Inayojiuza ni bar au watu? kwanini wasiwakamate wanaojiuza? kwanini na ile mitaa maarufu ya machangudoa isifungwe? mwenye bar akisema ni chuki binafsi DC atakataaje?
Kaka hawa viongozi wana mihemko na wala hawajui misingi ya Biashara, huwezi kisema mtu afunge Biashara yake bila kupata misingi na undani wa hiyo Biashara, Huyo mtu aliomba kibali cha kuuza pombe na akapewa, sasa habarimza hao Malaya yeye zinamuhusu nini?, yeye anauza Malaya?
Cha pili, huwezi kumwambia mtu afunge Biashara zake bila kujua status ya hiyo Biashara, Huyo mkuu wa Wilaya anajua capital ya hiyo Biashara imetoka wapi?, kama ni Bank je atalipaje deni huku kafungiwa biashara bila kufata sheria?
Je Mkuu wa Wilaya anajua hiyo Bar ina wafanyakazi wangapi na wanalipwa mshahara kiasi gani?, je wataendeshaje maisha yao ikiwa hakuna kazi?
Je TRA inapoteza kiasi gani cha mapato kwa hiyo Bar ikifungwa?
Vipi kuhusu viwanda vya Bia, Soda, Maji? Vipi watu wa tax, bodaboda, Bajaji?
Cha mwisho, je hao Malaya wakiamia Bar zingine nazo zitafungwa?