DCI Manumba: Mwakyembe hajalishwa sumu!

DCI Manumba: Mwakyembe hajalishwa sumu!

Siungani na Sitta kuwa Mwakyembe alikuwa poisoned lakini pia siwezi kumpinga kwa ushahidi wa Manumba!Yapo maswali ya kujiuliza juu ya jeshi la polisi vs Mwakyembe kabla ya kuafiki alichokisema Manumba. 1.Report ya awali ya police juu ya ajali aliyopata Mwakyembe Iringa ilieza kuwa maelezo ya Mwakyembe juu ya mazingira ya ajali yalikuwa ya uongo kwa kuwa alikuwa amesinzia wakati wa ajali(ikumbukwe kuwa ndani ya gari alikuwemo yeye na dereva tu).Alipohoji namna walivyojua kuwa alikuwa amesinzia,IGP albatilisha report ile;Je,wameshatoa report nyingine? 2.Aliandika waraka mrefu kwa IGP akiliomba jeshi la polisi lichunguze alichokiita njama za kuuawa kwake,watuhumiwa ktk waraka huo ni:Jeshi la polisi,Fred Lowasa(mtoto wa Edward Lowasa) na CASPIAN(kampuni ya Rostam Aziz). Kama kazi ya polisi ni kuchunguza tuhuma kama alivyosema Manumba,uchunguzi wao ulibaini nini? 3.Kama kweli Sitta amelidanganya taifa ni hatua gani za kisheria zinapaswa kuchukuliwa dhidi yake?Ninamuomba MUNGU Sitta awajibishwe tuujue ukweli wote.
 
Hivi serikali hii yenye viongozi ambao kila dakika midomo yao inasema uongo ni hadi lini?? Someni hata alama za nyakati basi!!!!!!!!
 
Hakuna cha sumu wala pilipili, huyo mgonjwa tu. Tena hata kichwa kina matatizo si ngozi tu.

Mwenye ushahidi wa sumu auweke hapa.
 
Mkuu mchambuzi ingekuwa vizuri kama ungeeleza zaidi kuhusu habari hii. Ukiangalia kwa undani unaweza kuona kuwa hizo kauli mbili ni kama hazijatolewa na DCI, ya kwanza inasema hakuna ushahidi kuwa amelishwa sumu, ya pili inasema jeshi halikuchunguza maradhi. Tuhuma ni kuwa Mwakyembe kalishwa sumu, so implied meaning ni kuwa anasema hajalishwa ila amejilisha, au anasema kuwa Mwakyembe hana tatizo la sumu. So Wizara ya afya inachunguza vipi shutuma? Ukiangalia hizi kauli unaona wazi kabisa mtu anayezisema hawezi kuwa DCI wa Tanzania.

Jeshi letu la Polisi au CID ina maabara na wanasayansi wanaoweza kuchunguza sumu za radiation? hapa Tanzania sumu ya panya yenyewe kuchunguza ni vigumu. Kuna Toxologists wangapi wanaoweza kufanya kazi na tukaamini kuwa wanafanya kazi kweli na tukapewa majibu kweli? au ndio yale yale ya kesi ya nyani kwa ngedere.

Kwa mtazamo wangu ambao unaweza kuwa finyu, ili kubaini kauli ya Manumba ina background gani, ni vizuri tukaangalia sequence of events pamoja na kauli mbalimbali kama ifuatavyo:

· Rais Kikwete katikati ya mwaka 2011 alitamka kwa masikitiko kwenye TV kwamba – "hali ndani ya CCM imefikia hatua mbaya kiasi kwamba watu hawa aminiani tena, na hauwezi kuacha glasi yako ya maji ovyo ovyo…."

· Baada muda mrefu kufuatia kauli hii ya Rais, Mwakyembe akabainika anasumbuliwa na ugonjwa wa ajabu wa ngozi. Mwakyembe akaenda India lakini bila ya kutoa tamko lolote kuhusu kunyweshwa sumu.

· Wakati Mwakyembe akiwa India, miezi kadhaa, Sitta katika kipindi cha Dakika 45 kwenye ITV akatamka kwamba amemuona Dr. Mwakyembe kabla hajaenda India kuchunguzwa afya yake, na dhahiri Dr. Mwakyembe "amelishwa sumu", kwani mwili wake umebadilika ghafla, unaota magamba, nywele mwilini zina momonyoka, na ngozi inapukutika kama unga….; Hili likawa tamko la kwanza la kiongozi wa serikali kwamba Dr. Mwakyembe amelishwa sumu. Lakini bado mwathirika mwenyewe (mwakyembea) alikuwa hajatoa tamko lake la kuhusisha maradhi yake na sumu.

· Mwakyembe akarudi kutoka India, na kusema kwamba anamshukuru Mungu amepona, na kwamba taarifa juu ya ugonjwa wake zimepelekwa serikalini. Lakini bado hakutamka lolote kuhusu sumu.

· Wiki kadhaa zilizopita, wakiwa pamoja katika ibada moja Viwanja vya Tanganyika Packers, Sitta akatangaza mbele ya umati kwamba Mwakyembe amelishwa sumu, na kwamba madaktari india wamesema ni bahati sumu haikwenda kwenye moyo, figo wala maini, bali ilitoka nje, ndio maana ngozi yake ikapata madhara husika. Sitta akasema pia kwamba Serikali ina taarifa zote juu ya hili na kama inataka kupingana nae, basi ielezee umma nini kimemsibu Dr. Mwakyembe. Kwa upande wake, Dr. Mwakyembe katika ibada ile, hakusema lolote kuhusu kulishwa sumu, zaidi ya kushukuru kwamba sasa amepona, Mungu atalipa, na kuomba wahumini wamwombee pia Professor Mwandosya na yeye apone.

· Baada ya tamko la Sitta kuhusu Mwakyembe kulishwa sumu, na kwamba serikali ina taarifa, Waziri Nahodha akakanusha madai ya Sitta – kwamba Wizara yake haina taarifa hizo. Nadhani Nahodha alikuwa sahihi kwa sababu maneno ya Sitta ni kwamba Serikali ina taarifa kwamba "Mwakyembe amelishwa sumu."; hii ni tofauti na kusema "serikali ina taarifa kwamba ugonjwa/maradhi yanayomsumbua Dr. Mwakyembe yanatokana na kuwa in contact na sumu kwa namna moja au nyingine. Binafsi, sidhani ripoti kutoka India inasema ‘Mwakyembe amelishwa sumu", ingawa lazima inasema ugonjwa wake umetokana na sumu.

· Lakini Sitta akapingana na Nahodha na kusema kwamba taarifa kuhusu kulishwa sumu kwa Dr. Mwakyembe tayari zipo mikononi mwa polisi siku nyingi. Mpaka hapo, bado Dr. Mwakyembe alikuwa hajatoa tamko lake kuhusu kulishwa kwake sumu.

· Pia ni muhimu kusema hapa kwamba – Waziri Mkuu Pinda na Katibu Mkuu Afya Blandina Nyoni, katika nyakati tofauti waliweka bayana kwamba serikali haiwezi kutoa maelezo kuhusu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe kwani ni ‘unethical', hivyo ni wajibu wa mgonjwa mwenyewe. Bado Dr. Mwakyembe hakakaa kimya.

· Leo, DCI Manumba akatoa taarifa ambazo sote sasa tunazifahamu. Kwa kauli ya Manumba, upelelezi wa kipolisi ulilenga kuchunguza maneno kwamba "amelishwa sumu", sio vinginevyo. Kama taarifa za uchunguzi wa madaktari wa India hazijatumia maneno "Mwakyembe amelishwa sumu", Maelezo ya DCI Manumba yanasimama kuwa sahihi kwani kwa maana hii basi, walichofanya DCI ni kuchanganya taarifa walizopokea kutoka vyanzo tofauti juu ya tuhuma kwamba mwakyembe "amelishwa sumu", pamoja na taarifa zilizopo Wizara ya Afya, kutoka India. Na huu ndio msingi wa Manumba kutamka kwamba, kazi ya Polisi ni kuchunguza tuhuma, sio maradhi, na yupo sahihi katika hilo.

My assumption:
DCI alikuwa na taarifa kutoka chanzo kingine zinazosema "Mwakyembe amelishwa sumu", hivyo DCI alifanya uchunguzi kuhusu "kulishwa sumu", na sio vinginevyo. Na baada ya DCI kufanya uchunguzi uliotokana na ushirikiano wa karibu na Wizara ya Afya, DCI amebaini kwamba taarifa za "kulishwa sumu", hazilingani na maneno yaliyopo kwenye faili lililopo Wizara ya Afya. Inawezekana kabisa Madaktari India wameweka wazi kwamba tatizo ni uwepo wa sumu mwilini, lakini hawajatumia neno "amelishwa sumu", na ndio maana alichokichunguza Manumba ni "TUHUMA" kwamba "Mwakyembe amelishwa sumu", SIO taarifa au tuhuma kwamba "Mwakyembe amenusishwa sumu, amepuliziwa sumu, kanawia maji au sabuni yenye sumu, amepata contact na sumu kutokana na mkono wa mtu n.k. Ni hali hii ndio inanipelekea kuamini kwamba Manumba amefanya kazi yake kwa usahihi kabisa, hivyo tusipoteze muda kuhoji kauli yake.

Ni dhahiri kwamba Dr. Mwakyembe ana tatizo lisilo la kawaida, na uwezekano mkubwa ni kwamba maradhi yale yanatokana na sumu. Natumia neno ‘uwezekano mkubwa', kwani bado Mwakyembe hajatueleza. Kwa mtazamo wangu, Sitta ni dhahiri hajazungumza bila ya ruksa ya Mwakyembe, lakini kama walitaka kufikisha ujumbe waliokusudia, basi Sitta angejaribu kuwa na busara kidogo na kukwepa kutoa tafsiri yake juu taarifa za madktari wa india, mfano kuepuka kutumia maneno "amelishwa sumu", na badala yake kutumia maneno kama vile, Dr. Mwakyembe "anasumbuliwa na maradhi yatokanayo na sumu kuingia mwilini"; au Maradhi ya Dr. Mwakyembe "yanatokana na sumu na kuna mkono wa mtu katika hilo " au, Dr. Mwakyembe alishatoa taarifa nyingi kwa polisi kwamba anatishiwa maisha yake lakini hakuna lililofanyika, na sasa imefikia hatua ya kuugua kutokana na sumu kumwingia mwilini…., hivyo ni wasaa sasa wa Serikali kutoa tamko lake kwa kufuatana na taarifa iliyo ipokea kutoka kwa madaktari wa India.

Maswali muhimu ya kujiuliza ni je:

1. Je, taarifa za uchunguzi wa madaktari kutoka India, ambazo zipo Wizara ya Afya, zimetumia neno "amelishwa sumu" au zimetamka tu kwamba "alipata contact na sumu?"

2. Je, alichokana Waziri Nahodha ni maneno ya Sitta kwamba "Mwakyembe amelishwa sumu", kwa maana ya kwamba taarifa kutoka india hazijatumia maneno hayo ingawa zinaelezea maradhi yatokanayo na sumu kuingia mwilini?

3. Je, taarifa zilizopo Wizara ya Afya ni zile zile ambazo Sitta anasema kwamba Polisi tayari wanazo? au Sitta na Mwakyembe walipeleka Polisi taarifa za ziada?

4. Je, katika uchunguzi wao, DCI (Polisi) wametumia taarifa zilizopo Wizara ya Afya ambazo hadi sasa hatujui kama zimetumia maneno ‘Mwakyembe amelishwa sumu? au Polisi (DCI) wametumia taarifa nyingine walizopokea zenye maneno "Mwakyembe amelishwa sumu, na kisha kutumia tuhuma hizi kwenda Wizara ya Afya kuangalia faili kutoka India lina maelezo ya namna gani"?

5. Na je, kutokana na Wizara ya Afya kutoa ushirikiano na DCI, hivyo kupelekea taarifa ya DCI kwamba hakuna ushahidi Mwakyembe "amelishwa sumu", je ni sahihi kutafsiri kwamba, matokeo ya uchunguzi wa DCI ambayo yamefanikiwa kutokana na ushirikiano wa Wizara ya Afya ambayo moja kwa moja ni Serikali Kuu, je ina maana kwamba sasa huu pia ndio msimamo/majibu/maelezo rasmi ya serikali kuhusu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe? Tusisahau Waziri Mkuu alishasema serikali haitatoa maelezo kuhusu nini kinamsibu Dr. Mwakyembe kwani ni unethical, hiyo kazi ni ya mgonjwa mwenyewe.

Mwisho, Mwakyembe ni mwanasheria, hivyo kukaa kwake kimya ni sawa na ‘ukimuona kobe kainama, ujue anatunga sheria'. Hivyo tuwe na subira, akiwa tayari ameshazingatia legal implications, lazima atatamka tu sasa rasmi kama ‘mwathirika wa sumu'.

Vinginevyo, iwapo sasahivi Serikali inashindwa kutoa taarifa kuhusu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe, ikitokea bahati mbaya (mungu pishilia mbali) kwamba Dr. Mwakyembe anafariki, je, serikali itatoa taarifa juu ya kufariki kwa kiongozi wake? Itasema marehemu alikuwa anaugua nini?
 
Secret of the dead- huyo aliyepanga mauaji hayo anashangaa kwanini huyu mtu amechukua muda mrefu kufa. by the time alipomtembelea kabla hajaenda India alijua hatafika huko India kabla ya kukata roho. God have mercy, Mwakyembe still breathing.
Viongozi hawa wachawi wamedhulumu maendeleo ya nchi na hatimaye wanadhulumu roho za watu wenye uadilifu na nchi hii. Watanzania ni kwanini matatizo ya Mwakyembe yanakuwa siyo yetu, au mpaka pale yatakapokufika ndio unajua viongozi hawa ni hatari kwa nchi hii tunayoipenda! nation stand up! kuna vifo vingi vya kupangwa na watawala vimetokea kipindi hiki cha katika miaka michache iliyopita lakini cha kushangaza ukweli hauwekwi wazi....sasa ndipo unapojua kuwa tumekalia kuti kavu ni mhimu kuishi kwa hadhari kali baada ya viongozi waliokuwa wezi kuwa ndio wanaendesha nchi hii. lakini haya yote yana mwisho.
 
Labda tuangalie tena maneno ya DCI kama yalivyoandikwa na magazeti tofauti:

"Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu katika maradhi yanayomsibu Mwakyembe." Gazeti la Mwananchi likirudia maneno ya DCI.

"Tulipewa ripoti ya kitabibu kutoka India alikotibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na ilitupatia ripoti na kuonyesha kuwa ugonjwa wake hautokani na sumu," aliongeza DCI. Gazti la Mtanzania Daima.

Magazeti yote mawili hayaongelei tu kwamba hakunyweshwa sumu bali ugonjwa wake hautokani na sumu.

Sasa mpira umerudishwa kwa Dr. Mwakyembe, kama hakubaliani na hiyo statement ya polisi basi atoe ukweli wake.
 
Hebu ngojeni; hivi nyi Mwakyembe mnamjua au mnamsikia tu?! Mwakyembe si mtu wa kusemewa na wana-JF wala huyo Sitta! Mwakyembe ni mwanasheria aliyekomaa, jasiri na asiyeogopa chochote kwa kile anachoona ni haki! Wakari Mkapa anauza NMB, Mwakyembe alikuwa ni mjumbe wa bodi na kv hakutaka kuhusika kwenye dhambi ile, Mwakyembe alichukua uamuzi wa kujiudhuru kama ambavyo alifanya CEO wa wakati wakati ule. Mwakyembe ni mpiganaji awezae kupigana mwenyewe bila ya kuhitaji msaada wowote! Endapo angelishwa sumu; Mwakyembe asingeogopa kusema ukweli!!! Kwa ujasiri alionao Mweakyembe; nitashangaa kwanini asifungue mashitaka dhidi ya washukiwa!!! By the way; hivi nyie watu mwaijua sumu au mwafanya mchezo?! Kwa upako gani alionao Mwakyembe hata sumu ishindwe kumwondoa?! Kama ambavyo wadau wanasema walitarajia kauli hii toka kwa jeshi la polisi; hiki ndicho hasa alichokuwa anakitaka Sitta! Kwamba, auaminishe umma kwamba Mwakyembe amelishwa sumu; ili hata pale itakapotolewa ripoti rasmi kwamba hakulishwa sumu, basi watu waamini kwamba ripoti hiyo imechakachuliwa kwavile tayari walishajengwa kisaikolojia kwamba alilishwa sumu!! By the way, kama issue ni Richmond; Mwakyembe alikuwa Mwenyeketi tu wa ile kamati na kama kuna watu ambao wamekuwa wakipiga kelele sana kuhusu Richmond, Mwakyembe si mmoja wao! Role ya Mwakyembe kwenye suala la Richmond iliisha pale aliposoma ripoti ile bungeni na siku chache baadae tena pale alipolazimika kufanya hivyo. Hata hivyo, bado kulikuwa na watu ambao waliendelea kuishupalia zaidi issue ya Richmond kuliko huyo Mwakyembe! Ole Sendeka, Anne Killango, Samuel Sitta (ingawaje huyu alikua anazumgumzia kimaslahi yake zaidi), Zitto na Mnyika ndio watu ambao naweza kusema hakuacha issue ile itulie na wala sio Mwakyembe! Ni kweli, Mwakyembe ndie alikuwa Mwenyekiti, lakini mwiba uliokwama shingoni mwa wana-Richmond ni ule uliotokana na wapiganaji kutotaka kuiacha issue hiyo iishe hivi hivi....!!! So, WHY MWAKYEMBE?! Hapa hakuna cha sumu wala nini, na kama ni sumu wala si ya kwamba kuna mtu alitaka kumwua....!!!!!

Pamoja na hayo, shime kwa Rais Kikwete.....juzi kwenye salamu zangu za Valentine nilikueleza kuhusu ni namna gani viongozi wa serikali yako wanavyotoa kauli tata kiasi naweza ku-conclude kwamba ni WAONGO, WAZUSHI, WAFITINI......List yangu iliwataja tu Anna Makinda, Mizengo Pinda, Salva Rweymamu bila kukusahau wewe mwenyewe. Kwamba, angalau mmoja katika listi hiyo atakuwa ni mwongo mkubwa na mzushi. List hiyo sasa imeongozeka....Ama Samuel Sitta au DCI Manumba, lazima mmoja wapo hapo atakuwa ni mzushi na mwongo wa kutupwa!!! NI hatari kuwa na watendaji wakuu ambao ni waongo na wazushi wasio na mfano. Katika list hiyo, ni lazima angalau mmoja awajibike ama kuwajibishwa kutokana na dhambi ya ya uongo na uzushi wa kupitiliza.

Hapo haupingiki hata kidogo, hakuna mwana siasa katika dunia hii ambae ni mkweli 100%
 
Labda tuangalie tena maneno ya DCI kama yalivyoandikwa na magazeti tofauti:

"Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu katika maradhi yanayomsibu Mwakyembe." Gazeti la Mwananchi likirudia maneno ya DCI.

"Tulipewa ripoti ya kitabibu kutoka India alikotibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na ilitupatia ripoti na kuonyesha kuwa ugonjwa wake hautokani na sumu," aliongeza DCI. Gazti la Mtanzania Daima.

Magazeti yote mawili hayaongelei tu kwamba hakunyweshwa sumu bali ugonjwa wake hautokani na sumu.

Sasa mpira umerudishwa kwa Dr. Mwakyembe, kama hakubaliani na hiyo statement ya polisi basi atoe ukweli wake.

Kwa mujibu wa Tanzania Daima kama ulivyoonesha hapo juu, inabidi Mwakyembe awapinge Manumba, Tanzania Daima, Apollo.

Itabidi Mwakyembe aje na ripoti ambayo ni tofauti na anayoongelea Manumba na Tanzania Daima.

Conclusion: Sitta muongo mpaka sasa hivi kwani yeye nilimsikia akitangaza Mwakyembe kalisha sumu, tena ilikuwa kanisani kama sikosei, Mwakyembe mwenyewe hakusema hayo. Tumsubiri Mwakyembe atasemaje maana yeye ninavyosikia ni mwanasheria aliyebobea labda alikuwa anangoja statement ya uchunguzi.
 
Bado taarifa ya police imeongeza maswali mengi sana.

Uchunguzi wa Apollo uliishia tu kujua kama alilishwa sumu au hakulishwa?.

Baada ya kugundua kuwa hakulishwa sumu police waliona hakuna haja ya kujua anaumwa ugonjwa gani?

Kama mtu yuko hai tu bado tunapata chunguzi zenye utata kama hii, je Mwakyembe angekuwa amekufa kungetokea uchunguzi wowote. Nina imani wengi wamekwenda na maji kwa mtindo huu.
 
Kama kuna TISS wa Upson na TISS Othman tutarajie nini?. Dalili yake moja ni hii ya idara inayopanga kumuua mtu ndio idara hiyohiyo inayofichua siri kwa mtuhumiwa. Haya mambo hayakuwepo siku za nyuma, watu walikuwa wanapotea kimyakimya. Ni muda mrefu police walishatuhumiwa na Mwakyembe kuwamo katika mpango wa kumuuwa, kwa misingi hiyo wala hawakupaswa kutoa hiyo taarifa kwani toka mwanzo kwenye sakata la Mwakyembe walishaonekana ni watuhumiwa wakuu. Nchi ikishaanza kutawaliwa na Mafia kamwe haki haiwezi patikana. Watu wanaugusa maslani ya mafia watakufa sana kwa sumu.
Ushauri wangu kwa Mwakyembe ni kuwa aache siasa. Kwa siasa zako za kutetea wanyonge na kuquestion mambo yenye maslahi kwa mafioso utakufa mapema sana. Wenzako akina Kubenea wamerudi kwenye mstari, Zitto karudishwa kwenye mstari. Kuwa makini na ngoma unayocheza. Ngoma inayokufanya kuwa mbele ya mstari huku huangalii nyuma kuna nani wako upande wako itakuuwa.
 
Kwa mtazamo wangu ambao unaweza kuwa finyu, ili kubaini kauli ya Manumba ina background gani, ni vizuri tukaangalia sequence of events pamoja na kauli mbalimbali kama ifuatavyo:

· Rais Kikwete katikati ya mwaka 2011 alitamka kwa masikitiko kwenye TV kwamba – “hali ndani ya CCM imefikia hatua mbaya kiasi kwamba watu hawa aminiani tena, na hauwezi kuacha glasi yako ya maji ovyo ovyo….”

· Baada muda mrefu kufuatia kauli hii ya Rais, Mwakyembe akabainika anasumbuliwa na ugonjwa wa ajabu wa ngozi. Mwakyembe akaenda India lakini bila ya kutoa tamko lolote kuhusu kunyweshwa sumu.

· Wakati Mwakyembe akiwa India, miezi kadhaa, Sitta katika kipindi cha Dakika 45 kwenye ITV akatamka kwamba amemuona Dr. Mwakyembe kabla hajaenda India kuchunguzwa afya yake, na dhahiri Dr. Mwakyembe “amelishwa sumu”, kwani mwili wake umebadilika ghafla, unaota magamba, nywele mwilini zina momonyoka, na ngozi inapukutika kama unga….; Hili likawa tamko la kwanza la kiongozi wa serikali kwamba Dr. Mwakyembe amelishwa sumu. Lakini bado mwathirika mwenyewe (mwakyembea) alikuwa hajatoa tamko lake la kuhusisha maradhi yake na sumu.

· Mwakyembe akarudi kutoka India, na kusema kwamba anamshukuru Mungu amepona, na kwamba taarifa juu ya ugonjwa wake zimepelekwa serikalini. Lakini bado hakutamka lolote kuhusu sumu.

· Wiki kadhaa zilizopita, wakiwa pamoja katika ibada moja Viwanja vya Tanganyika Packers, Sitta akatangaza mbele ya umati kwamba Mwakyembe amelishwa sumu, na kwamba madaktari india wamesema ni bahati sumu haikwenda kwenye moyo, figo wala maini, bali ilitoka nje, ndio maana ngozi yake ikapata madhara husika. Sitta akasema pia kwamba Serikali ina taarifa zote juu ya hili na kama inataka kupingana nae, basi ielezee umma nini kimemsibu Dr. Mwakyembe. Kwa upande wake, Dr. Mwakyembe katika ibada ile, hakusema lolote kuhusu kulishwa sumu, zaidi ya kushukuru kwamba sasa amepona, Mungu atalipa, na kuomba wahumini wamwombee pia Professor Mwandosya na yeye apone.

· Baada ya tamko la Sitta kuhusu Mwakyembe kulishwa sumu, na kwamba serikali ina taarifa, Waziri Nahodha akakanusha madai ya Sitta – kwamba Wizara yake haina taarifa hizo. Nadhani Nahodha alikuwa sahihi kwa sababu maneno ya Sitta ni kwamba Serikali ina taarifa kwamba “Mwakyembe amelishwa sumu.”; hii ni tofauti na kusema “serikali ina taarifa kwamba ugonjwa/maradhi yanayomsumbua Dr. Mwakyembe yanatokana na kuwa in contact na sumu kwa namna moja au nyingine. Binafsi, sidhani ripoti kutoka India inasema ‘Mwakyembe amelishwa sumu”, ingawa lazima inasema ugonjwa wake umetokana na sumu.

· Lakini Sitta akapingana na Nahodha na kusema kwamba taarifa kuhusu kulishwa sumu kwa Dr. Mwakyembe tayari zipo mikononi mwa polisi siku nyingi. Mpaka hapo, bado Dr. Mwakyembe alikuwa hajatoa tamko lake kuhusu kulishwa kwake sumu.

· Pia ni muhimu kusema hapa kwamba – Waziri Mkuu Pinda na Katibu Mkuu Afya Blandina Nyoni, katika nyakati tofauti waliweka bayana kwamba serikali haiwezi kutoa maelezo kuhusu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe kwani ni ‘unethical’, hivyo ni wajibu wa mgonjwa mwenyewe. Bado Dr. Mwakyembe hakakaa kimya.

· Leo, DCI Manumba akatoa taarifa ambazo sote sasa tunazifahamu. Kwa kauli ya Manumba, upelelezi wa kipolisi ulilenga kuchunguza maneno kwamba “amelishwa sumu”, sio vinginevyo. Kama taarifa za uchunguzi wa madaktari wa India hazijatumia maneno “Mwakyembe amelishwa sumu”, Maelezo ya DCI Manumba yanasimama kuwa sahihi kwani kwa maana hii basi, walichofanya DCI ni kuchanganya taarifa walizopokea kutoka vyanzo tofauti juu ya tuhuma kwamba mwakyembe “amelishwa sumu”, pamoja na taarifa zilizopo Wizara ya Afya, kutoka India. Na huu ndio msingi wa Manumba kutamka kwamba, kazi ya Polisi ni kuchunguza tuhuma, sio maradhi, na yupo sahihi katika hilo.

My assumption:
DCI alikuwa na taarifa kutoka chanzo kingine zinazosema “Mwakyembe amelishwa sumu”, hivyo DCI alifanya uchunguzi kuhusu “kulishwa sumu”, na sio vinginevyo. Na baada ya DCI kufanya uchunguzi uliotokana na ushirikiano wa karibu na Wizara ya Afya, DCI amebaini kwamba taarifa za “kulishwa sumu”, hazilingani na maneno yaliyopo kwenye faili lililopo Wizara ya Afya. Inawezekana kabisa Madaktari India wameweka wazi kwamba tatizo ni uwepo wa sumu mwilini, lakini hawajatumia neno “amelishwa sumu”, na ndio maana alichokichunguza Manumba ni “TUHUMA” kwamba “Mwakyembe amelishwa sumu”, SIO taarifa au tuhuma kwamba “Mwakyembe amenusishwa sumu, amepuliziwa sumu, kanawia maji au sabuni yenye sumu, amepata contact na sumu kutokana na mkono wa mtu n.k. Ni hali hii ndio inanipelekea kuamini kwamba Manumba amefanya kazi yake kwa usahihi kabisa, hivyo tusipoteze muda kuhoji kauli yake.

Ni dhahiri kwamba Dr. Mwakyembe ana tatizo lisilo la kawaida, na uwezekano mkubwa ni kwamba maradhi yale yanatokana na sumu. Natumia neno ‘uwezekano mkubwa’, kwani bado Mwakyembe hajatueleza. Kwa mtazamo wangu, Sitta ni dhahiri hajazungumza bila ya ruksa ya Mwakyembe, lakini kama walitaka kufikisha ujumbe waliokusudia, basi Sitta angejaribu kuwa na busara kidogo na kukwepa kutoa tafsiri yake juu taarifa za madktari wa india, mfano kuepuka kutumia maneno “amelishwa sumu”, na badala yake kutumia maneno kama vile, Dr. Mwakyembe “anasumbuliwa na maradhi yatokanayo na sumu kuingia mwilini”; au Maradhi ya Dr. Mwakyembe “yanatokana na sumu na kuna mkono wa mtu katika hilo ” au, Dr. Mwakyembe alishatoa taarifa nyingi kwa polisi kwamba anatishiwa maisha yake lakini hakuna lililofanyika, na sasa imefikia hatua ya kuugua kutokana na sumu kumwingia mwilini…., hivyo ni wasaa sasa wa Serikali kutoa tamko lake kwa kufuatana na taarifa iliyo ipokea kutoka kwa madaktari wa India.

Maswali muhimu ya kujiuliza ni je:

1. Je, taarifa za uchunguzi wa madaktari kutoka India, ambazo zipo Wizara ya Afya, zimetumia neno “amelishwa sumu” au zimetamka tu kwamba “alipata contact na sumu?”

2. Je, alichokana Waziri Nahodha ni maneno ya Sitta kwamba “Mwakyembe amelishwa sumu”, kwa maana ya kwamba taarifa kutoka india hazijatumia maneno hayo ingawa zinaelezea maradhi yatokanayo na sumu kuingia mwilini?

3. Je, taarifa zilizopo Wizara ya Afya ni zile zile ambazo Sitta anasema kwamba Polisi tayari wanazo? au Sitta na Mwakyembe walipeleka Polisi taarifa za ziada?

4. Je, katika uchunguzi wao, DCI (Polisi) wametumia taarifa zilizopo Wizara ya Afya ambazo hadi sasa hatujui kama zimetumia maneno ‘Mwakyembe amelishwa sumu? au Polisi (DCI) wametumia taarifa nyingine walizopokea zenye maneno “Mwakyembe amelishwa sumu, na kisha kutumia tuhuma hizi kwenda Wizara ya Afya kuangalia faili kutoka India lina maelezo ya namna gani”?

5. Na je, kutokana na Wizara ya Afya kutoa ushirikiano na DCI, hivyo kupelekea taarifa ya DCI kwamba hakuna ushahidi Mwakyembe “amelishwa sumu”, je ni sahihi kutafsiri kwamba, matokeo ya uchunguzi wa DCI ambayo yamefanikiwa kutokana na ushirikiano wa Wizara ya Afya ambayo moja kwa moja ni Serikali Kuu, je ina maana kwamba sasa huu pia ndio msimamo/majibu/maelezo rasmi ya serikali kuhusu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe? Tusisahau Waziri Mkuu alishasema serikali haitatoa maelezo kuhusu nini kinamsibu Dr. Mwakyembe kwani ni unethical, hiyo kazi ni ya mgonjwa mwenyewe.

Mwisho, Mwakyembe ni mwanasheria, hivyo kukaa kwake kimya ni sawa na ‘ukimuona kobe kainama, ujue anatunga sheria’. Hivyo tuwe na subira, akiwa tayari ameshazingatia legal implications, lazima atatamka tu sasa rasmi kama ‘mwathirika wa sumu’.

Vinginevyo, iwapo sasahivi Serikali inashindwa kutoa taarifa kuhusu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe, ikitokea bahati mbaya (mungu pishilia mbali) kwamba Dr. Mwakyembe anafariki, je, serikali itatoa taarifa juu ya kufariki kwa kiongozi wake? Itasema marehemu alikuwa anaugua nini?

Mkuu Mchambuzi umeangalia pande zote za suala la sumu na jinsi linavyozunguka hali ya afya ya Dr, na inaonekana kuwa kuna element moja ambayo hatuijui, yaani ripoti ya wataalamu inasema nini. Na huenda tusiijue kama Mwakyembe hataamua tuijue, unless tuwekewe hapa na wenye nayo. Kama Ripoti kutoka hospitali ya India itawekwa wazi, na kujua ni nini kimemsibu Mwakyembe basi tunaweza tukajua ni nini DCI anasema, na ni nini Nahodha alisema, na ndipo tutajua PM alikuwa na maana gani aliposema kuwa serikali haitatoa taarifa kuhusu ugonjwa wa Mwakyembe. Na Kwanini Manumba amesema hayo ambayo yanaonekana kuwa tofauti na yale aliyosema PM..

Lakini kwa watu wanaojua (naamini wewe ni mmoja wapo) uchunguzi wa suala kama la ugonjwa wa Mwakyembe hauwezi kufanywa kirahisirahisi na CID na MOH peke yake [Kumbuka uchunguzi wa kifo cha Livtinienko na polonium 210], na majibu yake kwa umma hayawezi kutolewa kirahisi rahisi namna hiyo, bila kusema ni hatua zipi zilifuatwa, ni nini kimeonekana, na kutokana na kilichonekana DCI amefikia hatua ya kuamini kuwa Mwakyembe haumwi na hakupewa sumu. Kuangalia faili walilonalo wizara ya afya, (ambalo inasadikiwa kuwa tayari yaliyomo ndani yake anayo mtoto mmoja wa kigogo) peke yake haitoshi kumfanya DCI kusema hakulishwa sumu.

Pamoja na kuwa baadhi ya watu hapa wanamshutumu Sitta kuwa hasemi kweli, is it true kuwa Sitta hasemi kweli? yeye alikwenda India kumwona Dr Mwakyembe, can he lie to us about what is happening with Dr's health? why would he do so. Ukiangalia accounts zote za suala la afya ya Dr sidhani kama yanaysemwa na PM, Waziri mambo ya ndani, DCI yanajitosheleza, hata aliyosema Sitta hayajitoshelezi.

Lakini kama si sumu serikali inatakiwa kutuambia ni ugonjwa gani na vipi tujikinge dhidi ya ugonjwa huo, na sio kusema tuwe waangalifu na glasi zetu za maji.

Serikali yetu iko wazi sana mtu akifa. Tutakachosikia ni kuwa "alikuwa mchapakazi, mwenye kupenda taifa lake, aliyesimama kidete kukitetea chama cha mapinduzi na sera zake, mzalendo Mungu aiweke roho yake pema peponi"

Inaonekana kuwa kuelekea 2015 siasa chafu na za mambo ambayo hayaelezwi zitaendelea kutokea, na kundi la wachafu ni kama litanedelea kutumia mbinu chafu. definatley kilichopo ni umafia dhidi ya potential candidates wa 2015, ni wale ambao ni front runners ndio wanafanyiwa mchezo.
 
Nadhani huu ndio ikweli wenyewe!. Kibarua sasa kimebaki kwa Mhe. Mwakyembe mwenyewe ku disclose anaumwa nini!.

Get well soon Mwalimu Mwakiyembe na achana na michezo michafu, rudi darasani ukaiendeleze fani ya kufinyanga wakombozi wa mahakamani.
Pasco,Mwakyembe na Mkewe wanataka kumuona Mwingira kwa maombi tusaidie utaratibu
 
Hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari mchana wa leo. Katika maelezo yake, DCI anasema kwamba:

"Kutokana na uchunguzi wa kipolisi ulioshirikisha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hakuna ushahidi juu ya hilo".

Alipoulizwa na waandishi wa habari:

Je, Dr. Mwakyembe anasumbuliwa na maradhi gani?

DCI alijibu kwamba:

"Kazi ya Jeshi la Polisi sio kuchunguza maradhi bali kuchunguza tuhuma, na baada ya uchunguzi wake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi limebaini kwamba tuhuma kwamba Dr. Mwakyembe amelishwa sumu hazina ukweli
."
Inawezekana Dci akawa sahihi.Mwakyembe hajalishwa sumu ila amekula mwenyewe sumu ya kuambukiza!
 
Pasco,Mwakyembe na Mkewe wanataka kumuona Mwingira kwa maombi tusaidie utaratibu
Mkuu Mwamakula, kwanza poleni kwa yote!.

Kwanza mimi sio mfuasi wa Mtume na Nabii Mwingira japo nimeshashiriki maombi pale kanisani kwake kama nilivyoshiriki kwa Gwajima ambako Mwakyembe ameshashiriki pia.

Kwenye TV namuona Mwingira uwezo wake ni kutibu maradhi yanayotokana na nguvu za giza tuu.

Mimi ni muumini mkubwa wa "will power" ambayo ni powers from within!. Akirudi toka India nitamtembelea kumpatia hii concerpt ya 'will'.
 
Yani spati picha Mwakyembe angekua ni Demu.. Hana msimamo...
 
Mchambuzi;3345787]Maswali muhimu ya kujiuliza ni je1. Je, taarifa za uchunguzi wa madaktari kutoka India, ambazo zipo Wizara ya Afya, zimetumia neno "amelishwa sumu" au zimetamka tu kwamba "alipata contact na sumu?"
Taarifa za kitaalamu huandikwa kwa weledi na umakini wa hali ya juu. Ni wazi kuwa Madaktari waliomtibu walielewa wazi kuna uwezekano wa uchunguzi wa kitaalamu kuthibitishwa katika vyombo vya sheria kama 'Forensic examination results' taarifa ingeeleza kilichoonekana na kilichotokea na sio kilichosikika.Ingawa sijaiona taarifa na sijui kama ipo au la,nakuhahkikishia kuwa neno'kalishwa sumu' halipo, na kama lipo basi litabadilisha mwenendo mzima wa taarifa ya DCI na Mwakyembe anaweza kulitumia vema akipenda
2. Je, alichokana Waziri Nahodha ni maneno ya Sitta kwamba "Mwakyembe amelishwa sumu", kwa maana ya kwamba taarifa kutoka india hazijatumia maneno hayo ingawa zinaelezea maradhi yatokanayo na sumu kuingia mwilini?
Nahodha amelijibu kisiasa kwasababu yeye kama waziri alisimama kutetea serikali kwa kumnukuu Sitta na si taairifa ya madaktari. Alichokisema ni kupooza hali ya kisiasa iliyoonekana wazi kuelemea serikali. Ushahidi wa hayo ni maneno ya PM na waziri waliokataa kuzungumzia hali ya Mwakyembe. Ikiwa nahodha alikuwa na taarifa za kuthibitika PM na waziri wake wasingebababika. Lakini pia, taarifa ya nahodha iilikiuka kanuni za uchunguzi. Yeye kama waziri wa mambo ya ndani hakupaswa kutoa taarifa wakati uchunguzi haujakamilika. Hakuna shaka kuwa taarifa ya DCI ilifuata maelezo ya bosi wake, na ndiyo maana uchunguzi wote unapoteza maana halisi.
3. Je, taarifa zilizopo Wizara ya Afya ni zile zile ambazo Sitta anasema kwamba Polisi tayari wanazo? au Sitta na Mwakyembe walipeleka Polisi taarifa za ziada?
Mwakyembe na Sitta sio tu ni wasomi waliobobea katika sheria bali pia ni weledi wa serikali pamoja na mahasimu wao. Isingewezekana wao kusema taarifa ipo Polisi kama haikuwepo. Polisi hawajakana uwepo au kutokuwepo kwa taarifa hizo. Kama ni uongo Polisi ambao wanatumikavema na makundi hasimu ya kisiasa wangeshachukua hatua. Mahasimu wao wangetumia hiyo window of opportunity kuwamaliza kisiasa. Taarifa ipo swali ni ipi hiyo?
4. Je, katika uchunguzi wao, DCI (Polisi) wametumia taarifa zilizopo Wizara ya Afya ambazo hadi sasa hatujui kama zimetumia maneno ‘Mwakyembe amelishwa sumu? au Polisi (DCI) wametumia taarifa nyingine walizopokea zenye maneno "Mwakyembe amelishwa sumu, na kisha kutumia tuhuma hizi kwenda Wizara ya Afya kuangalia faili kutoka India lina maelezo ya namna gani"?
DCI anafanya kazi kwa ukaribu sana na Polisi na DPP. Kunapokuwa na utendaji wa hisia kama tunaouona kuna tia shaka kuhusu suala zima la uchunguzi. Inaonekana DCI na Polisi hawakufanya uchunguzi juu ya uhalifu bali walifanyia kazi maneno ya Sitta. Hapa uchunguzi upo wapi na maana nzima ya uchunguzi imeangaliwaje. Hawakufanyia kazi tuhuma za uhalifu bali tuhuma zenye maneno ya uhalifu!
5. Na je, kutokana na Wizara ya Afya kutoa ushirikiano na DCI, hivyo kupelekea taarifa ya DCI kwamba hakuna ushahidi Mwakyembe "amelishwa sumu", je ni sahihi kutafsiri kwamba, matokeo ya uchunguzi wa DCI ambayo yamefanikiwa kutokana na ushirikiano wa Wizara ya Afya ambayo moja kwa moja ni Serikali Kuu, je ina maana kwamba sasa huu pia ndio msimamo/majibu/maelezo rasmi ya serikali kuhusu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe? Tusisahau Waziri Mkuu alishasema serikali haitatoa maelezo kuhusu nini kinamsibu Dr. Mwakyembe kwani ni unethical, hiyo kazi ni ya mgonjwa mwenyewe
DCI anateuliwa na rais. Kama taairifa yake haitakuwa ya serikali basi anapaswa kujiuzulu mara moja kwasababu hawajibiki kwa mamlaka zake. Kabla hajatoa taarifa ni wazi aliwasiliana na IGP, Nahodha, PM na Ofisi ya Rais. Kwa mantiki hiyo hii ni taarifa ya serikali bila ubishi hadi hapo atakapojitokeza kiongozi mkubwa kimamlaka kwa DCI atakayekanusha habari hiyo
Vinginevyo, iwapo sasahivi Serikali inashindwa kutoa taarifa kuhusu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe, ikitokea bahati mbaya (mungu pishilia mbali) kwamba Dr. Mwakyembe anafariki, je, serikali itatoa taarifa juu ya kufariki kwa kiongozi wake? Itasema marehemu alikuwa anaugua nini?
Waziri mkuu amesema anayepaswa kutoa taarifa kwa mintaarafu ya ethics ni Mwakyembe. Ethics hizo zinaweza kutumika kama zilivyotumika kwa Gavana Bilal ambaye ametuacha na kitendawili. Mungu pishilia mbali Dr arejee kazini.
 
Kazi imebakia kwa Sitta sasa kusema yote måna lazima haya maneno yake aliyasikia kwa swaiba wake Mwakyembe
 
Kwa mtazamo wangu ambao unaweza kuwa finyu, ili kubaini kauli ya Manumba ina background gani, ni vizuri tukaangalia sequence of events pamoja na kauli mbalimbali kama ifuatavyo:

· Rais Kikwete katikati ya mwaka 2011 alitamka kwa masikitiko kwenye TV kwamba – “hali ndani ya CCM imefikia hatua mbaya kiasi kwamba watu hawa aminiani tena, na hauwezi kuacha glasi yako ya maji ovyo ovyo….”

· Baada muda mrefu kufuatia kauli hii ya Rais, Mwakyembe akabainika anasumbuliwa na ugonjwa wa ajabu wa ngozi. Mwakyembe akaenda India lakini bila ya kutoa tamko lolote kuhusu kunyweshwa sumu.

· Wakati Mwakyembe akiwa India, miezi kadhaa, Sitta katika kipindi cha Dakika 45 kwenye ITV akatamka kwamba amemuona Dr. Mwakyembe kabla hajaenda India kuchunguzwa afya yake, na dhahiri Dr. Mwakyembe “amelishwa sumu”, kwani mwili wake umebadilika ghafla, unaota magamba, nywele mwilini zina momonyoka, na ngozi inapukutika kama unga….; Hili likawa tamko la kwanza la kiongozi wa serikali kwamba Dr. Mwakyembe amelishwa sumu. Lakini bado mwathirika mwenyewe (mwakyembea) alikuwa hajatoa tamko lake la kuhusisha maradhi yake na sumu.

· Mwakyembe akarudi kutoka India, na kusema kwamba anamshukuru Mungu amepona, na kwamba taarifa juu ya ugonjwa wake zimepelekwa serikalini. Lakini bado hakutamka lolote kuhusu sumu.

· Wiki kadhaa zilizopita, wakiwa pamoja katika ibada moja Viwanja vya Tanganyika Packers, Sitta akatangaza mbele ya umati kwamba Mwakyembe amelishwa sumu, na kwamba madaktari india wamesema ni bahati sumu haikwenda kwenye moyo, figo wala maini, bali ilitoka nje, ndio maana ngozi yake ikapata madhara husika. Sitta akasema pia kwamba Serikali ina taarifa zote juu ya hili na kama inataka kupingana nae, basi ielezee umma nini kimemsibu Dr. Mwakyembe. Kwa upande wake, Dr. Mwakyembe katika ibada ile, hakusema lolote kuhusu kulishwa sumu, zaidi ya kushukuru kwamba sasa amepona, Mungu atalipa, na kuomba wahumini wamwombee pia Professor Mwandosya na yeye apone.

· Baada ya tamko la Sitta kuhusu Mwakyembe kulishwa sumu, na kwamba serikali ina taarifa, Waziri Nahodha akakanusha madai ya Sitta – kwamba Wizara yake haina taarifa hizo. Nadhani Nahodha alikuwa sahihi kwa sababu maneno ya Sitta ni kwamba Serikali ina taarifa kwamba “Mwakyembe amelishwa sumu.”; hii ni tofauti na kusema “serikali ina taarifa kwamba ugonjwa/maradhi yanayomsumbua Dr. Mwakyembe yanatokana na kuwa in contact na sumu kwa namna moja au nyingine. Binafsi, sidhani ripoti kutoka India inasema ‘Mwakyembe amelishwa sumu”, ingawa lazima inasema ugonjwa wake umetokana na sumu.

· Lakini Sitta akapingana na Nahodha na kusema kwamba taarifa kuhusu kulishwa sumu kwa Dr. Mwakyembe tayari zipo mikononi mwa polisi siku nyingi. Mpaka hapo, bado Dr. Mwakyembe alikuwa hajatoa tamko lake kuhusu kulishwa kwake sumu.

· Pia ni muhimu kusema hapa kwamba – Waziri Mkuu Pinda na Katibu Mkuu Afya Blandina Nyoni, katika nyakati tofauti waliweka bayana kwamba serikali haiwezi kutoa maelezo kuhusu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe kwani ni ‘unethical’, hivyo ni wajibu wa mgonjwa mwenyewe. Bado Dr. Mwakyembe hakakaa kimya.

· Leo, DCI Manumba akatoa taarifa ambazo sote sasa tunazifahamu. Kwa kauli ya Manumba, upelelezi wa kipolisi ulilenga kuchunguza maneno kwamba “amelishwa sumu”, sio vinginevyo. Kama taarifa za uchunguzi wa madaktari wa India hazijatumia maneno “Mwakyembe amelishwa sumu”, Maelezo ya DCI Manumba yanasimama kuwa sahihi kwani kwa maana hii basi, walichofanya DCI ni kuchanganya taarifa walizopokea kutoka vyanzo tofauti juu ya tuhuma kwamba mwakyembe “amelishwa sumu”, pamoja na taarifa zilizopo Wizara ya Afya, kutoka India. Na huu ndio msingi wa Manumba kutamka kwamba, kazi ya Polisi ni kuchunguza tuhuma, sio maradhi, na yupo sahihi katika hilo.

My assumption:
DCI alikuwa na taarifa kutoka chanzo kingine zinazosema “Mwakyembe amelishwa sumu”, hivyo DCI alifanya uchunguzi kuhusu “kulishwa sumu”, na sio vinginevyo. Na baada ya DCI kufanya uchunguzi uliotokana na ushirikiano wa karibu na Wizara ya Afya, DCI amebaini kwamba taarifa za “kulishwa sumu”, hazilingani na maneno yaliyopo kwenye faili lililopo Wizara ya Afya. Inawezekana kabisa Madaktari India wameweka wazi kwamba tatizo ni uwepo wa sumu mwilini, lakini hawajatumia neno “amelishwa sumu”, na ndio maana alichokichunguza Manumba ni “TUHUMA” kwamba “Mwakyembe amelishwa sumu”, SIO taarifa au tuhuma kwamba “Mwakyembe amenusishwa sumu, amepuliziwa sumu, kanawia maji au sabuni yenye sumu, amepata contact na sumu kutokana na mkono wa mtu n.k. Ni hali hii ndio inanipelekea kuamini kwamba Manumba amefanya kazi yake kwa usahihi kabisa, hivyo tusipoteze muda kuhoji kauli yake.

Ni dhahiri kwamba Dr. Mwakyembe ana tatizo lisilo la kawaida, na uwezekano mkubwa ni kwamba maradhi yale yanatokana na sumu. Natumia neno ‘uwezekano mkubwa’, kwani bado Mwakyembe hajatueleza. Kwa mtazamo wangu, Sitta ni dhahiri hajazungumza bila ya ruksa ya Mwakyembe, lakini kama walitaka kufikisha ujumbe waliokusudia, basi Sitta angejaribu kuwa na busara kidogo na kukwepa kutoa tafsiri yake juu taarifa za madktari wa india, mfano kuepuka kutumia maneno “amelishwa sumu”, na badala yake kutumia maneno kama vile, Dr. Mwakyembe “anasumbuliwa na maradhi yatokanayo na sumu kuingia mwilini”; au Maradhi ya Dr. Mwakyembe “yanatokana na sumu na kuna mkono wa mtu katika hilo ” au, Dr. Mwakyembe alishatoa taarifa nyingi kwa polisi kwamba anatishiwa maisha yake lakini hakuna lililofanyika, na sasa imefikia hatua ya kuugua kutokana na sumu kumwingia mwilini…., hivyo ni wasaa sasa wa Serikali kutoa tamko lake kwa kufuatana na taarifa iliyo ipokea kutoka kwa madaktari wa India.

Maswali muhimu ya kujiuliza ni je:

1. Je, taarifa za uchunguzi wa madaktari kutoka India, ambazo zipo Wizara ya Afya, zimetumia neno “amelishwa sumu” au zimetamka tu kwamba “alipata contact na sumu?”

2. Je, alichokana Waziri Nahodha ni maneno ya Sitta kwamba “Mwakyembe amelishwa sumu”, kwa maana ya kwamba taarifa kutoka india hazijatumia maneno hayo ingawa zinaelezea maradhi yatokanayo na sumu kuingia mwilini?

3. Je, taarifa zilizopo Wizara ya Afya ni zile zile ambazo Sitta anasema kwamba Polisi tayari wanazo? au Sitta na Mwakyembe walipeleka Polisi taarifa za ziada?

4. Je, katika uchunguzi wao, DCI (Polisi) wametumia taarifa zilizopo Wizara ya Afya ambazo hadi sasa hatujui kama zimetumia maneno ‘Mwakyembe amelishwa sumu? au Polisi (DCI) wametumia taarifa nyingine walizopokea zenye maneno “Mwakyembe amelishwa sumu, na kisha kutumia tuhuma hizi kwenda Wizara ya Afya kuangalia faili kutoka India lina maelezo ya namna gani”?

5. Na je, kutokana na Wizara ya Afya kutoa ushirikiano na DCI, hivyo kupelekea taarifa ya DCI kwamba hakuna ushahidi Mwakyembe “amelishwa sumu”, je ni sahihi kutafsiri kwamba, matokeo ya uchunguzi wa DCI ambayo yamefanikiwa kutokana na ushirikiano wa Wizara ya Afya ambayo moja kwa moja ni Serikali Kuu, je ina maana kwamba sasa huu pia ndio msimamo/majibu/maelezo rasmi ya serikali kuhusu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe? Tusisahau Waziri Mkuu alishasema serikali haitatoa maelezo kuhusu nini kinamsibu Dr. Mwakyembe kwani ni unethical, hiyo kazi ni ya mgonjwa mwenyewe.

Mwisho, Mwakyembe ni mwanasheria, hivyo kukaa kwake kimya ni sawa na ‘ukimuona kobe kainama, ujue anatunga sheria’. Hivyo tuwe na subira, akiwa tayari ameshazingatia legal implications, lazima atatamka tu sasa rasmi kama ‘mwathirika wa sumu’.

Vinginevyo, iwapo sasahivi Serikali inashindwa kutoa taarifa kuhusu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe, ikitokea bahati mbaya (mungu pishilia mbali) kwamba Dr. Mwakyembe anafariki, je, serikali itatoa taarifa juu ya kufariki kwa kiongozi wake? Itasema marehemu alikuwa anaugua nini?
Mkuu Mchambuzi, nimependa unavyochambua, ki ukweli unazama deep!.
Nimeupitia uchambuzi wako kuna kitu sijakiona ukikizungumza kuhusu sumu.
Kuna sumu za aina tatu,
1. Intentions or delibarate poisoning, hii ndio ile dhana ya mtu kulishwa sumu, kutiliwa, kushikishwa au hata kutumiwa kwa barua kama 'anthrax', hii ni mtu kupewa sumu be it first poisoning or slow poisoning ila mwisho wa siku mhusika hudhurika!.
2. Food poisoning, hii ni aina ya pili ya sumu ambayo hutokana na kula chakula chenye sumu, mfano kuna baadhi ya mihogo ina sumu, uyoga, na baadhi vya vyakula vya proteion in nature kama nyama, samaki, maziwa, mayai etc ambapo aliyekula vinamdhuru ama instantly kwa kupata rushes, kuwashwa au kupata mafindofindo wanaita 'alergy' au slow reaction ambapo inaibuka baada ya kipindi kirefu na ineweza kuibuka kama kansa etc!.
3. Medical Reaction, japo sumu zote ni chemical reaction, hii sumu ya medical reaction ni sumu inayotokana na reaction ya madawa fulani fulani kwenye mwili wa binadamu mostly kutokana na prolonged use!. Hii humpata mtu ambaye kuna kitu ameugua na ni ugonjwa wa muda mrefu, mtu huyo anakuwa anatumia combination ya madawa fulani kwa muda mrefu imefikia muda madawa hayo yamereact from each other na kugeuka sumu na wakati huo huo mwili unakuwa umetengeza 'antigen' za kukabiliana na hiyo reaction na matokeo huwa ndiyo kama hiyo hali ya Mwakiyembe!.

Wanabodi nilishauri huko nyuma na hapa nashauri tena, tupunguze conspiracy theories tusubiri tamko la Mwakiyembe mwenyewe!.

Japo naye ili kumlindia Sitta heshima, anaweza kusema "Nimesha Muachia Mungu, hivyo naomba nisizungumze chochote"! hivyo kutosema anaumwa nini!.
 
Back
Top Bottom