, wauaji, na wote wanaoitakia kifo Tanzania ya leo.
Hatuwezi kubadili katiba kwa ajili ya kundi hilo bali kwa ajili ya nia njema na maisha bora ya demokrasia ya watanzania wote.
Demokrasia ni makubaliano ya jinsi ya kuendesha mambo yanayokubaliwa na wengi kwenye jumuiya husika. Kama tukiona wengi hawapendi demokrasia tuliyonayo na lazima wale wanaoiishi yaani wanachama wa chadema na wote wenye mapenzi mema itafanyiwa kazi.
Mamluki hawawezi kuwa ndio wanaolilia vyeo kwa manufaa yao.Rushwa haikubaliki ndani ya CDM. Hata mtumie njia gani 2015 hakuna huruma wananchi tumechoka magamba jipangeni kwa miaka mingine. this is our time, and that time is today.