DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,152
Kwa muda mrefu kumekuwepo taarifa kwamba baadhi ya viongozi wa serikali huwekewa sumu (poison) kwenye vyakula na vinywaji vyao. Ingawa mara nyingine huonekana kama tetesi, ukweli ni kwamba vitendo hivi vimewahi kuripotiwa hata kwa viongozi wakubwa duniani. Mfano ni kiongozi wa Palestina Yasser Arafat aliyefariki mwaka 2004 akidaiwa kuwekewa sumu, Alexei Navalny wa Urusi aliyewahi kushambuliwa kwa sumu mwaka 2020, na rais wa zamani wa Ukraine Viktor Yushchenko aliyenusurika baada ya tukio la aina hiyo mwaka 2004.
Hali kama hiyo pia imeripotiwa nchini Tanzania, hasa katika vipindi vya kisiasa na uchaguzi. Baadhi ya viongozi wamedai kuwekewa sumu lakini wakabaki hai baada ya kupata matibabu kwa siri, kisha baadaye umma ukaja kusikia ukweli. Miongoni mwa waliowahi kutaja tukio kama hilo ni:
Pia Soma:

- Mzee Philip Mangula, aliyedai kuwekewa sumu mwaka 2020 baada ya kufanyiwa vipimo vya kitabibu.
- Hayati Dk. John Pombe Magufuli, ambaye alipokuwa Naibu Waziri aliwahi kusema hadharani kuwa aliwekewa sumu.
- Paul Makonda, aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Arusha, naye amedai aliwekewa sumu mwaka jana.
- Kwa nini wale wanaodaiwa kuhusika na vitendo hivi hawakamatwi wala kufikishwa kwenye vyombo vya sheria?
- Je, ni kwa sababu ushahidi wa kutosha haupatikani?
- Au ni kwa sababu kuna mkono wa siri wenye nguvu za kisiasa unaolinda wahusika?
- Nia kuu ya kuwadhuru viongozi kwa sumu ni ipi – ni ushindani wa kisiasa, kulinda maslahi binafsi, au njama za kupora madaraka?
Pia Soma: