Tukimtaka Sitta ajiuzuru kwa uzushi tutakuwa tunamwonea, uzushi walianza akina Pinda na Makinda katika posho, tungeanza kuwataka wao wajiuzuru kwanza.
Pia uchunguzi anaousema Manumba kuwa ameufanya kwa umakini mkubwa kimsingi ni kusuma report ya MaDK toka India, hivi kusoma taarifa ndio uchunguzi???Hiyo report aliisoma kwa kutumia Darubini??huyu mzee anaongea nini???walisoma wapi hawa watu mbona wanajifanya MABOGUS???
Ni uchunguzi gan huo wa afya ya mtu unaomalizwa bila kuhusisha analysis ya body samples???kwanini wasingechukua body samples wakapime na waje na majibu ya kueleweka???Kwanini wasilete wataalum wakafanya uchunguzi huru wa afya ya Mwakyembe kama ilivyokatika Auditing?? Kimsingi katika sakata la Mwakyembe kulishwa sumu, Serikali ndiyo inayotuhumiwa, inawezekanaje mtuhumiwa akafanya uchunguzi dhidi yake na uchunguzi huo ukawa na majibu ya kueleweka?????Hawa wanatuona watanzania ni mazezeta kama wao walivyo.
Wafanye uchunguzi wa nini wakati majibu ya Apolo yanasema hakuna sumu?