MAHOJIANO MAHAKAMANI YATAKUWA HIVI:
WAKILI: Unaweza kuiambia mahakama umri na elimu yako?
DC: Nina umri wa miaka 29. Nimesoma hadi darasa la saba na kisha nikajiendeleza hadi ngazi ya cheti katika chuo cha chama Kivukoni.
WAKILI: Je, kuna sheria yoyote inayoharamisha biashara ya kuuza uchi katika nchi hii?
DC: Hapana
WAKILI: Kama ndivyo, je wauza uchi wakikamatwa na polisi hufunguliwa kesi gani?
DC: Hufunguliwa kesi ya uzururaji.
WAKILI: Je, mliwahi kumkamata mmiliki wa bar hii ndugu (anamtaja jina) akizurura na mlimchukulia hatua gani?
DC: Hapana. Hatujawahi kumkamata akizurura, hivyo hatuwezi kumfungulia mashtaka.
WAKILI: Unaweza kuiambia mahakama huyu mteja wangu mmefikisha hapa kwa kosa gani la jinai alilotenda?
DC: Tumemfikisha mahakamani kwa kuwa tulikuta watu wakizurura kwenye bar yake.
WAKILI: Kwanini hamkuwakamata wao badala ya kumkamata mmiliki wa bar?
DC: (huku akikuna kichwa) KIMYA!!!!!!!!!!
WAKILI: Je, ni nani mwenye jukumu la kuwakamata na kuwafungulia mashtaka wazururaji?
DC: Ni polisi na kisha kuwafikisha mahakamani.
WAKILI: Nikikuambia kwamba elimu yako ni ya kutiliwa mashaka sawa na ya ndugu Bashite nitakuwa nimekosea?
DC: Utakuwa sahihi kabisa mheshimiwa. Unachosema ni........
....INTERUPTION....wakili wa serikali anasimama na kumzuia DC asiendelee kujibu swali hilo lakini wakili wa utetezi anapinga na mahojiano yanaendelea.....
WAKILI: Je, kuna kifungu chochote kinachotamka kwamba mtu anaweza kushtakiwa na kufungwa kwa kosa au makosa yaliyotenwa na mtu au watu wengine?
DC: Hapana.
Maswali kutoka upande wa utetezi yanafungwa na baada ya siku tano hakimu anasoma hukumu.
*********************************************
HAKIMU: Baada ya kupitia hoja za pande zote mbili nimejiridhisha kwamba mtuhumiwa hana kosa lolote kisheria hivyo upande wa mashtaka (DC na wapambe wake) wanaamriwa kulipa gharama za kesi, pamoja na fidia ya Tsh 1.2 bilioni kwa kuvuruga biashara ya ndugu (anamtaja jina).
Koooooooooooooooooti!!!!!!!!!!!!!!!!