Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Mh. Zitto Kabwe,
Kwa heshima na taadhima naomba nikuzungumze pamoja na wasifu wako.
Ni wasifu gani alionao Zitto Kabwe?
Kijana, Msomi, Mwanaharakati, Mwanasiasa, Mwanataaluma, na kadhalika.
Lakini tunapokaa na Zitto Kabwe ambaye bado ni kijana mbichi kisiasa na kiumri, tunampokea kwa namna gani na tunashabihiana naye kwa mantiki ipi?
Je Zitto huyu ambaye yu nasi humu JF, tunamuelewa? Je anaeleweka kwetu na kwa jamii ya Watanzania?
Kwangu mimi, Zitto ni kijana, msomi na mtaaluma kuliko mwanasiasa. Bado yupo katika nafasi ya kutambaa kama mtoto anavyotambaa!
Je kauli zake zinaeleweka au kuaminika? Majibu ni ndiyo na hapana. Ndiyo kwa maana huongea bila kufikiria Kisiasa na Hapana kwa kuwa majibu na kauli zake huleta mgongano wa hisia au kiitikadi na hivyo kufanya wasifu na taswira ya Zitto isieleweke.
Nimewahi kukutana na Zitto na tukapiga soga kwa saa moja, tukiongelea mambo mbali mbali. Zitto huyu hana tofauti na mimi nilivyokuwa miaka 7-10 iliyopita katika utashi wa mambo ya kisiasa.
Tofauti yetu, Zitto ni Mtaaluma (academic, intellectual) mno wakati mimi ni mbangaizaji wa mtaani nikiangalia kilichopo na kukipima kisiasa. Wakati Zitto ni Centrist, mimi ni Radical, hivyo utaona tofauti zetu hata kama tunaweza simamia kitu kimoja na upande mmoja.
Je inawezekana kushindwa kwetu kumuelewa Zitto kunatokana na uchanga wake na kushindwa kwake kujitambulisha kama Mtaaluma au Mwanasiasa?
Yes Zitto can be Naive, sound Arrogant and very Self assured. It is a blessing and a curse in the environment of Watanzania today.
Je ana msimamo imara na thabiti? majibu nayo yanakuja ni Ndiyo na Hapana, ikitegemea na upande ulioegemea wewe unayempim na kumsikiliza na utashi wako.
Kwangu mimi, Zitto tunamt\wisha mzigo na msalaba mzito kabla ya wakati wake. Ana nafasi kubwa ya kujifunza kutoka kwetu na sisi kujifunza kutoka kwake.
Zitto ana uwezo mkubwa akishaweza jitengeneza na kuwa na taswira moja ambayo tutaikubali na kumuelewa kuwa kiongozi mkubwa na mwenye mvuto mkubwa mno. Lakini taswira hii ni lazima iwe yake mwenyewe na si kwa matakwa yetu. Ni sisi ambao itnabidi tumkubali na taswira yake pindi itakapopevuka na sisi kuiva na kumkumbatia.
Wengi wetu hapa JF na katika jumuiya za Watanzania tunaotaka mabadiliko, tunatafuta Radical na si Centrist katika mazingira tuliyonayo sasa hivi na ndio maana sishangai jinsi Zitto anavyobanwa humu ndani na kusulubiwa kila siku.
Kadri anavyokua na kukomaa na sisi kushabihiana naye, ndivyo tunaweza kuungana na kuelewana.
Lakini, bado kuna mambo ambayo Zitto itabidi ayaweke sawa kwanza machoni mwa Watanzania wote aeleweke si kwa wachache tuu bali kwa wote kwa kuwa tayari watu wameshaanza kumtarajia awe kiongozi makini.
Mambo haya ni Uchaguzi Mkuu wa Chadema 2009, Kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Rais ya Bomani na kauli zake kuhusiana na Dowans na IPTL.
Gharama za kuwa mwanasiasa ni kuwekwa kwenye kiti moto, usailiwe na wapiga kura.
Je Zitto anaweza kujijenga na kueleweka ndani ya jamii ya Watanzania na hata kadiri anavyopevuka tunaweza kumkumbatia na kumwamini anaweza kutuongoza akiwa ni mtu mwenye siasa za mrengo wa kati?
Mh. Zitto, napenda kuwasilisha salamu zangu,
Nduguyo, Mchungaji!