DC Hapi aagiza baa maarufu Jijini Dar, Corner bar ifungwe!

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,666
22,674
Dar es Salaam. Baada ya malalamiko kuzidi kutokana na kuwapo biashara zisizo rasmi katika baa maarufu ya Corner, sasa baa hiyo imeamriwa kufungwa.

Akiwa katika ziara ya kawaida leo (Jumamosi) mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza Ofisa Biashara wa Kinondoni, Mohamed Nyasama kuifunga baa hiyo.“Hatuwezi kuvumilia vitendo hivivikaendelea kufanyika huku tukiwa kimya...

Natoa agizo kesho nendeni kaifungieni hiyo baa kwa kuwa inakiuka maadili,”amesema Hapi.

Hata hivyo Nyasama amesema walishaitoza baa hiyo faini ya Sh 300,000 kwa kosa hilo.“ Mkuu hii baa ni sugu, nimeahawahi hata kuipiga faini na bado imeendelea na utaratibu huo huo wa kuruhusu kina dada kujiuza.

Kwa amri yako mkuu naanza taratibu za kuifungia leo, hadi kufikia keshoitakuwa tayari,” amesema.

Chanzo: Mwananchi

img_20170225_203946-jpg.474544
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom