DC Gondwe atoa onyo kali kwa Madereva walevi, Wananchi Wazo waomba Barabara itanuliwe

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
2,011
4,165
Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Godwin Gondwe ametoa onyo kali kwa madereva wanaondesha magari huku wakiwa wamelewa.

DC Gondwe ameyasema hayo wakati alipokuwa akiongea na wananchi wanaoishi eneo la Wazo Hill na Madale alipotembelea eneo hilo kutokana na ajali mbaya iliyotokea jana asubuhi na kusababisha kifo cha mtu mmoja huku wengine wakijeruhiwa vibaya

” Siku za wikiendi unatokea uharibufu mkubwa wa miundombinu za barabara na maisha ya watu yanapotea hivyo wito wangu kwa madereva wasiendeshe magari wakiwa wamelewa, na tayari kamanda kashaanza ukaguzi na ameongeza askari wa kutosha kwa ajili ya ukaguzi wa magari barabarani,” DC Godwin Gondwe

Aidha Gondwe amewaomba wananchi wa eneo hilo kuwa watulivu wakati Serikali inajiandaa kupanua barabara hiyo ili kuepusha ajali za mara kwa mara zinazohusishwa na magari ya kiwanda cha Twiga Cement.

DC Gondwe ameambatana na Meneja wa Tanroad ambapo amemtaka achukue maoni na maombi ya wananchi wa Wazo ya kuomba kutanuliwa kwa barabara hiyo ayapeleke Serikalini ili aweze kuingiza barabara hiyo kwenye bajeti inayokuja.

Aidha mwenyekiti wa kamati ya dharura iliyoundwa kutokana na ajali ya jana ndugu Charles Kimworo amesema kwamba baada ya kamati ya dharura kukaa na kujadiliana wanaiomba serikali kutoa tamko kwa Uongozi wa kiwanda cha Twiga Cement ili malori ya kiwanda hicho yaanze kutumia barabara mbadala ambayo ipo nyuma ya kiwanda hicho kuepusha foleni na ajali za mara kwa mara kwani barabara ya Wazo Hill kwa sasa wanatumia wananchi wengi pamoja na magari makubwa na mabasi yanayoelekea mikoa ya kaskazini.

358526A1-FF2B-4015-BB95-C5C5C3C15BF1.jpeg


Wajumbe wa Kamati ya Dharura wakiwa Katika picha ya pamoja.
FAB2505C-A11D-4FEF-80BE-9EAF2C6FF4EF.jpeg


Mkuu wa wilaya ya Kinondoni akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya kikao na wananchi wa Wazo na Madale kufuatia ajali iliyotokea Jana na kusababisha kifo na majeruhi.
 
Madale ni nyumbani kwake ana kiwanja huko akataka mtaa uitwe jina lake. Lakini mrejesho aliopigiwa hana hamu na wananchi. Wamemgomea mtaa kuitwa jina lake. Mtaa unaitwa Mama Makete.
Nafikiri bado mdaa upo wa kuifanya kazi yake kwa weledi tu hadi pale wananchi wake watakapoelewa ameonyesha mchango upi na jitihada huwa hazifichiki hayo ya majina ya mtaa ni maswala madogo sana!
 
Hii barabara ya wazo imeua sana tangu hata haijewekwa lami nzuri.

Pale Tegeta kibaoni kulikuwaga na bar imegongwa mara kibao na magari ya cement yanaposhuka mlima wa wazo.

Ajali mbaya zaidi iliwahi kutokea chini ya club ya Wazo ilimgonga bosi wa Wazo na dereva wake alikuwa jirani yangu.

Yaani suzuki zile za zamani ilipitiwa juu.

Kilichoumiza watu zaidi raia walikshambulia cement badala ya kuokoa.

Kuna jamaa mdogo wake na dereva aliyegongwa hakujua kuwa kaka yake ndiye yuko uvunguni mwa gari badala yake yeye aliungana kuiba cement.

Baada raia kumjulisha..kuwa mbona hata hushughuliki kuokoa kakako?

Jamaa alishtuka na kuziacha cement alizoiba na kukimbia nyumbani.

Ilikuwa ajali inayohuzunisha sana
 
Watanzania huwa tunamambo flani ya kudhauliana wenyewe kwa wenyewe hata uwemtenda mema kwa kiasi gani bado utapingwa nao!
Sana mtu mwenyewe DC kuna vitu vingine hapo mtalainisha lakini anapewa mtu ambaye basi tu sifa zake za ajabu ajabu tu, sie wenyewe aliyepewa hilo hata sijawahi muona japo si mbali nam ila ndiyo hivyo acha aitwe tu mtaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii barabara ya wazp imeua sana tangu hata haijewekwa lami nzuri.

Pale Tegeta kibaoni kulikuwaga na bar imegongwa mara kibao na magari ya cement yanaposhuka mlima wa wazo.

Ajali mbaya zaidi iliwahi kutokea chini ya club ya Wazo ilimgonga bosi wa Wazo na dereva wake alikuwa jirani yangu.

Yaani suzuki zile za zamani ilipitiwa juu.

Kilichoumiza watu zaidi raia walikshambulia cement badala ya kuokoa.

Kuna jamaa mdogo wake na dereva aliyegongwa hakujua kuwa kaka yake ndiye yuko uvunguni mwa gari badala yake yeye aliungana kuiba cement.

Baada raia kumjulisha..kuwa mbona hata hushughuliki kuokoa kakako?

Jamaa alishtuka na kuziacha cement alizoiba na kukimbia nyumbani.

Ilikuwa ajali inayohuzunisha sana
Ilikua huzuni sana kwake huyo kijana mwenyewe na familia yake baada ya kugundua alichokifanya wakati huo na alikua very shameful that moment 🧐
 
Back
Top Bottom