DECI Tanzania: Ilivyoanza, ilipo na hatma yake

DECI Tanzania: Ilivyoanza, ilipo na hatma yake

Taasisi za fedha zinazokopesha baada ya kuweka akiba (mbegu) kama saccos zinategemea sana uaminifu wa wanachama. Ndo maana saccos zinasisitiza sana kuwa watu wa jamii moja yaani mnaojuana na mnauwezo au namna ya kuwajibishana pindi yanapotokea matatizo.

Deci ilianzishwa na waumini wa madhehebu ya kipentekoste ili kujikwamua kiuchumi wao wenyewe. Kwakuwa inaleta mafanikio watu wengine pia wakaamua kuingia. Ninachotaka kumaanisha hapa ni imani ya uaminifu miongoni mwa wanachama.

Nimuombe Mzee Mwanakijiji na wengine wanaopinga Deci kwa nguvu zote kutokana na dhana ya kiuchumi kwamba haipo sustainable watuwekee hapa namna deci inavyofanya kazi. Tusiburuzwe na dhana za vitabuni tu, tusiburuzwe na akina Idd Simba na Pride yake nk. Tumeona siku za karibuni Barclays wamesimamisha mikopo kwa sababu ya hasara kwamba watu wamekopa hawarejeshi, mabilioni ya CIS yamekopwa na matajiri/wanasiasa hayajarudi mpaka leo. Lakini hawa walalahoi wanakopeshana na ni waaminifu kurejesha mikopo.

Ninamaanisha kwamba badala ya kupiga kelele na kueleza dhana za vitabuni, tuseme DECI imefanya nini? kwanini itashindwa na kuishia pabaya. au ni lengo la kutaka kujua mbinu yao ya kibiashara?

These people believes in God, God will not let them down. Maybe is the beginning of economic revolution.
 
hii deci haina tofauti na rostam.....
ccm wanapanda kwa rostam kutumia (dowans, epa) halafu wanavuna wakati wa uchaguzi.
 
Inasikitisha kuona kuwa maaskofu ambao wanatakiwa kuwa na upeo mkubwa wa kuongoza wenzao nao hawaelewi athari za Mchezo kama wa DECI. Taasisi za kidini zinatakiwa ziwe na viongozi wenye ufahamu mzuri wa kiuchumi na pia wawe wanajiendeleze na updates za dunia maana sasa Technolojia ni muhimu. Nini sababu ambazo zimefanya hili swala likafikia hapa lilipo.

1. DECI wameingia kwa njia ya dini ambapo watu wamejenga uaminifu mkubwa sana. Huwezi kumwambi mtu ikiwa swala linaingilia dini.

2. Serikali ilitakiwa igundue hili mapema, ingekuwa na vyombo au idara ambazo zinaweza kugundua mambo kama haya.

3. Kwa maoni yangu ningependa kusema kwa Jina la Upatu lisihusishwe na Pyramid/Ponzi schemes. Maana yangu haswa ni kuwa UPATU kwa taswira yta mtu wa kawaida inawezakuwa kundi la watu wa tano ambapo watu hupokezana hela kwa zamu na uaminifu; huu ni mzunguko iwapo wote watakuwa waaminifu basi mzunguko huwo unaweza kudumu milele bila mpasuko. Sasa kwa taswira yangu Pyramid scheme sio mzunguko bali iko kwenye "straightline".

Malipo hutengemea watu wapya wanao jiunga na kwa hili lazima kutakuwa na mwisho wake tu maana hata Watanzania wote tukijiunga inabidi tutegemee ladba kwa wanaozaliwa ndio walipe mavuno yetu. inaweza kuchukua hadi miaka 40 (kama Bernard Maydoff) lakini mwisho wake utafika na hasara itakuwa kubwa mno. Kwa hiyo tukiita pyramid scheme UPATU basi watu wa kawaida wanaweza kudhani kuwa "Mbona upatu ni poa na wanachama wakiwa nauwezo na uaminifu unaweza kudumu vizuri".

Hapo ndipo watu au wananchi wanaweza kuona kuwa wanaonewa na wasione athari za pyramid schemes. Vile vile hata hizi pyramid schemes zinatofautiana kuna zile zinazo husisha bidhaa na zile zinazo husisha huduma. Nyengine ziko complicated "kwenye internet au emailing system". Kwa hiyo ni vizuri hili jambo likachumbuliwa vizuri.

Pwani Raha contributor
 
Kwa nini Watanzania wanakimbilia kupata fedha za haraka haraka kupitia DECI?
 
Wewe inakuuma nini watu kama madhara walisha pata raha gani watu waliyo nayo hili la DECI ndio umeona , Je madawa feki tunayoletewa na watendaji wa serikali wanaruhusu yapite hauoni ila DECI ndio umeona au umetumwa .
Ruhusu Ubongo wako ufikilie kwanini mpaka sasa tren ni mbovu na haifahi hata kidogo? jiulize vitu kama hivyo.
Kwanini Hospital mpya na kubwa za kisasa hazijengwi?..............
Unakaa unatokwa na povu eti DECI .............blah blah.
Yaaaani ilo ndio umeona bonge la inshu wakati mafukara wanaifurahia na hakuna aliye lalamika.

Two wrongs dont make a right kamanda! Wizi ni wizi haijalishi ananufaishwa nani! Hatutaki double standards hapa! maskini au tajiri wote ni wezi!!
Wewe unaona tu watu wanaovuna wananufaika, haufukirii balaa la mbele itakapokuja kukolapse! na hili ndo tatizo la watu mnafikiria short term sana.

Inaniuma sana kuona watu wafanywa wajinga, na kila Mtanzania inabidi imuume. Na tutaendelea kukandamiza humu hadi mtuelewe au ifungwe hii Ponzi Scheme yenu!!!
 
Inasikitisha kuona kuwa maaskofu ambao wanatakiwa kuwa na upeo mkubwa wa kuongoza wenzao nao hawaelewi athari za Mchezo kama wa DECI. Taasisi za kidini zinatakiwa ziwe na viongozi wenye ufahamu mzuri wa kiuchumi na pia wawe wanajiendeleze na updates za dunia maana sasa Technolojia ni muhimu. Nini sababu ambazo zimefanya hili swala likafikia hapa lilipo.

1. DECI wameingia kwa njia ya dini ambapo watu wamejenga uaminifu mkubwa sana. Huwezi kumwambi mtu ikiwa swala linaingilia dini.

2. Serikali ilitakiwa igundue hili mapema, ingekuwa na vyombo au idara ambazo zinaweza kugundua mambo kama haya.

3. Kwa maoni yangu ningependa kusema kwa Jina la Upatu lisihusishwe na Pyramid/Ponzi schemes. Maana yangu haswa ni kuwa UPATU kwa taswira yta mtu wa kawaida inawezakuwa kundi la watu wa tano ambapo watu hupokezana hela kwa zamu na uaminifu; huu ni mzunguko iwapo wote watakuwa waaminifu basi mzunguko huwo unaweza kudumu milele bila mpasuko. Sasa kwa taswira yangu Pyramid scheme sio mzunguko bali iko kwenye "straightline".

Malipo hutengemea watu wapya wanao jiunga na kwa hili lazima kutakuwa na mwisho wake tu maana hata Watanzania wote tukijiunga inabidi tutegemee ladba kwa wanaozaliwa ndio walipe mavuno yetu. inaweza kuchukua hadi miaka 40 (kama Bernard Maydoff) lakini mwisho wake utafika na hasara itakuwa kubwa mno. Kwa hiyo tukiita pyramid scheme UPATU basi watu wa kawaida wanaweza kudhani kuwa "Mbona upatu ni poa na wanachama wakiwa nauwezo na uaminifu unaweza kudumu vizuri".

Hapo ndipo watu au wananchi wanaweza kuona kuwa wanaonewa na wasione athari za pyramid schemes. Vile vile hata hizi pyramid schemes zinatofautiana kuna zile zinazo husisha bidhaa na zile zinazo husisha huduma. Nyengine ziko complicated "kwenye internet au emailing system". Kwa hiyo ni vizuri hili jambo likachumbuliwa vizuri.

Pwani Raha
 
Kwa nini Watanzania wanakimbilia kupata fedha za haraka haraka kupitia DECI?

Ni mchanganyiko wa vitu, hali ngumu ya maisha, elimu duni ambayo haina critical thinking, serikali iliyolala, mafisadi kila kona, siwezi kuamini kuwa hakuna mkubwa anayepata 10% yake pale Deci!
 
hela ya fasta fasta ajabu!

lakin itaendelea mpaka lini? kadri siku zinavyopita ndivyo watu wanazidi kujiunga/kuweka pesa zaid. lakin hii itaendelea mpaka lin?

hawa deci siamin kama lengo lao ni faida. lengo lano ni 'kusaidia kuleta maisha bora nchini'. safi! kwahiyo hawawezi kuumia mioyoni kama wengine pia wakianzisha deci kama yao.

kama hilo ni kweli basi watuambie ni jins gani wanaendesha hii deci. isiwe siri. waseme lak 2 inawezaje kuwa lak 4 na zaid ndan ya muda mfupi. wasione tatizo kufanya hivyo maana wao lengo lao ni 'kusaidia kuboresha maisha ya mtz'. ama thru deci au kwingineko

baadae serikali na vyombo vyake vinaweza kuja kulaumiwa kwa kuifumbia macho deci (assume itashindwa kuwalipa wanachama wake)
 
I am deeply dissapointed na wakristo hawa wa DECI kwa sababu I've always rated highly katika mamabo ya mipango na hasa maaskofu wao ambao kusema ukweli kulinganisha na masheikh tulionao elimu yao ni ya juu sana

sasa sielewi ilikuwaje kuwaje mpaka wakakubali huu upuuzi wa Ponzi scheme

Mchongo huu ungekuwa BAKWATA sawa lakini hawa jamaa nwa kipentekoste sikudhania

anyway

hebu mie nikajisomee cheche nimeambiwa cheche la wiki hii tamu kichizi
 
Nzeki,
Mkuu kamawewe unaamini hili basi utaamini kila kitu..
Hivi kweli Idd Simba kaingia vipi ktk mjadala huu, mbona wao PRIDE tunaona wanachokifanya na wanasaidia vipi iweje hoja za Deci zibadilike na kuwa za Idd Simba..
Ebu tazama Idd Simba anavyofanya mkuu wangu kuliko hata vyama vya siasa na hizo Saccos zenu ambazo kila kitu kinafichwa.. Lini investment zikawa ni siri ya chombo kinachouza, ama kweli Bongo jamani kila kitu kinauzika....
PRIDE
 
hela ya fasta fasta ajabu!

kama hilo ni kweli basi watuambie ni jins gani wanaendesha hii deci. isiwe siri. waseme lak 2 inawezaje kuwa lak 4 na zaid ndan ya muda mfupi. wasione tatizo kufanya hivyo maana wao lengo lao ni 'kusaidia kuboresha maisha ya mtz'. ama thru deci au kwingineko

baadae serikali na vyombo vyake vinaweza kuja kulaumiwa kwa kuifumbia macho deci (assume itashindwa kuwalipa wanachama wake)

Ndugu yangu hii kitu itakuja kuliza watu tu!! Biashara gani wanafanya? Wanazungusha fedha, kwa hiyo wala usitafute siri, kwa sababu hawana!!! Tatizo unamwambiaje mtu aliyevuna? Yote yanatokea kwa watu kupenda vitu vya bure bila kutoka jasho, nadhani hata wale wajasiriamali wameshaacha kujishughulisha. Hata mafisadi nao wako hivyo hivyo.

Hao maaskofu mbona hawaelezi kinagaubaga namna hii biashara ilivyo, naanza kupata mashaka kuhusu mambo mengi sasa!!
 
Naipenda deci
naitamani deci
usiniache deci
endelea kunitunza nami ntakutunza deci
usiogope vijiba vya roho deci#
i luv u dec

tunaomba mtuachie deci yetu kama mikopo nendeni pride mingi tu mtaikuta
 
Idadi ya washiriki wa Deci wazidi kuongezeka

Na Waandishi Wetu

IDADI ya wanachama wanaopanda katika taasisi ya Development Intrepreneurship Community Initiative (Deci), imezidi kuongezeka baada ya wanachama karibu 2,000 kupanda kwenye ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo zilizoko Mabibo Dar es salaam.


Benki Kuu (BoT) imetoa tahadhari kwa wananchi kuwekeza fedha zao kwenye taasisi hiyo, ikisema kuwa mfumo unaotumika ni ule wa kuchangia wachache na kwamba bado inafanya utafiti kabla ya kuchukua uamuzi.


Lakini tahadhari hiyo inaonekana si kitu mbele ya watu na badala ya wanachama kupungua, idadi inazidi kuongezeka.


Jana mabasi ya daladala yaendayo Mabibo yalikuwa yanafurika abiria ambao walieleza bayana kuwa walikuwa wakielekea kuwekeza fedha, ambazo hulipwa kwa zaidi ya mara mbili yake katika muda wa wiki 16 hadi 20.


Katika ofisi za taasisi hiyo zilizoko Mabibo, kulikuwa na msululu wa watu waliojipanga kwenye mistari kwa ajili ya kuonana na uongozi wa taasisi hiyo kwa shida mbalimbali.


Mistari ilianzia kwenye ofisi za Deci hadi katika lango la Chuo cha Usafirishaji (NIT), ambacho kiko takriban mita 500 kutoka ofisi za taasisi hiyo.


"Tunaenda kupata namba ili tuweze kuingia ofisi za Deci," alisema mmoja wa watu waliokuwa kwenye foleni hiyo alipoongea na Mwananchi.


“Sijui nitaanzia wapi kama foleni ndio ipo hapa.”


Watu wa rika na kada mbalimbali walikuwa kwenye misululu hiyo, wengi wakitaka kuwekeza fedha na wachache wakitaka kuondoa fedha zao. Tayari Deci imeshaeleza kuwa itawarejeshea fedha wale tu ambao wana shida kubwa kwa kuwa mkataba wao na washiriki ni kwa ajili ya kupanda na kuvuna na si kung'oa mbegu.

Wakizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalum jijini Dar es Salaam jana, wanachama hao walisema wanaendelea na upandaji wa mbegu na kwamba bado wana imani na taasisi hiyo.


“Tumekuja kupanda mbegu na sio kung’oa, kwa sababu tumeshawahi kupata faida kubwa ambayo imetufanya tuweze kuendesha familia zetu," alisema Rehema Juma.


Alisema kitendo cha serikali kutaka kuifunga Deci ni kinyume na taratibu na kinawaumiza wananchi wanyonge, hivyo walikuwa wakisubiri tamko rasmi la taasisi hiyo ili waweze kupanda mbegu.


Alisema zaidi ya watu kumi katika familia yake wamenufaika na Deci, kutokana na hali hiyo wanaamini kuwa matatizo yanayojitokeza hivi sasa ni chuki ambayo inawakandamiza wanyonge.


Mwanachama mwingine, Juma Abdalah alisema tangu aanze kuisikia kampuni hiyo hawajahi kusikia malalamiko ya kutapeliwa kwa hiyo anaamini kuwa maneno ya sasa dhidi ya Deci ni fitina.


“Tunajua kuwa wanachama wengi waliokuwa katika taasisi mbalimbali za fedha wamehamia Deci. Jambo hili linaiudhi serikali ndio maana inapiga kelele. Sisi hatuachi kupanda kwa sababu tunasubiri tukivuna tunaweza kufanikiwa kimaisha," alisema Abdalah.


Wakati wanachama hao wakiendelea kupanda, baadhi walifika ofisini hapo kung'oa mbegu walizopanda kwa hofu ya kutapeliwa.



Kutokana na watu wengi kutaka kupanda na baadhi kung'oa, wananchi wa maeneo ya Mabibo na jirani walipata adha kubwa kutokana na kuwepo kwa mikusanyiko mikubwa iliyosababisha hata magari kupita kwa shida.


Katika vituo vya vya daladala vya Usalama Magomeni, Mwembechai, Kagera, Manzese, Tiptop na Mahakama ya Ndizi, usafiri wa daladala ulikuwa wa shida kutokana na msongamano wa wasafiri hao.


“Mabibo sasa imekuwa kama Mbagala,” alisema abiria mmoja.


“We huoni abiria wanavyopigana pale kugombania magari. Kabla ya kuibuka kwa sakata la Deci ulikuwa unachagua magari ya Mabibo lipi unataka kupanda na lipi hutaki, lakini leo hata ukileta Lori watapanda,” alijibu abiria huyo.


Kufuatia ongezeko la abiria hao, baadhi ya magari yanayofanya ruti nyingine tofauti na Mabibo, yalikuwa yakikatisha ruti zao na kwenda Mabibo kutokana na ushauri wa wapigadebe wao vituoni.


Akizungumza na Mwananchi ofisini hapo, mteja mmoja wa Deci ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, aliilaumu serikali kwamba lengo lao ni kuiua kampuni hiyo kwa hofu kwamba kuendelea kwake kutapunguza mapato ya serikali.


“Serikali inaogopa kwamba itafika wakati watu watakuwa hawafanyi tena kazi kwa kuwa wanajua, wakiweka fedha Deci wanapata faida kubwa tena kwa muda mfupi,” alisema.


“Wafanyakazi wanalipa kodi, kwa hiyo kodi itakosekana serikalini, jambo ambalo linaweza kupunguza mapato ya serikali, NSSF na hata mabenki, hiyo ndio hofu yao.”
 
Maelfu ya watu Dar wakutana kudai shughuli za Deci ziendelee





Sehemu ya maelfu ya wanachama wa Deci, wakiwa katika mkutano katika Jengo la PTA Uwanja wa Saba saba wakidai kuendelea kwa mpango wao baada ya kuonekana kwa dalili za kusimamishwa na serikali.

Na Waandishi Wetu

MAELFU ya wanachama wa Taasisi ya Development Entrepreneurship Community Initative (Deci) kutoka sehemu mbalimbali nchini, jana walifurika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, kujua hatima yao kutoka kwa uongozi wa taasisi ulioitisha mkutano huo.


Katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa PTA katika viwanja hivyo, huku mvua kubwa ikinyesha, viongozi hao walimtaka Rais Jakaya Kikwete kuwa makini na ushauri wa kuifungia taasisi hiyo kwa kuwa umetolewa na wachache katika misingi ya unafiki.


Viongozi hao ambao walidai kutoyumbishwa, walitangaza kuendelea na shughuli zao na kuitaka serikali kutokurupuka kuchukua maamuzi.


Umati huo wa watu uliokadiriwa kukaribia wa watu wanaofika katika viwanja hivyo kwa ajili ya maonyesho ya SabaSaba kila mwaka, ulihudhuriwa na wanachama kutoka mkoa wa Dar es Salaam, Morogoro, Pwani na Lindi.


Kadiri muda ulivyosonga, idadi ya wanachama ilizidi kuongeza na wengi wao walifika kwa magari binafsi na usafiri wa daladala.


Baadhi ya wanachama waliokuwa wakishuka kwenye magari hayo walikuwa na mabango na wengine kuhoji hatima ya taasisi hiyo na kulaani hatua ya serikali kuingilia huduma hiyo ambayo waliasema inawasaidia kukabiliana na umasikini.


Baadhi ya mabango hayo yalisomeka: “Mmeshindwa kutuambia kiasi gani cha pesa za EPA zimerejeshwa, mnaamua kutuzuia wanyonge tusinufaike na Deci”, “Matajiri, tuacheni na sisi wanyonge tunufaike na Deci”.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa taasisi hiyo inayoundwa na Baraza la maaskofu wa Makanisa ya Pentekoste Tanzania (PCT), walisema tasisi hiyo ilianzishwa baada ya kubaini kuwa vyombo vingi vya kuinua uchumi vilivyoanzishwa nchini vilikuwa vikijali faida kubwa kuliko kuwatetea wanyonge.


Akisoma tamko la Deci kwa niaba ya wenzake, maaskofu hao, Bathromeu Sheggah, alisema inasikitisha na inakatisha tamaa kuona kwamba kwa kipindi cha miaka isiyopungua mitatu ya huduma ya taasisi hiyo, Benki Kuu (BoT) inatangaza katika vyombo vya habari kuwa taasisi yao haitambuliki.


Alisema tangu waanzishe taasisi hiyo, Serikali imefanikiwa kupata zaidi ya Sh120, 674,497 milioni kama kodi ya mapato na kuwa wafanyakazi 400 wa taasisis hiyo wamekuwa wakilipiwa kodi ya mapato ‘PAYE’ na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).


Alisema ikiwa serikali italazimisha kusitisha kwa huduma za taasisi yao, wananchi wapatao 3,500,000 toka kwa washiriki wao 700,000 wataathirika kiuchumi, kiafya, kielimu na kijamii na hatimaye kuchangia vunjivu kwa amani ya nchi.


Alisema hasara nyingine ni kukosekana kwa ajira sambamba na serikali kutofaidi mzunguko wa fedha unaotokana na mapato ya wajasiliamali wanaovuna fedha kutoka katika shirika hilo.


Askofu Sheggah alisema kuna mashirika mengi yanayotoa mikopo kwa riba kubwa ambayo yamekuwa yakiwafedhehesha wananchi wanaoshindwa kurudisha madeni kwa kuwafilisi mali zao bila huruma, kuwanyang’anya mali zao zikiwemo nyumba na mashamba na kuwaacha wakiendelea kuwa maskini.


Alimtaka Rais Kikwete kulisaidia shirika hilo ili tamko la serikali litakalotolewa liwe la haki kwani kitendo cha kutoa ajira 400 na kuwalipa wafanyakazi mshahara unaowawezesha kumudu maisha yao, kumechangia kutimiza ahadi aliyotoa wakati akiingia madarakani kuwa ataongeza ajira kwa watanzania.


“Mtoto wako akifanya vizuri msaidie, usimkatishe tamaa hivyo serikali inapaswa kuingiza macho na miguu yake kuisaidia Deci ifanye vizuri zaidi, ili tuweze kufanya shughuli zetu kihalali kama kuna kasoro, lakini si kutunyoshea vidole na kutulaumu wakati lengo letu ni jema, ambalo ni kutekeleza ilani ya CCM”, alisema na kuongeza:


“Kama yapo mapungufu yoyote ya kuanzishwa kwa Deci yashughulikiwe kwa busara badala ya kutoa vitisho vya kukifunga chombo hiki ambacho kimo mioyoni mwa wananchi wengi wanaonufaika nacho,” alisema Askofu huyo.


Maaskofu hao walisema nia ya kuanzisha taasisi hiyo ni kuunga mkoano Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kauli mbinu yake ya ‘Maisha bora kwa kila Mtanzania’, baada ya kubaini kuwa idadi kubwa ya waumini wao wanaishi maisha duni bila kupata msaada wowote.


Aliitaka serikali kuhakikisha kuwa BOT inaendelea kufanyakazi kwa kufuata taratibu bila kuangalia au kusikiliza maneno ya uchochezi yanaoweza kuifanya itoe maamuzi yatakayoiathiri idadi kubwa ya watu.


“Tunaitwa wezi, tumeiba nini? Tangu Deci ianze kazi miaka mitatu iliyopita, hatujawahi kupata malalamiko ya kudhulumiwa kutoka kwa mwananchi yeyote, licha ya kuwa tunawashiriki wengi wao wakiwa wananchi wenye maisha ya chini ambao walisahaulika kabisa” alisema


Akielezea mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo, Askofu Sheggah alisema kuwa wamechangia kukuza uchumi wa wananchi na wa nchi na kutekeleza mkakati wa taifa wa kupunguza umasikini na ikiwezekana kuutokomeza kabisa.


Alidai kuwa Deci imeleta matumaini makubwa kwa wananchi wa kipato cha chini wakiwemo wamachinga, mamalishe, faraja kwa wajane na yatima.


Alisema huduma yao imewawezesha watu wengi kulipa karo za shule na kuinua maisha ya wastaafu waliojiunga na taasisi hiyo tofauti na kabla hawajajiunga Deci.


Aliongeza kuwa wamekuwa wakitoa elimu maalum kwa wajasiriamali wanaochukua fedha hizo kwa ajili ya mitaji ya biashara, hivyo kufanikiwa kukabilina na ushindani wa kibiashara na kupata faida, ambayo kwa njia moja ama nyingine imekuwa ikilinufaisha taifa.


Maaskofu hao walisema katika kipindi cha takribani miaka 48 tangu uhuru, vyombo vya kuinua uchumi nchini zikiwemo benki zimekuwa zikizijali faida bila kuzingatia viashiria vya ukandamizaji, unyonyaji na umaskini hali iliyowafanya wabuni njia itakayomwezesha mnyonge kupata sehemu ya kukimbilia.


Walisema licha ya vyombo hivyo kuwepo, ukweli umebaki pale pale kwamba, wananchi wengi vijijini na mijini wameathirika na ujinga, maradhi na umaskini wa kipato huku baadhi yao wakipata mlo mmoja kwa siku.


Walisema kwa mantiki hiyo, taasisi hiyo haikuona sababu ya kuacha kuendesha shughuli zake kwa kificho ili kuwakommboa maskini.


Hata hivyo, baadhi ya wanachama walionekana kububujikwa na machozi huku wakishindwa kuelewa hatma ya Deci kwa serikali kwa sababu wanadai kuwa inawasaidia kimaisha na hawakuwahi kupata tatizo tangu wajiunge na shirika.


Deci ni shirika lililoanzishwa na taasisi za kidini chini ya ulezi wa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya pentekoste ili kuwasaidia waumini wao na jamii nyingine zisizo za kikristo kuinua hali zao maisha.


Wakati mkutano huo ukiendelea viwanja ni hapo, mamia ya wanachama wengine walikuwa wamekusanyika makao makuu ya taasisi hiyo iliyopo Mabibo kwa lenga la kupanda na kuvuna fedha.


Kama ilivyo katika viwanja vya Sabasaba, idadi ya wanachama hao ilikuwa ikiongezeka kadiri muda ulivyosonga mbele ingawa hawakufanikiwa kuonana na viongozi wa Deci.


Baadhi ya wanachama waliozungumza na gazeti hili waliendelea kupinga mtazamo wa serikali kuwa taasisi hiyo ni ya kitapeli, haijawahi kuwaibia katika kipindi chote cha miaka mitatu ilichotoa huduma.


“Huu ni mpango wa serikali kutaka wananchi wa chini wasiendelee kwa kuwa wameona watu wanatoa fedha zao katika benki na Saccos na kuziweka Deci," alisema mmoja wa wanachama hao ambaye jina lake halikupatikana.


Wakati huo huo, Chama cha NCCR-Mageuzi kimeitaka serikali kuichunguza kwa undani taasisi hiyo na kusaidia kuboresha huduma zake kwa jamii badala ya kutaka kuifunga.


Katibu Mkuu wa NCCR, Samwel Ruhuza alisema jana kuwa serikali inatakiwa kuichunguza taasisi hiyo kuona kama ina kasoro na hatimaye itafute mbinu ya kuiwezesha.


“Serikali kupitia Benki Kuu ina wajibu wa kujua Deci inapata vipi faida, lakini pia iangalie njia zinazotumika kulipa wateja maana ukiweka fedha Deci, baada ya siku cheche unachukua nyingi sasa hapa kinachotakiwa ni kutambua njia wanazotumia kupata fedha zote hizi za kuwalipa watu.


“Kwanza wana wateja wengi na inawezekana wakazishinda hata benki zilizoanza biashara siku nyingi, wachunguzwe kama wapo sahihi waboreshewe huduma hadi mikoani, lakini kama wanafanya uhuni wachukuliwe hatua,” alisema Ruhuza


Alisema mpaka sasa hakuna malalamiko yeyote yaliyotolewa na wananchi kuhusiana na taasisi hiyo, hivyo inaonyesha wazi kuwa haina tatizo lolote kwa wananchi.


“Sina uhakika lakini sijawahi kusikia kama kuna malalamiko juu ya taasisi hii, hivyo inaonyesha kuwa watu wanaweka fedha zao na kupata faida bila kuwa na kasoro zozote” alisema Ruhuza


Kwa mujibu wa taratibu za taasisi hiyo, mshiriki huwekeza kati ya Sh10,000 na Sh5 milioni na kulipwa zaidi ya mara mbili kwa kiasi hicho katika muda wa kuanzia wiki 13 hadi 20 kwa wanaowekeza fedha nyingi.


Hata hivyo wakati Deci ikizidi kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kona mbalimbali za nchi, mamlaka za serikali zimezidi kuimaliza baada ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kusema hiyo si benki bali ni kampuni ambayo imesajiliwa kutoa mikopo kwa wajasiriliamali.


Kauli hiyo ya TRA ni ya nne kutolewa na mamlaka za serikali, ambapo tayari BoT imesema haijatoa kibali cha kibenki kwa Deci, huku Wizara ya kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana pamoja na Soko la Mitaji na Hisa, wakipinga kazi za Deci.


Akizungumza na gazeti hili jana Mkurugenzi wa Elimu kwa Walipakodi wa TRA, Protas Mmanda, alikiri kuwa Deci imekuwa ikilipa kodi kama kampuni ya kutoa mikopo kwa wajasiriliamali kama inavyoonyesha katika usajili wake.


Kwa mujibu wa Mmanda, TRA ilisajili Deci kama mlipa kodi kwa kigezo ambacho kimo katika usajili wake huo kutoka Wakala wa Usajili wa Makampuni na Majina ya Biashara (Brela).


Mmanda akifafanua, alisema katika usajili huo, Deci inaonekana ni kampuni ya biashara iliyoanzishwa kutoa mikopo kwa wajasiriliamali na si vinginevyo.


Mkurugenzi huyo wa TRA alisema, hata hati ya makubaliano (MoU) ambayo hutumika kama katiba, inaonyesha Deci si taasisi ya kibenki.


Alipoulizwa awali kwamba, vipi wamekuwa wakipokea pesa za kodi kutoka kwa kampuni ambayo inajiendesha kinyume cha sheria alijibu: "Hadi sasa tunasubiri ripoti yao ya hesabu ya mwaka 2008."


Mmanda akifafanua, alisema ni kweli Deci imesajiliwa kama mlipakodi wa TRA kwani tayari ililipia usajili wa awali kwa biashara inayofanya baada ya kujisajili na kupewa cheti (TIN).


Hata hivyo, alisema Deci ilianza kazi zake mwaka jana baada ya kuomba kujisajili mwaka 2007 na kuongeza kwamba, hesabu za mwaka wa kwanza wa kulipa kodi wa kampuni hiyo zitaanza kutolewa Juni mwaka huu.


Habari hii imeandaliwa na Tumaini Msowoya, Patricia Kimelemeta, Hidaya Kivatwa, Victoria Kombe, Fidelis Butahe na Ramadhani Semtawa
 
Natoa ushauri kama ifuatavyo, Deci kwavile maskini wanadai kuwa inawapa maisha Bora basi serikali iungane nayo hata yale mabilion ya Jk yapitie huko Deci. Lakini hawa viongozi wa Dini wana Akili sana maana wamebu kitu ambacho kita wainua Watanzania woote waislam kwa wakristo. Kazi nzuri sana. Serikali uchukue nafasi yake kuweka wataalamu na washauri maana Deci imekuwa huduma ya kijamii.
 
Milioni 26/- za DECI zaibwa..!
Watu wasiofahamika wamevamia katika ofisi za taasisi ya fedha ya DECI inayowezesha watu kupanda na kuvuna mapesa kwa faida ya zaidi ya asilimia 250 na...

From IPPMEDIA Main Page page ya full story haifunguki.
 
Mjadala wa DECI ufungwe mara moja,wahusika wakamatwe watiwe lupango,kwisha.Sheria iko wazi kuchezesha upatu ni criminal offence, period,hakuna cha kujadili hapa,huwezi kujadiliana suala la mhalifu na kujiuliza kama umkamate au usimkamate ,huo sio utawala bora.

As for me this is my last post on this DECI ponzi scheme,hamtanisikia tena naizungumzia,i am fed up na ujinga wa DECI.
 
Watanzania Wengi bado wako nyuma katika kuitika hasa katika masuala ambayo mtu kaona mmoja kavuna mara tatu basi na yeye hata akiambiwa kuwa hilo ni shimo ambalo likifunga umeumia, hatokusikia.
 
Back
Top Bottom