Defining, Refining and Understanding Zitto Kabwe

Kishoka, Mkandara,

..hii hoja hata mimi imeanza kunichefua.

..huu mchezo anaoufanya Zitto wa kutumia jina lake na nickname Omarilyas ni utoto wa kupindukia.

..kitu kimoja nimejifunza ni kwamba Zitto/Omarilyas anahitaji muda akue.

Mkuu m,bona hao ni watu wawili tofauti na majina yao ni halisi?

Unataka picha zao(kidding)?
 
Waberoya,

..kwa hapa ilipofikia nahitaji Administrators privilleges ku-sort out suala hili.
 
Binafsi naona zito kama mwanaharakati yuko sawa kabisa, ni kijana wa kuigwa na vijana wengi wa kitanzania tunataka mtu anayejiamini na anayesimamia hoja yake mpaka mwisho kama mwanasiasa huwezi kuwa well defined, kila mtu anamjudge kutokana na msimamo wako na ueleo wako. Zito anatoa constructive criticism kwenye bunge ambazo ni za kisomi sio hadithi tu kama wabunge walio wengine ambao wamepitwa na wakati.
 

Nadhani ushauri mzuri, Omarlyas unamweka kwenye wakati mgumu Zitto.



HAwa akina MWAFRIKA, Solomon, Julius wanatoa challenge tu na ni nzuri kuwa nazo katika maisha , Challenge zinakomaza na zina kuza, zinakupa mwanga wa kuangalia many dimensions.In other words na wewe unatoa same challenge kwao, ila zisiwe harsh

Wanapotoa mawazo wanasema kama wao, wewe nawe unapojibu jib u kama wewe Zitto asiwemo.

Zitto atabaki kuwa great leader of his time, na ndio maana kaanzishiwa thread, mimi nikianzishiwa thread humu, ni baada ya kufanya kituko ambacho ni unique sana! labda ugoni(God forbid)! tehe, tehe, tehe
 
Waberoya,

..kwa hapa ilipofikia nahitaji Administrators privilleges ku-sort out suala hili.

wako so close kiasi cha kuwa huwezi kutofautisha, Omar anakosea kwa kumwaga kila kitu humu, kiasi cha ww kuchanganyikiwa.

Omar ana hasira sana, akija kupewa uwaziri mkuu, lazima ataleta za Sokoine
 

Jokakuu,

Zitto na Omarilyas ni watu wawili tofauti. Wote wanatumia majina yao halisi. Omarilyas alikuwa anatumia nick ya Tanzanianjema zamani ila akaamua kubadili na kutumia jina lake la kweli ambalo ni Omar Ilyasi.

Omar na Zitto wote wamesoma mlimani na ni marafiki wakubwa sana. Kama wanajua pw za kila mmoja na kuzitumia hapa, hilo siwezi kujua na sina hata chembe ya uthibitisho. Wakati mwingine inakuwa too convenient kwa Omar kuingia hapa kila mara zitto anapobwana. Je ni zitto anaingia kwa jina la Omar? Sina jibu katika hili ingawa ukweli ni kuwa Zitto na Omar ni watu walioko karibu sana na unaweza kudhani kuwa wanafikiri sawa.

Tofauti ya Zitto na Omar ni kwamba, Zitto ni mbunge lakini pia ni mpinzani wa ccm kisiasa (ni mwanachadema) ila Omar hajui kama awe mpinzani au awe mwanaccm.

Omar hana cha kupoteza baada ya kujitoa kwenye staff ya Zitto kiaina kwa hiyo hana ukaribu wowote na chadema na hajali kitakachotokea huko chadema. Mara nyingi nimekuwa namuuliza kama anachoandika ni mawazo yake binafsi au ni ya Zitto lakini amekuwa hasemi.

Wanaomfahamu Omar kama mimi, wanajua anachotaka - anataka kula pande zote mbili (za ccm na chadema). Usishangae sana kusoma anachoandika humu.

Habari ndiyo hiyo.
 
Rev. Kishoka,
Yaani hata sina nguvu tena na kumjadili mtu yeyote...after all, siwajui hivyo!

kweli sikio la kufa halisikii dawa
yani hawa watu gani wasioelewa, kila siku waonywe wao tu...
baada ya yaliyotokea kwenye uchaguzi wao tukategemea watajifunza
mabadiliko TZ bado ni safari ndefu sana..
 
...
Wanaona wao ndio wana haki ya kumtukana na kumzushia kila uozo na kugeuza maneno ya Zitto kila wakati wakitegemea Zitto hatakuwa tayari kuwajibu kwa maslahi ya chama chake.

Acha hizo omar,

Mbona Zitto alijibu kwa hasira nyingi sana na kutoa mambo yasiyo na uthibitisho wowote kuhusu kifo cha Wangwe na kuhusu jamii za wachaga ndani ya chadema na kwenye vyombo vya habari.

Unajua inachukua nguvu kidogo sana kumjua mnafiki, uchaguzi wa chadema ulimfunua Zitto kwa watu wengi sana waliokuwa hawamfahamu vyema.

..

Hawa jamaa wanapaswa kukaa chini na kufanya self reflection ya matatizo yao badala ya kukimbilia kutafuta mchawi kwa Zitto ama Omarilyas. Wachawi wao wenyewe wakiongozwa na sumu mbaya za Kiranja aka Mpakakieleweke....

Omar,

Hauna uthibitisho wowote kuwa Kiranja ndiye Mpakakieleweke. Hasira zako hizi mpaka unataka kuvunja sheria za JF?

Kuhusu kumuongelea Zitto, as long as wanakuja hapa na kwengineko na uzandiki wao i will not stop deciphering their cheap and loosy spinnings.....Kama wao wanadhani wana haki ya kumpaka uozo wao wa Zitto basi nami nina haki ya kupambana na uozo wao.

Acha vitisho mkuu,

Hata wewe uzandiki wako hautaachwa kupita hivi hivi. Wewe huitakii mema chadema na hili linajulikana wazi. Mbinu zako za kichochezi hizi nitakutana nazo sehemu yoyote, mahali kokote na wakati wowote ule.
 
Na wewe bana...sasa "undavyaundavya" ndio nini maana'ake?

Julius,

Wewe unamkosoa Mwl? Utakamatwa (msemo wa UD) wakati wa mtihani ... ohh shauri yako.

Kitila, heshima mbele mkuu, this is just a snack
 
Julius,

Wewe unamkosoa Mwl? Utakamatwa (msemo wa UD) wakati wa mtihani ... ohh shauri yako.

Kitila, heshima mbele mkuu, this is just a snack

Heheheheheee...nathubutu kufanya hivyo kwa vile nimekimbia huko. Ningekuwepo unadhani hata ningethubutu?
 
Zitto: Ushauri wa bure: Whenever you feel like saying "I" put "We". There is no "I" in a team with a common cause. Are thinking of "I" now ....mmmh dont say it put "We" then say whatever you want to say..... Ok. Always we we we we we ... right sio 'mimi', "mimi", "mimi":Sisi sisi Sisi.When there is too much I's people gets bored and always want to attack and it is a sign of lack of team work... which is very key ingridient in modern leadership...team work ... thenku ndugu Zitto
 
Zitto - who is Zitto! Made to think by rev and all of you. Who are my friends? Ninaanzia hapo. Kila la kheri
Kwa waliosoma vitabu vya Ngugi wa Thiong'o nadhani watamkumbuka character mmoja kwa jina Kabonyi. That is Zito. Bongolander kakuelezea vizuri sana hapo chini.
You nailed it. Kwenye thread iliyokuwa inazungumzia ununuzi wa mmitambo ya DOWANS nilisema he is a traitor.

Ujasiri wa kuhalalisha tumlipe mwizi wetu?

Ameishia hapo hapo haendi zaidi kwani si mtu wa kujisahihisha

Halafu eti watu wanataka tuamini ni mtu wa misimamo
Mkuu Next Level mimi simfahamu zitto sana ila kwa hii issue ya Dorwans nimeona hana msimamo kabisa maana mara iuzwe baada ya wananchi kuja juu angaangalia nitoke vipi akaja tena na kuitaifisha
That is what is about

Unatoa criticism na inakuwa constructive kama mtu anasikiliza kama ambavyo wewe umeanza kuwa msikivu. Nadhani labda kuna dalili za mafisadi kushindwa (lol) Mchukia Fisadi naona anakufahamu vyema
Kumbe kuna wakati akili zako huwa zinafanya kazi vizuri?
inaelekea mara nyingine ukisema mambo ovyo tofauti na hapa nitakupeleka Milembe!

Wote hatuwezi kuwa mjengoni. Mchango wetu ni mawazo na hayo tulimpa wakati kahongwa tununue dowans. Ka make 360 degrees turn bila kukiri alikosea.

May be I should twist the wind this way. Why are we seeking for Zitto to conform to our desires and needs rather than us conforming to his leadership syle and personality?
Our needs are to see a country without corruption. anybody who associates himself with this vice we can not conform with his leadership and personality.
Mawazo ya ovyo ovyo hayawezi kuheshimiwa kwa sababu tu ya demokrasia




Asante mkuu huwa humng'unyi maneno. Taabu hawa jamaa kumbukumbu zao ni mbofu

Halafu huyu ndio eti alitaka kuwa mwenyekiti wa chama. Na chini ndio mshauri wake.


Je tuliingiaje mkataba wa kuzalishiwa umeme kwa kutumia mitambo chakavu?
Hoja yako hapa ni ipi? Kwamba kwa sababu tuliingia mkataba basi mitambo siyo chakavu au?

Katumwa na mafisadi na anakuja kama nyati aliyejeruhiwa na nyati
Umefanya jumuisho zuri sana.
 
Sasa Cpt Hadock, nini hitimisho lako?

Kama sikufikia hitimisho wacha niseme hapa. Zito anaweza kuwa charismatic kama watu wanavyodai lakini mi nasema siyo. Ni opportunist tu. The guy is arrogant, egoistic and stubborn. Kwa akili ya kawaida huwezi kusema tununue halafu kesho unakuja na tutaifishe bila hata kukiri ulipotoka. Hafai kuwa kiongozi wazee wa CHADEMA waliona mbali ni kama Nyerere alivyomkata JK lakini watu wakaona mzee yule yule alikuwa amepitwa na wakati na sasa tunaona nji inayumba.
 
Quote:


Je tuliingiaje mkataba wa kuzalishiwa umeme kwa kutumia mitambo chakavu?

Hoja yako hapa ni ipi? Kwamba kwa sababu tuliingia mkataba basi mitambo siyo chakavu au?

Blistering Barnacles,

Hoja yangu ni kuhoji aliyesema kuwa TANESCo isinunue mitambo mikuukuu au michakavu. Mimi nikauliza, ilikuwaje tukaingia mkataba wa kuzalishiwa umeme kwa kutumia mitambo mikuukuu?

Je kama mfanp Richmond wangeweza kufanya kazi yao na hawakuwa kampuni ya mazabe, lakini wakatumia mitambo mibovu na chakavu, je pale ambapo wangeshindwa kuzalisha umeme inavyotakikana kutokana na ubovu huo tungemlaumu nani?

Or in other owrds, kwa nini Serikali huruhusu kukodisha mitumba mfano kama ule wa ATCL kukodisha Airbus lililochoka lakini tukaingia gharama karibu sawa na kununua ndege mpya?

That is my point Jellyfish!
 
Would Zitto raise and be as charismatic and motivating like Mwalimu Nyerere?

Zitto, tuko nyuma yako! (Usiogope kama Mzee Mwinyi alipoogopa aliposikia watu wakidai wako nyuma yake! kwi kwi kwi)

Mwinyi ni wa pwani zitto ni wa bara, hahisi wala haogopi mtu kuwa nyuma yake hahaha!
Ninayo machache dhidi ya Mhe. wangu Zitto. Kwanza nikubaliane na wewe Rev.Kishoka, Zitto ni charismatic leader to be. Zitto ana malengo, malengo lazima yapaliliwe kabla ya kufikiwa. Kupalilia kwa Mhe.Zitto, ni kujidhihirisha mbele ya wtz kwa yale anayoyatetea kwa maslahi ya umma. Unapopalilia malengo yako, kuna vikwazo njiani, kwanza, wasiopenda mtizamo wako watakuzulia mabaya ili kukuchafulia juhudi zako. Au kama hauko kwenye system yao kwa lugha rahisi kama si mwenzao basi watajiunga pamoja kwa lengo la kukumaliza. Haya yamefanyika dhidi ya zitto, kasimamishwa Bungeni, akina Matlida Burian mashangingi ya Chama yakishangilia tukio hilo. Lakini umma wa wtz, ulikuwa nyuma yake, wapiga kura wake wako pamoja naye. Tumpe support, tunamkosoe pale anapofanya ndivyo sivyo, tumsaidie kumnyooshea njia apite bila matatizo na kufika kwenye enzi (Urais) anazochugulia bila kukwama. Ni kiongozi, ni mzalendo, ana sifa, ana uchungu na nchi yake, tujiandae kumkabidhi rungu, rungu hilo liwapige Mafisadi wa RICHMOND, KAGODA, RADA, NDEGE YA RAISI, TICTS, IPTL na wenzi wengine wa mali ya umma. Lazima atufikishe pale tunapotaka kwenda, Maisha bora kwa wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…