Mwanakili90
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,568
- 246
Hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari mchana wa leo. Katika maelezo yake, DCI anasema kwamba:
"Kutokana na uchunguzi wa kipolisi ulioshirikisha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hakuna ushahidi juu ya hilo".
Alipoulizwa na waandishi wa habari:
Je, Dr. Mwakyembe anasumbuliwa na maradhi gani?
DCI alijibu kwamba:
"Kazi ya Jeshi la Polisi sio kuchunguza maradhi bali kuchunguza tuhuma, na baada ya uchunguzi wake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi limebaini kwamba tuhuma kwamba Dr. Mwakyembe amelishwa sumu hazina ukweli."
Kwa watu waliotazama taarifa ya habari ya saa mbili usiku atakubaliana na mimi ya kuwa DCI Ametoa taarifa za uongo.
Kwanza alipoanza kuzungumzia swala la Dr . Mwakyembe hata SURA yake ilibadilika, ilidhahirisha machungu ambayo moyo wake ulikuwa unayapata hasa anapotoa maneno yale kwa taifa.(hapa inaonesha wazi alikuwa anasema kitu ambacho hata yeye anajua anapindua agano kwa kuzungumza uongo)
Wataalamu wa saikologia wanaweza kututolea ufafanuzi jinsi DCI Alivyokuwa na fake face,kuhusiana na Ugonjwa wa DR mwakyembe.