Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,172
- 128,875
Huyu DCI ni muongo, leo rais Magufuli katuthibitishia kuwa Mwakyembe alitiliwa sumu.Hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari mchana wa leo. Katika maelezo yake, DCI anasema kwamba:
"Kutokana na uchunguzi wa kipolisi ulioshirikisha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hakuna ushahidi juu ya hilo".
Alipoulizwa na waandishi wa habari:
Je, Dr. Mwakyembe anasumbuliwa na maradhi gani?
DCI alijibu kwamba:
"Kazi ya Jeshi la Polisi sio kuchunguza maradhi bali kuchunguza tuhuma, na baada ya uchunguzi wake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi limebaini kwamba tuhuma kwamba Dr. Mwakyembe amelishwa sumu hazina ukweli."
Akiwa Kyela rais Magufuli amethibitisha Dr. Mwakyembe alitiliwa sumu. Tangu kuibuka kwa kadhia ya sumu ya Mwakyembe, hii ndio kauli from the highest authorities kuwa Mwakyembe alitiliwa sumu. Kutiliwa sumu ni criminal offence ya attempted murder, kama rais anathibitisha Waziri wake alitiliwa sumu na wahusika anawajua na hakuna sio aliyekamatwa, bali aliyehojiwa!, what are the chances kwa wasiojulikana wa Shambulio la Lissu ambao hawajulikani kabisa?.Mkuu Mchambuzi, nimependa unavyochambua, ki ukweli unazama deep!.
Nimeupitia uchambuzi wako kuna kitu sijakiona ukikizungumza kuhusu sumu.
Kuna sumu za aina tatu,
1. Intentions or delibarate poisoning, hii ndio ile dhana ya mtu kulishwa sumu, kutiliwa, kushikishwa au hata kutumiwa kwa barua kama 'anthrax', hii ni mtu kupewa sumu be it first poisoning or slow poisoning ila mwisho wa siku mhusika hudhurika!.
2. Food poisoning, hii ni aina ya pili ya sumu ambayo hutokana na kula chakula chenye sumu, mfano kuna baadhi ya mihogo ina sumu, uyoga, na baadhi vya vyakula vya proteion in nature kama nyama, samaki, maziwa, mayai etc ambapo aliyekula vinamdhuru ama instantly kwa kupata rushes, kuwashwa au kupata mafindofindo wanaita 'alergy' au slow reaction ambapo inaibuka baada ya kipindi kirefu na ineweza kuibuka kama kansa etc!.
3. Medical Reaction, japo sumu zote ni chemical reaction, hii sumu ya medical reaction ni sumu inayotokana na reaction ya madawa fulani fulani kwenye mwili wa binadamu mostly kutokana na prolonged use!. Hii humpata mtu ambaye kuna kitu ameugua na ni ugonjwa wa muda mrefu, mtu huyo anakuwa anatumia combination ya madawa fulani kwa muda mrefu imefikia muda madawa hayo yamereact from each other na kugeuka sumu na wakati huo huo mwili unakuwa umetengeza 'antigen' za kukabiliana na hiyo reaction na matokeo huwa ndiyo kama hiyo hali ya Mwakiyembe!.
Wanabodi nilishauri huko nyuma na hapa nashauri tena, tupunguze conspiracy theories tusubiri tamko la Mwakiyembe mwenyewe!.
Japo naye ili kumlindia Sitta heshima, anaweza kusema "Nimesha Muachia Mungu, hivyo naomba nisizungumze chochote"! hivyo kutosema anaumwa nini!.
Hivi katika hili sakata la sumu ya Mwakyembe, iliwahi kuthibitishwa na authorities zozote kuwa ni kweli Mwakyembe alitiliwa sumu, au uthibitisho ndio huu wa leo wa rais Magufuli?.
P.