Soko huria na hatma ya korosho

Agama_Agama

Senior Member
Sep 13, 2016
143
250
Tanzania iliingia kwa nguvu katika soko huria kipindi cha uongozi wa Rais Mkapa. Kwenye soko huria kama yalivyo mambo mengine mengi kuna faida na hasara.

Kwa serikali ya awamu ya tatu kuamua kuingiza nchi katika mfumo huu wa uchumi zipo sababu nyingi na kubwa ikiwa kufeli kwa mfumo wa ujamaa duniani kote, mfumo ambao tumekuwa tukiutumia toka baada ya uhuru.

Serikali ile ilifanya mwendelezo au kurasmisha uchumi wetu kuingia kwenye hili soko huria ambapo serikali iliyopita iliweka misingi.

Huu ni mfumo wa kibepari ambao unamfanya mwenye uwezo zaidi kunufaika zaidi na matunda ya soko. Ni katika kipindi hiki ndipo tuliona kushamiri kwa biashara mbalimbali na hata Rais Mkapa kuheshimika katika bara la Afrika kwa spidi ya kukua uchumi. Pamoja na haya kulikuwa na kesi au shutuma nyingi za ufisadi katika michakato mbalimbali iliyoletwa na soko huria.

Awamu iliyofuata haikubadili mfumo huu pamoja na kuwepo malalamiko mengi kuwa wenye nacho wanazidishiwa. Tuliona pia ongezeko la biashara (za ndani na za nje) huku maisha hata ya yule aliye chini kabisa kwenye mnyororo wa ulaji (food chain) akinufaika na kuona matokeo ya jasho lake. Hapa pia ufisadi ulisemekana kuongezeka na wajanja wachache kuvuna kiulaini majasho ya wadanganyika.

Awamu ya tano ikaja na hoja za kurudisha uzalendo na kufikiria maendeleo ya mdanganyika huku ikichukia hadharani ufisadi na ubadhilifu. Tumeona watu wengi wakifunguliwa mashtaka ya namna mbalimbali za uhujumu uchumi katika awamu zilizopita kwa kutumia mianya na opportunities za soko huria kujinufaisha kwa namna moja au nyingine. Hii ni hatua nzuri!

Hoja ya msingi hapa inakaa juu ya swali hili: JE, KUUA SOKO HURIA NA SERIKALI KUJIMILIKISHA BIASHARA KUNA MSAADA KATIKA MAENDELEO YA KIUCHUMI YA BAADAE?

Swali hili linakuja baada ya kuona mengi mazuri yaliyokwisha fanywa na uongozi wa awamu ya tano na kusahau kuwa sekta binafsi imekuwa sehemu muhimu zaidi ya kukuza uchumi wa nchi. Nilianza kupata maswali wakati tenda za ujenzi wa majengo yanayolipiwa na serikali walipoanza kupewa TBA. Kisha tukaambiwa tenda nyingine wanapewa Suma JKT. hii haikuishia hapo mpaka hivi karibuni tulipoambiwa jeshi litapewa pesa ya kununua korosho kule kwetu kusini.

Hili limeshindikana kama ambavyo mengine mengi yameshindikana au hayakukidhi viwango vya soko. Ikiwa imebaki takribani miezi minne kabla ya maandalizi ya msimu mwingine wa kilimo cha korosho kuanza, bado kuna watu hawajalipwa na hawajui hatma ya korosho zao zilizochukuliwa, maana hazijanunuliwa.

Kwa kunyima soko huria la korosho leo tunasikia yakisemwa kuwa korosho hazina viwango, wale wanunizi walionyang'anywa mchongo hawakuwa na longolongo za namna hii maana kuna madaraja ya viwango vya korosho.

Kwa kiasi kikubwa serikali hii haiwezi kuepuka lawama za wakulima wale maana waliwapa ahadi na kuchukua mazao yao wakiwaaminisha watalipwa better prices. Mlolongo wa malipo na jinsi mchakato ulivyoendeshwa hautoi picha nzuri kwa zao hilo hapo baadae.

My take:

Serikali irudishe uhuru katika soko na ibaki na capacity ya kudhibiti soko bila kuingilia. Kuna kodi zinakosekana na pia kuongeza umaskini wa wadanganyika kuliko walivyokuwa awali. Soko huria ndio mfumo unaotumika duniani kote hakuna namna tutaepuka maana ujamaa ulikufa hatuna budi kuenda na mfumo huu kwa kuweka taratibu thabiti za kuhakikisha tunafaidi kama nchi (na wananzengo).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
munkango

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
342
1,000
Serikali ilifanya makosa ilipochukua fedha za mfuko wa korosho. Baada ya bei kushuka ikawa inabebeshwa lawama na ndio maana ikaingia lakini bila kuwa na mbinu na fedha za kutosha, matokeo yake wakulima wameathirika sana. Cha kufanya inatakiwa Serikali irudishe bil. 250 za mfuko wa korosho na kuachia soko huria lifanye kazi yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Buffet

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
587

baada ya tangazo la ikulu kuwa serikali itanunua korosho wananchi wa lindi,mtwara na tunduru waliandamana kumpongeza mh rasi na walipewa kibari,vipi nauliza safar hii tutapewa kibali cha kuandamana kuililia serikali baada ya kutusababishia hasara kubwa sisi wakulima wa korosho??
 
Agama_Agama

Senior Member
Sep 13, 2016
143
250
Serikali ilifanya makosa ilipochukua fedha za mfuko wa korosho. Baada ya bei kushuka ikawa inabebeshwa lawama na ndio maana ikaingia lakini bila kuwa na mbinu na fedha za kutosha, matokeo yake wakulima wameathirika sana. Cha kufanya inatakiwa Serikali irudishe bil. 250 za mfuko wa korosho na kuachia soko huria lifanye kazi yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani serikali ingeachana na biashara tu. Maana wafanyabiashara wapo na kodi wanalipa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
fred mwakitundu

Senior Member
Dec 31, 2018
141
250
Waliandamana wakijua wameshukiwa na Neeema lakini kinachoendelea kwa kweli ni shida juu ya shinda,kuna uhakiki usiokuwa na kikomo kwa mashamba ya wakulima sijui huu uhakiki ulikuwepo hata kwa wanunuzi binafsi au kwa vile serikali inanunua inahofia wapiga dili?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom