DCI Manumba: Mwakyembe hajalishwa sumu!

DCI Manumba: Mwakyembe hajalishwa sumu!

Nimefurahi jeshi la polisi limemshushua Sitta.

Huyu sita ni mtu wa kuogopwa sana! naona ni mnafiki na mchonganishaji!
 
Lakini Dr Kasema kuwa anakwenda Appolo atakapo rudi ndio ataweka wazi,so tusubiri na subira huvuta kheri

i really agree with you..hakutaka ku disclose mwenyewe ugonjwa nwake that time perhaps his doctors told him may be he was in INCUBATION period,so maybe ilikuwa ngumu ku trace uwepo wa sumu....wakamwambia this time wao doctors watakuwa in a gu position ku detect kila kiti..thats why kasema akirudi this time ataweka kila kitu hadharani....
 
Wanabodi, tuacheni conspiracy theories, vuteni subira kwanza mkijue anachoumwa ndipo mziendeleze hizi conspiracy theories zenu!.

Serikali makini itamshughulikia Sitta haraka iwezekanavyo, scrap him his ninisterial positions na kumpandisha kizimbani kwa kosa la "uchochezi"!.

How much are you paid for being a VUVUZELA? Next time andika kwa kiswahili kingereza hukijui ....." Ministerial positions"!!! should be ...'Ministerial position". Sababu ya degree zenu za kuchonga!
 
Wanabodi nilishauri huko nyuma na hapa nashauri tena, tupunguze conspiracy theories tusubiri tamko la Mwakiyembe mwenyewe!.Japo naye ili kumlindia Sitta heshima, anaweza kusema "Nimesha Muachia Mungu, hivyo naomba nisizungumze chochote"! hivyo kutosema anaumwa nini!.
Mkuu Pasco, tulikwambia awali kabisa kuwa ni makosa kuchukua 'side' bila kuwa na mitazamo tofauti. Nashukuru kuwa umeliona hilo na ku-retreat kutoka katika maneno haya
By Pasco Serikali makini itamshughulikia Sitta haraka iwezekanavyo, scrap him his ninisterial positions na kumpandisha kizimbani kwa kosa la "uchochezi"!.
quote_icon.png
By Pasco
viewpost-right.png
Mkuu Nguruvi3 kwenye hili la sumu, mwisho wa uwezo wa serikali kusema sio sumu ndio hapo. Serikali haipaswi kusema ilichunguza nini na ni kwa vigezo gani waliend up kuhitimisha sio sumu. Ile hoja kuwa alishalalamika huko nyuma bali polisi hawakufanya chochote its still valid, polisi walipaswa wauambie umma wa Watanzania why ili wengi wenu msio mwelewe vizuri Mwakyembe what he is really is!.Tuhuma za Mwakiyembe kutishiwa kuuwawa,sasa hizi tuhuma za sumu si angalau wamejibu!, si wangeweza kukaa kimya na wasiulizwe chochote kama kawaida yao!.
Hakuna conspiracy bali ni ukweli unaotokana na maneno ya Nahodha, Pinda na Manumba.

Conspiracy ni pale mtu atakapodai kuwa ima amelishwa au la kwa maneno ya kufikirika.
Nimeandika huko nyuma kuwa lazima tu- strike balance kwa yale tunayosikia na kuambiwa, na ni wajibu wetu kufikiri na si kumeza kila kitu midhali aliyesema ni DCI kwa niaba ya serikali.

Kwakuwa unashauri suala hili tuliache hadi Mwakyembe atoe habari zake, basi ni vema mkuu ukaomba radhi kwa mambo yafuatayo
1. Kumhukumu Sitta na kudai afutiwe wadhifa na kufikishwa kizimbani kama nukuu inavyoonekana
2. Kutoa picha tofauti ya Dr Mwakyembe ili 'tusio mwelewa tumwele' kama nukuu inavyosema hapo juu.
3. Kuitetea serikali kuwa imekamilisha kazi kwa kusema siyo sumu kama nukuu inavyoonyesha hapo juu.
 
Kama hajalishwa sumu wangetoa ufafanuzi nini kinamsibu ?.

Kama unaamini Mwakyembe kalishwa Sumu mwambie atoe vyeti hadharani, Mwakyembe na Sitta watajuta kutumia ugonjwa kwa ajili ya faida za kisiasa
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Sitta matatani [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Friday, 17 February 2012 21:42 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0diggsdigg

sitta-mikono-top.jpg
Waziri wa Afrika Mashariki,Samuel Sitta

Festo Polea
WAZIRI wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ameingia matatani baada ya Jeshi la Polisi nchini kutolea tamko ugonjwa wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na kueleza kuwa hautokani na kulishwa sumu, huku likisema limefungua jalada kwa ajili ya uchunguzi wa kauli yake hiyo.

Tamko hilo la polisi lililotolewa jana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. DCI Manumba aliwataka watu kuupuza madai hayo akieleza kuwa ushahidi uliopatikana kutoka nchini India alikolazwa Dk Mwakyembe hauonyeshi kuwa alilishwa sumu. Manumba alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya kumaliza mkutano wake kuhusu hali na mwenendo wa uhalifu nchini katika kipindi cha mwaka jana.

Akifafanua kuhusu kauli hiyo ya Waziri Sitta, DCI Manumba alisema, "Jeshi la Polisi limekaa kimya muda mrefu likifanyia uchunguzi kauli hiyo kwa kuwa maneno hayo ndani yake yanaonyesha jinai." Aliendelea “Kazi ya Jeshi la Polisi ni kuchunguza makosa na si kufuatilia nani anaumwa ugonjwa gani. Nani anaumwa nini ni jukumu la madaktari. Lakini tumekuwa kimya muda mrefu tukichunguza tuhuma hizo nzito.’’ DCI Manumba aliendelea kufafanua “Ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India.

Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu katika maradhi yanayomsibu Mwakyembe.’’ Manumba aliongeza kuwa kwa kuwa suala hilo ni la kisheria na kiupelelezi, Jeshi la Polisi linaandaa jalada la upelelezi kuhusu kauli hiyo ya Waziri Sitta na likikamilika, litapelekwa kwa DPP kwa ajili ya uamuzi.

“Hata hivyo, Sitta mwenyewe nilimsikia katika kauli yake akisema kuwa naye ameisikia katika vyombo vya dola, hivyo tunaandaa jalada la upelelezi na likikamilika litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kwa uamuazi wa kisheria wa nani ashtakiwe au nani ana makosa. Lakini sasa ni hayo kuhusu kauli hiyo Waziri Sitta ninayoweza kusema,’’ alisema Manumba.

Awali Manumba alisema kabla Dk Mwakyembe hajaanza kuumwa na kukimbizwa India kwa matibabu, Jeshi la Polisi lilipokea maandishi kutoka kwa waziri huyo yaliyodai kuwa alikuwa akitishiwa uhai wake, lakini likiwa katika hatua za mwisho kukamilisha upelelezi wake, akaanza kuugua na kukimbizwa India kwa matibabu.

“Jeshi la Polisi liliwahi kupata maandishi kutoka kwa Mwakyembe kuwa anatishiwa uhai wake, lakini tukiwa katika hatua za mwisho za uchunguzi, Mwakyembe akaanza kuumwa,’’ alisema Manumba. Historia ya ugonjwa wa Mwakyembe Dk Mwakymbe alianza kuumwa Oktoba 9 mwaka jana na baadaye kupelekwa nchini India na kulazwa katika Hospitali ya Apollo kwa matatibu. Alirejea nchini Desemba 11, mwaka jana baada ya kulazwa hospitalini humo kwa takribani miezi miwili.

Msemaji wa familia ya Dk Mwekyembe na Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa alisema mara baada ya mbunge huyo wa Kyela kurudi nchini kuwa, afya yake ni nzuri ndio maana ameruhusiwa kutoka hospitali.

Kauli za Waziri Sitta Mara kadhaa Waziri Sitta amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akisisitiza kuwa ugonjwa wa Dk Mwakyembe, umetokana na kulishwa sumu. Akiwa kwenye uzinduzi wa Programu ya Neno la Hekima kutoka kwa Kiongozi iliyoanzishwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe, Jijini Dar es Salaam Januari 28 mwaka huu, Sitta alisema:

“ Nasema Dk Mwakyembe kapewa sumu, kama vyombo vya uchunguzi vinasema siyo, basi watueleze ukweli, tena haraka,” alisisitiza Waziri Sitta katika hafla hiyo.

Sitta alihoji “ Ni vipi uone binadamu ambaye ukimshika katika ngozi unga unamwagika chini, mhudumu anakuja kuufagia, lakini baada ya saa moja unarudia tena, kitu hicho si cha kawaida.” Sitta alisema wamejaribu wameshindwa kwa kuwa Dk Mwakyembe analindwa kwa jina la Yesu ambalo ni kubwa kuliko yote.

Waziri Nahodha
Akijibu moja ya kauli hizo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nohodha alimtaka Waziri Sitta awasilishe ushahidi wake ili ufanyiwe kazi badala ya kuzungumza nje ya vyombo vya sharia. Hata hivyo, Sitta alisema hatapeleka ushahidi wa madai aliyotoa kuwa Dk Mwakyembe alilishwa sumu kwa kuwa polisi tayari wanao ushahidi.

Alisema wanachotakiwa kufanya Polisi ni kufanya uchunguzi kuhusu madai hayo ya Dk Mwakyembe kulishwa sumu kwa kuwa ushahidi wanao na wasianze kurushiana mpira.
“Waziri Nahodha anataka ushahidi gani ikiwa taarifa za madaktari zinazomhusu Dk Mwakyembe kuhusu sumu aliyopewa zilishapelekwa polisi, anataka mimi nitoe ushahidi gani,” alisema Waziri Sitta.

Kuhusu mwenendo wa uhalifu nchini kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana 2010, Manumba alisema kulikuwa na matishio mbalimbali ya usalama ikiwamo ugaidi, uharamia baharini, wahamiaji haramu na biashara haramu ya usafirishaji binadamu. Manumba alitaja matishio mengine yaliyojitokeza mwaka huo kuwa ni uingizwaji bidhaa bandia na silaha haramu, dawa za kulevya, migogoro ya kisiasa, kidini, migogoro ya wanafunzi wa taasisi na vyuo vya elimu ya juu na migogoro na migomo ya wafanyakazi. [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Iko hivi Dr Mwakyembe ni kweli kabisa hakuwekewa sumu kwenye chakula. Sumu iliingiaje kwenye mfumo wa kimwili wa Harrison? Alikuwa akiviziwa sana na jamaa walimwekea sumu kwenye sabuni ya kunawia mikono Dodoma, mara baada ya kuitumia ile sabuni ilitoweka. Cartel ya waliohusika kufanya uharamia huo wa kumtegeshea sumu Mwakyembe inaongozwa na Mbunge wa Monduli, ambaye bunge lilimlazimisha aachie ngazi nafasi ya uwaziri mkuu. Wahusika wote waliisha lipwa kwa kazi hiyo na wana kiapo cha kutosema kwa mtu yeyote.

Kama wana kiapo cha kutosema popote wewe uliyapata wapi yaya?Na hapo popote ni wapi? Inawezekana nawe ukawa KAYUMBA wa kata aka DiCiAI:A S-coffee:
 
Tutabaki kufanya speculation, assumption, conspirancy theories etc Lakini UFUNGUO wa JIBU hili anao Dr. Mwakyembe na report ya madaktari kutoka Appolo India.

SWALI langu ni kwanini Si Dr. Mwakyembe wala Serikali ambao wako tayari kuiweka hadharani report ya madaktari wa Appolo?

Dr. Mwakyembe anasema kwamba tayari report ameshapa serikali na amewaruhusu Serikali kuiweka hadharani.

Seriikali inasema ugonjwa wa mtu ni SIRI anayeweza kuuweka wazi (report) ni mgonjwa mwenyewe (Dr. Mwakyembe).

Kutokana na sintofahamu hiyo mimi ninaona sababu za serikali zina mashiko. THE ONUS STILL LIE IN DR. MWAKYEMBE'S SHOULDERS
 
Tanzania ni nchi ya Wasanii, Chochote kinawezekana.

Mkuu polisi wakishirikiana na wizara ya afya ndio wametoa report .. nyengine wanazoamini watu ni uzushi mtupu ..

Sent from my HTC Incredible S using Tapatalk
 
Kwa wale mliofuatilia taarifa ya habari hapo jana ITV Mkurugenzi wa Makosa ya jinai DCI manumba alikanusha yale yaliokuwa yakisemwa na Mh.sitta juu ya kinachomsibu Mh. mwakyembe kwamba alipewa sumu.Sasa kinachotatanisha man jf ni kuwa ni nani mkweli kati ya sitta na manumba?.Je! WATANZANIA WAMUAMINI NANI???..Mh.SITTA au DCI MANUMBA?
 
Mkuu Pasco, tulikwambia awali kabisa kuwa ni makosa kuchukua 'side' bila kuwa na mitazamo tofauti. Nashukuru kuwa umeliona hilo na ku-retreat kutoka katika maneno haya Hakuna conspiracy bali ni ukweli unaotokana na maneno ya Nahodha, Pinda na Manumba.

Conspiracy ni pale mtu atakapodai kuwa ima amelishwa au la kwa maneno ya kufikirika.
Nimeandika huko nyuma kuwa lazima tu- strike balance kwa yale tunayosikia na kuambiwa, na ni wajibu wetu kufikiri na si kumeza kila kitu midhali aliyesema ni DCI kwa niaba ya serikali.

Kwakuwa unashauri suala hili tuliache hadi Mwakyembe atoe habari zake, basi ni vema mkuu ukaomba radhi kwa mambo yafuatayo
1. Kumhukumu Sitta na kudai afutiwe wadhifa na kufikishwa kizimbani kama nukuu inavyoonekana
2. Kutoa picha tofauti ya Dr Mwakyembe ili 'tusio mwelewa tumwele' kama nukuu inavyosema hapo juu.
3. Kuitetea serikali kuwa imekamilisha kazi kwa kusema siyo sumu kama nukuu inavyoonyesha hapo juu.
Mkuu Nguruvi3 nakubali yaishe kama ifuatavyo,

1. Samahani Kumhukumu Sitta mapema kwa kutaka afutwe uwaziri na kupandishwa kizimbani kwa kosa la uchochezi. Anayepasa kunfuta kazi sio mimi bali mwajiri wake, na anayepaswa kihukumu pia sio mimi bali ni hakimu'. Pia nachukua fursa hii kuwaomba wana jf wenzangu tusiwe wepesi kuhukumu, tusije kuhukumiwa!. Samahani!

2. Samahani kwa Kutoa picha tofauti ya Dr Mwakyembe ili 'msio mwelewa mwelelewa' mwelewa what he really is!. Naomba mtapima tuhuma zake na kulinganisha na ukweli halisi. Hivyo jukumu la kuwaelewesha zaidi kuhusu Mwakiyembe halitakiwi kuwa la kwangu bali facts zitajipambanua wazi hivyo wakuelewa wataelewa na sio kueleweshwa!. Samahani!

3. Samahani Kuitetea serikali kuwa imekamilisha kazi kwa kusema siyo sumu wakati kiukweli halisi Dr. Mwakiembe amedhurika kwa sumu, ila siyo ya kulishwa ili adhurike bali ni madhara ya sumu iliyomo mwilini mwake na hatimaye kumdhuru. Swali la hiyo sumu iliingiaje bila kulishwa sumu, jibu litapatikana mtakapo elezwa anaumwa nini, alianza lini kuumwa hicho anachoumwa, alitumia madawa gani na kwa muda gani, matumizi ya madawa hayo yana athari gani kwa mtumiaji. Hivyo utetezi wa serikali kuwa Mwakiyembe hajalishwa sumu utapatikana kwa taarifa ya kitabibu na sio kwa mimi kuitetea serikali bali kwa wote kuubaini ukweli ulioa wazi. Samahani!
 
Ni kweli luga ya marikia inanisumbua sana na hasuwa glama ya kingeleza. Asavali kiswahili nakiwezea vizuli na ndiyo luga yetu sisi watu wa uswazi sio kama nyie watoto wa magolofani!.
Ndugu yangu Pasco, kama unajua kuwa lugha ya wageni inakupa shida kimawasiliano kwanini unaing'ang'ania? Kwanza unapowasiliana na sisi wamatumbi wenzio unahaja gani kuchanganya lugha?
 
Mwakyembe mwenyewe alikiri 2wks ago kuwa ni kweli alilishwa sumu, na sumu hiyo sasa imeanza kumdhuru mkewe, sasa Manumba hana maana hapa. Ukizingatia anafaanya ndani ya serikali ya ccm hata kama ni ukweli lazima watakataa tu. Hata kama watakanusha wenye akili tunajua hatuna haja ya Kubishana.
 
Sisi hatusema kitu tunamwachia Mungu, yaan kakaetu anapigwa danadana like nini.
Amna noma every one will die!
 
Haya majibu rahisi huwa yanaendelea kuacha maswali.Hivi watawala wataendelea kutupa majibu rahisi hata lini?
Kama anashindwa kujua chanzo ni heri asingetoa ripoti hii.
 
Apo ni utata, wote ni members wa Executive lakini wana opinion tofauti. Cha ajabu mmoja anasema ni sumu halafu mwingine anapinga bila kusema tatizo ni nini?
 
How much are you paid for being a VUVUZELA?
Mkuu Bulesi, kiukweli nalipwa hela nyingi sana!. Zile bahasha za khaki nalipwa 20,000 kila bahasha hivyo kwa wiki ninamake some good 100,000 per week, kwa mwezi ninamake 400,000 nikifanya kazi na Jumamosi na Jumapili zinafika 500,000 kwa mwezi!. This is a lot of money kwa mwandishi wa habari freelance!. Haswa ukizingatia media za Tanzania zinawalipa freelance 2,500-5,000 per story na 5,000-10,000 kwa makala!.

Malipo hayo ni nje ya malipo ninayolipwa kuposti humu jf, nikijumlisha malipo yote kabisa, natengeneza kama Laki 600,000 kwa mwezi, its a lot of money!. I'm rich!. Ndio maana hata usafiri nimebadili, nilikuwa natumia pikipiki, sasa natumia bajaj!.
 
Back
Top Bottom