Wanajamvi,
Nchi hii tunafikishwa pabaya muda si mrefu. Hivi kuna shida gani ktk serikali yetu hii? Kwanini kila inapokuja na tamko la tatizo au shida fulani, yaani majibu yake huwa ni tatizo kubwa zaidi au huongeza shida hiyo kuwa kubwa zaidi kuliko tatizo au shida yenyewe? Huko Nyuma niliwahi kusema, tumefika kipindi ambapo sijui tunaviongozi gani sijui, ambao, kila solution ya tatizo wanalotoa huwa ndio tatizo kubwa zaidi. Sasa kwa hili la DCI, limezua tatizo kubwa zaidi badala ya kulipunguza.
Kwanini nasema hivyo:
1. Ripoti ya Madaktari wa Apollo, ilionyesha kuwa Dr, Mwakyembe mwili wake umeathirika na sumu, tena sumu mbaya, tena ni sumu ambayo haipatikani kirahisi, kama hizi za kuulia Panya, au zile za ndugu zake wa Mbeya wanazopiga kwenye Mikahawa. Ni sumu hatarishi sana ambayo upatikanaji wake na mpaka mtu awe na access nayo, basi ni lazima kuwe na kazi ya ziada imefanyika. Na ripoti ikaonyesha Dr. ameathirika na sumu hiyo. Ripoti ikaenda mbali, kuonyesha ni namna gani sumu hiyo inaweza kumpata mtu. Kwa vile ni sumu kali sana basi mtu anaweza kuathirika kwa kuivuta, kuigusa, kunywa, au hata kutumia kitu kilichowekwa sumu hiyo kali. Ripoti hiyo, ilionyesha pia estimation ya time ambayo muathirika anaweza kuwa alikutana na sumu hiyo kwa mara ya kwanza, kitu ambacho kingeweza kusaidia ku narrow down kwa ratiba za Dr. na Kujua possible areas ambazo DR. alikuwepo na kupata tatizo hilo.
2. Kwa vile Dr. ni Kiongozi wa Serikali tena wa kuteuiwa na Rais, na kukabidhiwa mikoba ya siri za Serikali, kulikuwa na utata mkubwa kuwa, kiongozi huyu wa Serikali amekutana wapi na sumu hii kali? Hivyo basi, jukumu likawa kwa ripoti ile kuletwa Serikalini ili Serikali ifanya uchunguzi wake ni vipi mteule huyu wa Rais ameathirika na sumu hiyo. Kwanza kwa kuchuchunguza simu hiyo inawezapatikana wapi, na possible areas ambazo Dr alikuwepo na angeweza kukutana na tatizo hilo. Ndio maana, kwa vile Dr. alijua uzito wa suala lenyewe na kwa vile yeye ni mteule wa Rais, akaona ni vyema aiachie Serikali ifanye kazi yake kwani ndio wajibu wake. Ukiunganisha na malalamiko ambayo Dr. Mwakyembe alikuwa ameshayatoa ktk jeshi la Polisi kuhusiana na mpango wa mauaji juu yake na viongozi wengine, kukawa hakuna ubishi kuwa na hili la sumu ni mbinu zilezile, ndio maana Dr. akawaachia Polisi na hasa Serikali ndiyo ifanye uchunguzi na kumjulisha Dr wabaya wake.
3. Cha kushangaza na kwa mastaajabu makubwa, nadhani hata Dr. Mwakyembe mwenyewe atakuwa ameshanga ni hiyo taarifa ya DCI kuhusu sakata hilo. Taarifa ya DCI inamtwika mteule wa Rais kuwa yeye mwenyewe ndiye anajua amepata wapi hiyo sumu kali, ambayo si rahisi kupatikana kwa mtu wa kawaida, na yeye mwenyewe ndiye labda amejidhuru, kitu ambacho nadhani kinaleta mkakanyiko mkubwa, na kama nilivyosema, kinazua tatizo kubwa zaidi.
4. Sakata hili, linazidi kutuonyesha mpasuko mkubwa ktk serikali yetu, kuwa hata vyombo vya usalama tunavyovitegemea, navyo vimepasuka vipande vipande na kila upande unasema na kufanya litakalo, kitu ambacho ni mwisho mbaya ninao uzungumzia utatukuta muda si mrefu sisi watanzania.
5. Labda nimkumbushe tu DCI kuwa, historia itakuja muhukumu na kuwa yeye ni mtaalamu wa masuala ya upelelezi na si mtalaamu wa field nyingine kama vile Human Psychology. DCI lazima akumbuke, anafanya kazi ktk jamii ya watanzania ambao wamebobea ktk fani mbalimbali, na si mbumbumbu, na kufikiri ni watu wa kukubali kila kitu. Watanzania wa leo na jinsi dunia ya leo ilivyo ktk kiganja, huwezi kuwadanganya kwa kauli zisizo na mshiko, kichwa wa miguu.
6. Sasa tusubiri tamko la kutoka upande wa Dr. Mwakyembe, na mtakubaliana nami hayo niliyoyasema hapo juu.
Source: Personal analysis ya mambo yanavyokwenda Tanzania kwa sasa na hasa Sakata zima la Dr. Mwakyembe.